Usilogwe ukaondoka nyumbani na kwenda usipopajua kwa kigezo cha kutafuta maisha

SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI

Ilipoishia,,,,,,,,,,,,,

Tukarudi kwenye magari tukaanza kupiga stori, kumbe wale jamaa wameenda kujikusanya limekuwa kundi kubwa wamekuja pale yard wanataka wafunguliwe waingie lasivyo wanavunja geti, wapo na mawe, mapanga, mafimbo, basi ikawa fujo pale, kesi ikawa kwamba Wakongo wameshirikiana na Watanzania kuwapiga wazambia, fujo zilipozidi wale walinzi ikabidi wapige simu polisi, Polisi wakaja pale wakapewa maelezo na wananchi na wale walinzi, wakaja kwenye magari wakatuchukua,

Endelea,,,,,,,,,,,,,,

Tukapelekwa Kituo cha polisi Nchelenge, Tukatoa maelezo pale, kweli ikaonekana tumewashambulia wazambia, halafu sisi ni wageni, polisi wakatutisha pale kuwa hii kesi ni kubwa na kama itaenda mahakamani lazima tufungwe, kwaiyo tuangalie mifuko yetu hii mambo iishie pale,

Wao wakawa wanataka kila mtu atoe kwacha elf moja sawa laki moja ya kibongo, Kisoda akasema hiyo hela sisi hatuna, sisi tutatoa kwacha hamsini hamsini kama haifai bora twende huko mahakamani,

Wakajitafakari pale ,wakasema leteni hiyo hela, kweli Kisoda na Anko wakatoa hiyo hela , Wale polisi wakatupa escort mpaka kwenye magari yetu tukarudi tukalala,

Kesho yake jumapili tukafua fua pale, na mimi nikafua maana nguo zangu ni zile alizonipa Kisoda na zile nlizokuwa nimevaa mwanzo,

Jumatatu asubuhi tukaenda kwenye zile ofisi za migration na ZRA, tukafanya process pale tukamaliza, tukarudi kwenye magari, wenyeji wa pale wakatuambia kutoka pale mpaka ufike Pweto boda ni kama km 100 hivi ila barabara ni mbovu kichizi, yaan ukitoka hapo asubuhi unafika boda jioni,kwaiyo tukaona kwa huo muda tutachelewa bora tulale tuanze safari asubuhi, Siku hiyo tukalala,

Asubuhi tukaamka tukajaza maji kwenye madumu maana huko tuliambiwa maji ni shida, kumbe yale mafuta yanaenda mgodini huko kongo kijiji kimoja kinaitwa kapulo, Tukalipia parking pale tukaondoka, tukafika sehemu lami ikaisha ikaanza barabara ya vumbi, yaani huko magari kupita ni nadra sana, hadi watu wanashangaa magari yakipita, barabara yenyewe kama za mtaani jinsi ilivyo mbovu, basi ikawa ni mdogo mdogo, gari unaibembeleza kuingia kwenye korongo usije ukapasua busta,

Tukawa tunaambaa ambaa na mwambao wa lile ziwa, tukafika sehemu mvua acha ianze kupiga, ikapiga mvua balaa, barabara haipitiki, tukatafuta sehemu tupaki magari mpaka mvua ikate, kabla hatujapata gari ya anko ikateleza ikaingia mtaroni, piga resi pale kuitoa haitoki, hiki kisanga kingine tena, mvua ndo imechanganya kichizi, tukasimama tukazima gari katikati ya barabara maana tungesema tupaki pembeni na sisi tungeingia mtaroni, tukatulia kwenye gari mpaka mvua ikate, ikanyesha wee mpaka ikaamua kukata, sasa mtihani ni kuitoa ile gari ya Anko, hatuna rope wire hatuna nini!,

Tukenda kwa wanakijiji kuazima jembe na beleshi tukaja kuchimba, jaribu kuitoa lakini wapi, zama huko chini chimba weee, tukajaza majani lakini ngoma haitoki,hapo tumechafuka matope balaa, tukapambana pale mpaka jioni ilkaingia lakini wapi, ajabu ile njia magari hamna kabisa, yaani tumepaki katikati ya barabara lakini hakuna hata gari moja iliyofika pale,

Basi tukawa hatuna jinsi, ni kulala tu mpaka kesho , tukaomba kuni kavu pale kijijini tukawasha moto tukatafuta vijana wawili wa pale kijijini tukasaidiana kulinda magari,

