SEHEMU YA KUMI NA NANE
Ilipoishia,,,,,,,,,,
Kumbe bana mule ndani si wote wanafurahia wakiona mambo yako yakiwa yanaenda fresh, kumbe si huku mtaani tu hadi jela watu wenye roho za husda wapo,
Endelea,,,,,,,,,,,,,
Siku moja ndo tumerudi kutoka kiwandani, tumeingia ili tupige msosi, Mara afande mmoja akaniita, akaniambia twende unapolala, tukaenda,mi sina hili wala lile, akaniambia nyanyua godoro, nikanyanyua, heeh mara naona kifurushi cha bangi na ugoro, basi akanipiga buti hilo, akaniambia kumbe ndo tabia yako, sisi tunapambana kuzuia hivi vitu alafu we ndo unaleta humu ndani, basi nikala mabuti ya kutosha, namwambia afande mi sijui hivi vitu lakini hanielewi, mzee baba nilikula kisago cha maana,
Basi nikapelekwa kwa mkuu wa gereza, Nikaambiwa niseme natoa wapi hivyo vitu, mi nikasema hata sielewi,mi pia nashangaa, wakawa hawanielewi, Nikaamriwa nipewe adhabu kali na nipigwe kitambaa chekundu mgongoni, sema yule afande wa kiwandani aliyekuwa ananikubali akanitetea pale kuwa mi sina hizo tabia, basi ndo ikawa ponea yangu,
Kule jela kuna vitambaa vya rangi mbalimbali na maana zake, ukiona mfungwa ana kitambaa cha njano kwenye kola basi huyo ni wa kifungo cha maisha, kitambaa cha rangi ya ugoro mgongoni ni mfungwa mwenye nidhamu, kitambaa chekundu ni mfungwa hatari, anatakiwa uangalizi maalum na kazi zake ni ngumu sana, mfungwa mwenye ufito wa kamba huyo anaitwa mchungi, mchungi ni mfungwa aliyetumikia kifungo chake sasa kabakiza kidogo sana amalize, hawa huwa wanaachwa tu huko nje, wanafanya kazi huko nje hata kulala wanaweza kulala hukohuko nje,
Basi nikasamehewa pale baada ya kuombewa msamaha, ila nikatolewa kiwandani kazi zangu zitakuwa kulima,
Basi nikarudi ndani nikamwelezea yule jamaangu, akaniambia huo mchezo upo sana huku ndani, yaani mtu akishakuwa na kinyongo na wewe basi anakuwekea bangi au mirungi ili ionekane wewe ndo unaviingiza humo ndani alafu anaenda kukuchongea kwa afande, Sa nikamuuliza kwani mi nna bifu na nani, akasema si lazima uwe na bifu na mtu, anaweza tokea tu mtu hakupendi basi akakufanyia hivyo ili kukuharibia, Daah hatari sana,
Basi nikawa napiga kazi za nje tu sasa, ni ngumu sana, kazi za kuzibua chemba za vyoo kwenye nyumba za maaskari ni za kawaida kabisa, Nilipiga kazi mpaka nikawa nawaza kitoroka nisije kufia huku,
Mungu saidia siku zikakata, ikafika siku kesho ndo namaliza kifungo natoka jela, Daah siku hiyo usiku tulipiga stori sana na yule jamaangu, akaniambia we nenda bana sisi bado tupo sana huku, ila fanya ufanyavyo usije ukarudi tena huku, we mwenyewe si umeona haya maisha, si poa kabisa, Nikamwambia ni kweli,pia nikamshukuru sana kwani kwa kipindi chote amekuwa saport kubwa sana kwangu, Tuliongea sana siku ile,
Kesho yake kweli nikaitwa,nikaambiwa kifungo chako kimeisha upo huru, ila usije ukatenda kosa tena ukarudishwa huku, basi nikapewa nguo za kiraia nikavaa,
Nikatoka gerezani, sasa naenda wapi, Nikawaza ningekuwa na nauli ningerudi zangu Dar, huko ningewakuta Sity na Da J, Au hata ningeenda zangu kwetu kijijini maana ni kitambo sana tangu nitoke huko, ningemkuta happy na mtoto, baba na mama, nimewamis sana,
Nikawa natembea na barabara tu huku nawaza, nikatembea paka nikajikuta nimetokea moshi stand, nikapita natembea tuu tena mikono nyuma maana naogopa nisije nikarusha mikono nikamgonga mtu akasema nimempiga nikarudi jela, Maana hawa watu nimesha waogopa sasa!
Nikatembea nikafika stesheni ya treni nikavuka zile reli nashuka tu huko chini sijui hata naenda wapi, nilitembea sana, paka nikafika sehemu nikakuta msitu, mwanzo nilijua ni pori tu kumbe ni msitu mkubwa, Na jioni ilikuwa imeshafika, nikasema kuliko usiku unikute mtaani ni bora unikute msituni, maana mtaani hawachelewi kuniita mwizi, yani kwa yaliyonipata watu nikawa nawaogopa sana, nibora nikutane na wanyama wakali lakini si watu,
Basi nikazama msituni, natembea tu huko, giza likaingia nikawa sioni tena mbele, nikasema nipande juu ya mti nilale ila nikaogopa nikipitiwa na usingiza nikaanguka itakuwaje, Basi nikaingia kwenye kichaka nikatandika majani nikalala,
Ajabu nikawa hata siogopi, yaani nikaona kawaida sana utadhani nipo nyumbani,
Kweli bana kuka pambazuka, nikatoka kichakani nikaendelea kutembea, nikatembea sana huko msituni, nikisika sauti za watu naingia kichakani nanyuti, wanapita unakuta ni watu wamebeba kuni, basi natoka naendelea kutembea,
Sasa njaa ikaanza kuuma, nikawa natafuta angalau matunda pori nile, kweli nikakuta sehemu vimti flani hivi kinakuwa na vitunda vidogodogo kama vigololi,vikiiva vinakuwa vyeusi, vitamu ukila, basi nikakinga shati kwa mbele nikaanza kuvichuma, nikavichuma vingi tu nikaanza kula huku natembea, kufika mbele nikakuta mto umepita mule msituni, nikashuka mtoni nikanywa maji yakitosha tu, ni machafu lakini sikujali,
Nikakaa pembeni ya mto pale nikamalizia vitunda vyangu, nikanywa maji tena nikajiskia fresh sasa, nikavuka ule mto nikaendelea na safari yangu, nikatembea mpaka msitu ukaisha nikatokea kijijini,
Itaendelea