Usilogwe ukaondoka nyumbani na kwenda usipopajua kwa kigezo cha kutafuta maisha

Mkuu ukipata time na wewe shuka nondo hapa,tupate kujifunza na sisi.
 
SEHEMU YA KUMI NA SITA

Ilipoishia,,,,,,,,,,

Mara nikapigwa na kitu sjui ni nini, kuanzia hapo ndo sikujua nini kiliendea tena, nikawa nimefloot,

Endelea,,,,,,,,,,,,,,,

Nilikuja kupata fahamu nikajikuta nipo wodini, Nimelala kitandani nimetundikiwa drip, nimepigwa bandeji karibu kila mahali, Sa najiuliza nimefikaje fikaje pale ,Kumbu kumbu haziji kabisa, Naona tu manesi wanapita pita, watu wana pitapita,

Basi nesi mmoja akaja kwenye kitanda changu, akaangalia angalia ile drip, anataka kuondoka nikamuuliza, Nesi hapa ni wapi? Akasema pale ni Majengo hospital, Nimefikaje hapa? Akasema uliletwa hapa na polisi ukiwa na hali mbaya sana, basi akaondoka,

Sasa pale ndo kumbukumbu zikaanza kunijia, nikaanza kukumbuka matukio, Nikakumbuka wale vibaka, nikakumbuka nilivyokuwa napigwa, Daah machozi yakawa yananitoka, Nikakumbuka begi langu walichukua wale vibaka, mbaya zaidi lilikuwa na vyeti vyangu vyote kuanzia vya shule paka cheti cha kuzaliwa,

Ahhhah niliumia sana, nikasema sasa yote haya ni nini, kwanini yanitokee mimi, Basi nikamkumbuka Sity nikasema lait angekwepo angenisaidia, Nikakumbuka maneno ya Da J siku ile namwambia kwamba nataka kuondoka niende Arusha, alisema "Usiende huko Utakufa" Nikahisi Da J alifunuliwa yatakayokwenda kunikuta huko,

Basi nikakaa pale hospitali, kumbe polisi bado wananilinda, Wanakuja pale kitandani wananiangalia wanaondoka, Basi nikawa nasikia watu pale wodini wananong'onezana huku wananinyooshea kidole, Wanasema yule pale ni mwizi, Aliletwa hapa hafai ila saivi kapata nafuu, Moyoni nikawa naumia sana maana mi najua mi si mwizi, sema ndo hivyo nani ataniamini,

Basi badae nilikuja kufahamu kilichotokea siku ile, Kumbe wakati wanataka kunipiga kibiriti pale chini kumbe polisi wakatokea, Watu walivyoona polisi wakakimbia wakaniacha ndo ikawa ponea yangu, Kumbe kituo cha polisi cha majengo hakipo mbali na pale uwanjani kwaiyo polisi walipopata taarifa wakaja fasta, Basi nikatiwa kwenye gari yao wakanileta pale hospitali, kumbe hospitali yenyewe ilipo na pale uwanjani imetenganishwa na barabara tu,

Basi nilikaa sana pale hospitali, paka majeraha yakaanza kupona, polisi wapo tu na mimi hawaniachi, basi siku ya siku nikapewa ruhusa, basi polisi wakanichukua paka pale kituoni, Nikaandika maelezo pale badae wakanitia ndani kwenye kiselo chao pale kituoni , mzee baba maisha ya huko selo sitaki hata kuyasimulia,

Basi siku ya pili nikapandishwa mahakamani pale moshi mjini mahakama ya mwanzo, nikasomewa shitaka langu la kutaka kuiba kwa kutumia nguvu, Akaja askari mmoja wa kituo cha majengo kutoa ushahidi, akaelezea jinsi walivyopata taarifa, na jinsi walipofika pale wakanikuta napigwa, pia akasema dada ambaye nilitaka kumuibia pia walimpata na yeye akatoa maelezo yake,

Badae akaitwa dada aliyetaka kuibiwa na yeye atoe ushahidi, basi akapanda yule dada, akasema yeye alikuwa anakatiza pale uwanjani huku anaongea na simu, mara ghafla mimi nikatokea nikaanza kumkimbiza nataka kumnyang'anya simu, alipoona vile ndo ikabidi ajitetee kwa kukimbia na kupiga ukunga,

Basi na mimi nikaambiwa nijitetee na kama nina mashahidi pia nilete, Mi nikasema sina mashahidi nitajitetea mwenyewe, Basi nikaileza mahakama kila kitu, kuanzia nilipoenda pale shule, nilivyokimbizwa na wale vibaka, nilivyopigwa mpaka nilipojikuta hospitali,

Basi hakimu akasema kesi imeahirishwa mpaka kesho kwa ajili ya hukumu, kwa sasa nitaenda mahabusu ila milango ya dhamana ipo wazi, Nani sasa wa kuniwekea dhamana, ikabidi nipelekwe mahabusu gereza la Karanga lilopo pale moshi,

Mzee kwa mara ya kwanza natimba gerezani, wacha kabisa!! Siku hiyo sikulala kabisa, niliwaza mambo mengi sana, Nikakumbuka maneno ya Sity " Ebu jichunguze ni wapi ulipo mkosea Mungu", Nikakumbuka sana kijijini kwetu, Nikasema bora na mimi ningesepaga home kama Kidosho, Nikamkumbuka Happy na Mwanamgu Joyce, toka nimwone kwenye picha sijawahi kumwona tena, nikawaza saivi atakuwa mkubwa, sijui kama nitawaona tena,

Itaendelea
 
Haya maisha watu tumepitia. Inaonekana story lakini ina uhalisia sana. Ni hali inayosikitisha sana. Ndugu na marafiki wanafiki wanakutenga kipindi hiki. Hata wazazi wengine pia wanakutenga...
Hakuna kitu kibaya kama kumaliza chuo tena umesomea kozi ngumu kama hiyo afu unakosa ajira,nimejipanga kuhakikisha wanangu wasipitie hii hali kama nitakuwepo.
 