Tukakaa pale mpaka kukakucha, tukaendelea na mchakato wa kutoa gari, uzuri kulikuwa kumenyauka kwaiyo tukachukua belt, tukaikunja, kisoda akarudisha gari yake nyuma, tukaifunga ile gari ikavutwa ikatoka, ikabidi twende ziwani kuoga maana tulikuwa tumechafuka sana, tuliporudi safari ikaendelea,

Tulifanikiwa kufika pale boda ya Pweto kwenye saa nne hivi, tukapeleka documents pale tukaruhisiwa kuvuka, tukatembea kama kilomita mbili hivi tukakuta migration ya upande wa kongo, kuna kulipia pale na process nyingine, nao wakaturuhusu kuendelea na safari,

Barabara ya huku kidogo ilikuwa na afadhali maana ilikuwa na moramu, ngoma zikatembea, kuonesha kule ni nadra magari kupita basi watoto wanatoka kwenye vinyumba vyao wanakuja kushangaa magari yakipita,

Hatimae tukafika pale kapulo kwenye ule mgodi, tukaingia huko ndani tukaoneshwa sehemu ya kuegesha magari, tukapaki, kwa vile ilikuwa jioni tayari ikabidi tufanye mpango wa msosi pale, tukala tukaoga usiku ukaingia tukalala,

Kesho yake tukashusha mafuta, tukapewa documents safari ya kurudi ikaanza, Kweli tulirudi salama mpaka dar hakukuwa na shida yoyote,

Chuma ikaenda service, mi nikatumia muda huo kwenda msewe kwa Da J ila sikufanikiwa kumkuta, nilikuta milango imefungwa nyumba nzima haina mtu,

Basi safari nyingine tukaenda tena kongo lakini sasa hivi tukaenda Lubumbashi, tulipitia mpika, serenje, kapiri, ndola, tukaingia kasumbalesa, tukaingia 114( kasumbalesa upande wa zambia), siku hiyo hiyo tukafanikiwa kuingia 200( kasumbalesa upande wa kongo) tukalala pale,

Kesho yake tukatimba mpaka lubumbashi kampuni moja inaitwa Kongo petrol ndo tukaenda kushusha mafuta hapo, Basi wakati wa kurudi upande wa zambia magari ni machache hivyo kisoda akawa ananifundisha kugonga gear, yale madude ni matamu asikwambie mtu,

Basi tukaenda safari kadhaa, Lusaka, ndola, lubumbashi ndo zilikuwa safari ndefu, Nilipata hela nikanunua smart phone kongo maana ni bei poa sana, Niliingia facebook nikamtafuta Sity, nikamtumia messej lakini hakunijibu,

Basi nikaingia kwenye email yangu, kwenye zile post za kazi nilikuwa natumaga, nikadownload vyeti vyangu, nika apdate cv yangu, nikaanza kutuma maombi ya kazi mitandaoni,

Nikawa nikipata nafasi naenda kwa Da J ila nakuta hayupo, nilipoulizia pale nikaambiwa alishahama, nikasema poa,

Siku moja tumetoka kongo, nipo geto ( maana ilibidi nikae geto kwa kisoda), mara simu ikaita namba ngeni, kupokea akaongea sauti serious kidogo, " Naongea na Akili sina", nikajibu ndio, " Ulituma maombi kampuni deshi deshi nafasi ya desh desh Manager ? " nikajibu ndio, " Jumatatu unahitajika kwenye interview kwenye ofisi zetu zilizopo posta",

Mzee simu ilipokata sikuamini eti, nikajiuliza naota nini!!, Kisoda akaja nikamsimulia, akaniambia sasa hayo mambo utayaweza kweli mambo ya kisomi hayo!, Nikamwambia mi sindo mambo yangu haya nimesomea, akaniuliza umesomea wapi, kumbe nilikuwa nimeshasahau kuwa nilimdanganya kwamba sikuendelea na chuo bali nianza biashara ndogo ndogo, basi pale ikabidi nimchane live, nikamwambia nilijiskia aibu tu kukwambia kuwa nilisoma chuo kwa ile hali niliyokuwa nayo,

