Usilogwe ukaondoka nyumbani na kwenda usipopajua kwa kigezo cha kutafuta maisha

Well summarized
 
Reactions: Auz
Ila nilikuwa na wazo. Mkuu Akili sina anaonaje akamkumbuka na Jane pia wa Buguruni. Jane alimpa huba kijana wa UD pale alipoachia Happy
 
Dah aisee a very ending story. Mkuu umetisha saaana.
Nilichofurahi ni kuwa ulipokelea simu ukiwa mafinga my hometown hapa nilipo sasa.
Mkuu alikisina nakupongeza kwa kutokumuacha Happy aisee.
Homeboy mafinga kitaa ipi Apo, Mimi napatikana maeneo ya kitaa Cha kikuni kilabu Cha ddc Apo sema nipo kwenye miji ya watu uku napambana
 
Nmewah kuptia magum lkn sio kwa level iz aiseeee [emoji6][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Hili chaka lilikuwa tamu balaa, likipatikana lingine linaloeleweka tujulishane wakuu, ila siyo la Mpwayungu
 
Maisha yako hivi, vile unavyopambana kupata ridhiki na Mungu anakupa mlango wa kutokea. Kama mwanaume uliyekamilika lazima ukatafute maisha popote pale haijalishi una ndugu au hauna.
Unafikiri ungebaki Dar na Sity ungekuwa hapo ulipo? Kote huko ulipopita ulikuwa unatafuta mlango wa kutokea ndipo ukakutana na Kisoda.
Mimi ni mfano hai tosha, nilienda Dar kuna rafiki yangu, maisha yakanishinda nikarudi home, nikaenda Shinyanga nikalala msibani, sina ndugu wala rafiki. Nikapata kazi ya ulinzi, nako nikaishia kudhulumiwa, nikarudi nyumbani. Ukumbuke hapo nimemaliza chuo 2015, nina degree ya ualimu kutoka UDOM. Ajira alifuta marehemu Magufuli.
Nikaunga Singida, hapo sina ndugu wala rafiki. Nikalala Guest, nililipa 5,000 nikala msosi, jioni hiyo hiyo nikaanza kutafuta chumba. Nikapata kwa 15,000 nikalipa miezi mitatu, nikabakiwa na 2,000 na hapo ni mji wa watu. Nalala kwenye box najifunika shati mbili na nishalala na njaa mpaka siku 2, unaweza ukafikiri natania ila ndiyo ukweli wenyewe huo.
Huu ni mwaka wa tatu, namshukuru Mungu, nimepanga na maisha yanaenda fresh tu na nimeoa
Muhimu
Nawashauri vijana wenzangu wanaotafuta maisha, nenda sehemu yoyote ukatafute maisha haijalishi una ndugu au hauna maana mafanikio ni mchakato. Usiogope shida, sijui hauna sehemu ya kulala wala hela. Ukiwa na afya njema unatoboa
 
Bonge moja la story
 
Taarifa ya kifo cha Sity imenisikitisha sana, kuna watu huwa tunakutana nao mara moja lakini kwa matendo yao wanaishi mioyoni mwetu milele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…