Nimesoma title na sehem yakwanza nimegundua kichwa cha habari hakiendani na maelezo ....... labda ni some kama stori tu lakini hakuna uhalisia kabisa
 
Pole Sana kaka
 
Nzuri
 
Kwanini hukwenda kuwapiga pindi madogo kama ulivyokuwa unafanya kipindi cha nyuma?
 

Chumvi imekolea mboga, kama ni sukari imekolea chai.
 
Huwezi kuona vikiendana maana hauna akili ya kufatilia jambo kabla ya kuhukumu
Sipingi stori ya mtu mkuu wala sina tabia hiyo ....katika hali ya kawaida huwezi tuambia athari za kuondoka sehemu uliyozaliwa then ukanza kutueleza maisha ya shule ...hatakama hko mbeleni alibadili lakini ameanza vibaya .....why stori itengeneze mashaka ndani ya sehem ya kwanza tu?
 
Kaka we si umekuja kusoma story yake na huwezi mpangia mtu asimuliaje anachokiamini nadhani sometimes hakuna haja ya kukosoa kitu cha mtu ambaye hukumpa kazi ya kuandika sio kwa ubaya, Story ni yake.
 
Unataka aanze kulingana ubongo ama mind itakavyo comply or contemplate. Mbona watu hamuheshimu tofauti tulizo nazo binadamu mkuu. Mie mfano mpira sipendi yaani naonaga watu wanajazana nawatani kuwa suala la kuona mwanaume mwenzangu akimeki mane namie napoteza muda hiyo jobu Sina.
Ila Sasa akija hapa like Shakira hata Kama kiingilio 10M ninayo nitaenda kumcheki MTT wa kilatino. Ama wanamieleka akina Huko Hougan na Cena wakija hapa bongo kwa show nahudhuria Kama iyo gharama naimudu.
Hujui kuwa Ana Mana gani kuanza kuelezea ivyo. Yaani Kuna logic behind so Kama huwezi Iona subiria huko mbele mkuu.
Kila mtu huwa Ana namna ya kuwasilisha kitu. Yaani umeshawahi kuwa na marafiki wa madhehebu yote ama dini ambazo sio asili ya afrika ukawauliza ni kwa Nini unasali ama kuswali ama kuabudu hapo ulipo kila mtu Ana reasons zake na ziko sawa kulingana na yeye.
Listen two men, one says impossible and onother says possible both are equal/alright.
Halafu Sasa mfano kupinga baadhi ya vitu vya maana huo ubavu hatuna. Mfano umeshawahi kuona detects zilizopo katika Newton's laws kweli. Ama Tesla alivyogundua umeme umeshawahi fanya research ukatoa andiko kuwa ni kwa Nini alianza vibaya wewe ukaweka vizuri.
Ama hizi chanjo u critize mkuu negative sides zake uje na njia mzuri ya chanjo.
Ama namna ya barabara zinavyojengwa uje na materials mbadala ya kutumia tusitumie lami Mana ghali sana.uje na option ya material simple Sana cheap ili uokoe our global Kama watu walivyokuja na magari ya umeme ili kuiokoa our global na global warming Mana tunaharibu ozone.

Sasa Kama huwezi Bora ukakaa kimya ili tupeane koneksheni na kupeana ujanja wa kula mbususu mpaka itetemeke Mana blacks hatuna zaidi ya akili ya kuichakata mbususu ili ituheshimu.

Yaani mie unakuta mtu anakuwa makini kinouma nukta kwa nukta badala hata uje na mbadala wa songaz, bandari ya bagamoyo kwa mustakabali wa Taifa letu. Ama elimu gani kizazi Cheri kipate ili kisitegemee ajira Bali waweze kujiajiri.
 
Kaka we si umekuja kusoma story yake na huwezi mpangia mtu asimuliaje anachokiamini nadhani sometimes hakuna haja ya kukosoa kitu cha mtu ambaye hukumpa kazi ya kuandika sio kwa ubaya, Story ni yake.
Utadhani akamlipa. Yaani blacks bana tuko poa Sana kufuatilia visivyotakiwa kufuatiliwa. Stori unaburika na kujifunza ama kuelimisha. Sasa hapa Kuna mtu atajikita mbona herufi umekosea ni unabudulika na sio unaburika. Mie naijua r hii l haipo kwenye jamii yangu so it's up to you kunisahisha utadhani unanilipa mie nijikite namna ya kuandika vizuri as along najua lengo langu litafikia hadhira
 
Umekaa unakuna kende nyumbani kwenu halafu unaanza kumpangia mtu aanzie wapi kusimulia....

Useless sperm...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…