Basi Kisoda akanisaport pale, nikaenda kutafuta nguo za interview na viatu, maana nguo zangu nyingi yalikuwa majinsi, Nikawa najiuliza sijawahi kufanya interview toka nimezaliwa, hii itakuwaje? Nikawa naingia google nacheki maswali yanayoendana na ile position na majibu yake,

Kweli siku yae siku nikatimba kwenye interview, nilijua nitakuwa peke yangu ila nikakuta tupo kama saba hivi, tukaanza kuitwa mmoja mmoja, ilipofika zamu yangu nikazama, nikakuta panel ina watu watano, wabongo watatu wazungu wawili,

Wakajitambulisha pale, wakaanza maswali yao, mwanzoni niliingiwa upepo ila kadiri muda ulivyozidi kwenda nikazoea yale mazingira, wakaniuliza maswali mengi sana ila nikayajibu yote, wakataka waone vyeti vyangu orijino, hapo ndo ikawa kimbembe, ikabidi nidanganye kuwa viliungulia ndani ila kwa sasa nipo kwenye process ya kupata vingine,

Interview ikaisha, nasubiri majibu sasa, lakini kila nikipima sioni nafasi yangu kuchaguliwa, maana nilikuta wana pale wamekuja na magari, mtu kapiga suti yupo smart sembuse mimi hata vyeti sina,

Siku zikaenda tukaendelea na mishe zetu, siku tupo njiani tunaenda zetu ndola, tukiwa mafinga pale tunapiga msosi mara simu ikaita, nikapokea , nikasikia " Ndugu akili sina" nikajibu naam, " Unaongea na flani flani kutoka kampuni flani flani, napenda kukupongeza kwa kupita kwenye interview , nikutaarifu kuwa kesho saa mbili asubuhi unatakiwa uwepo hapa kwa ajili ya mambo mengine" simu ilipokata nikajisachi kwanza, hivi ni kweli au naota,

Kisoda akauliza ni nini nikamwelezea pale, Akaniambia ndo ushakula shavu ivyoo mzee, nikawa siamini, sasa itabidi mi safari yangu iishie pale, ikabidi tufanye mchakato wa usafiri muda uleule nigeuze dar, kweli nikapata, kisoda akanipa kama elf 70 hivi akasema hizi zitakusukuma, nikachukua na ufunguo wa geto nikawaaga pale nikadandia gari kurudi dar, kwenye saa tano hivi usiku nipo dar tayari, nikafika geto nikaoga nikalala,

Kesho asubuhi nikatimba pale kampuni, nikapokelewa, nikapelekwa kwa director, nikakuta ndo yule mzungu, tukaongea pale, nikapewa mkataba niusome, ila wakasema huu mkataba hutasaini kwa sasa, kwa sasa utafanya kama intern kwanza kwa miez sita, wakiridhika na performance ndo nitasaini mkataba wa kudumu, na kipindi cha intern ntalipwa mshahara nusu, akaniuliza kama nipo tayari , nikamwambia yes sir!!

Basi nikapelekwa kwa hr ni mmoja kati ya wale wabongo wa siku ya interview, kuna documents za kujaza jaza na nyingine natakiwa kuleta,

Kazi ikaanza hvyo, nikapewa ofisi yangu pale iko poa, nikaambiwa nitafute leseni kuna gari la kampuni nitapewa, basi mambo yakawa byee,

Mwisho wa mwezi zikaingia M kadhaa kwenye account, nikasema huu ndo nusu mshahara au wamekosea?

Basi ikabidi niame pale kwa Kisoda nikatafuta nyumba kubwa inayoendana na meneja,

Nikaanza kumtafuta Sity, nikaenda kwa Ant yake mmoja madale alinipelekaga Sity, nikafika Anti akanipokea fresh, ila alichoniambia kilifanya nilie kama mtoto,

Akaniambia Sity alifariki, alipata ajali morogoro wakati anaenda kwao bunda, nililia sana, nikamwomba shangazi siku moja anipeleke huko bunda nikalione tu kaburi la Sity,

Siku kweli tukapanga tukaenda, tukafika mpaka kwao, tukamkuta mama yake Sity, ajabu akawa kama ananifahamu vile, aliponiona akaanza kulia, tukajikuta wote tunalia sasa, kumbe kwenye album ya picha za sity kuna picha tulipiga nae zipo kule ndo maana yule mama akawa ananijua,

Tukaenda kwenye kaburi la Sity ,nililia sana pale juu ya kaburi, nililia paka makamasi yakanitoka, nikawa kama nimefufua msiba upya, wote wanalia,

Tukatoka pale, tukaenda ndani, nikawapa pole sana, nikawasimulia jinsi Sity alivyokuwa msaada kwangu, nikamkuta mdogo wake pale wa kiume, ndo kamaliza four ila kafeli yupo nyumbani, Nikamwahidi mama nitamsomesha yule dogo mpaka chuo kikuu, pia nikamwambia nitamjengea nyumba pale pembeni yote ni kujaribu kulipa kwa sehemu tu fadhila zote alizonifanyia Sity, nikaondoka nikarud zangu town,

Kule kijijini kwetu nilitimba siku moja, hawakuamini, wakashangaa sana, wakasema walijua nimeshakufa zamani, mzee na mama walifurahi sana, nikakuta dogo ana watoto watatu sasa,

Nikakutana na Hapy, hakuamini kuniona, kwanza akajua nimeshaoa na sina hata time nae, nikamwambia nitamwoa nani na wewe ndo mke wangu umesahau nilikwambia,

hakuamini eti, nikakuta joyce kawa mkubwa nae shule ameshaanza , nikamwambia happy ajiandae nimekuja kumchukua, hakuamini mzee, pale home walifanya sherehe siku ile, nikalala siku moja, kesho yake nikawaaga maana mjini nipo kwenye kazi za watu,

Kesho yake nikamchukua Happy na Joyce tukaja zetu Dar kuanza maisha mapya,
Da J nilimtafuta mpaka leo sijamuona,

Mdogo wake Sity akarudi shule namsomesha na anaendelea vizuri, pia nyumba nimeshaanza kuijenga saiv ndo ipo kwenye lenta,

Na pale kwetu pia nimeshaanza msingi nataka niangushe mjengo pale,

Mshikaji wangu kisoda sijamuacha, mara nyingi naenda pale na nna mpa saport na yeye maana ana nyumba yake kigamboni anajenga kwaiyo nampa saport mara kwa mara,

Saiv nipo na happy mke wangu na tuna mtoto mwingine Anaitwa Angel maisha ni mazuri asee nakula hela ndefu kiasi, nna usafiri fresh yani,

Kwa wale tunaosota kitaa sababu ya ajira, niwatie moyo tu mlango wako upo, siku moja utafunguka, ila tu Sikushauri kujilipua na kwenda sehemu hukujui, huna ndugu, huna hela eti unaenda kutafuta maisha, siku shauri,

MWISHO

Na mimi Akili Sina nichukue nafasi hii kuwashukuru wote tuliokuwa pamoja kuanzia mwanzo hadi mwisho kwenye stori ya ndugu yetu huyu, Niwajuze tu huu mkasa haujanikuta mimi, nilihadithiwa tu na mtu na mimi nikaona niwasimulieni nyie, Karibuni Mbinga huku tule dagaa nyasa,

HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA, HAIRUHUSIWI KUKOPI WALA KU EDIT BILA IDHINI
Mkuu Akili Sina umetisha, story tamu sana hii. Nipo maguu hapa
 
shukrani sana mkuu kwa kumalizia historia yako ila hayo mengine tunamuachia mungu
 
Kaandika realism kabisa ya wanafunzi hasa mwaka wa kwanza....udsm nimesoma..kila angle anayoongelea naielewa....mpaka Bagamoyo nimewah sindikiza pia rafik yangu kwa mganga lkn yeye alikuwa na kesi nyingine.....pure true story....sijui sahv utakuwa na status gani kiongozi...na huogopi id yako kuwa identified maana unaweka siri zako waziwazi hivi....labda una uhakika hazita leak lkn.....japo bado story inaendelea.....hahaaaaaaa maisha....Gongolamboto Explossion tragedy....Never forgotten[emoji28], enzi hizo nilikuwa Nachingwe Lindi.
 
Daah..leo ndio nmeimaliza..kongole kwako mwandishi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Jamaa una akili nyingi, lkn changamoto hazituishi na zipo kwa ajili yetu, maliza yako umetupiga na deception moja kali kabisa.

Lkn tumekuelewa, hii story hujahadithiwa wala nini ni purely yakwako, ila kwa sababu za privacy umeamua kwenda nasi kwa namna hii.

Kama ni chumvi, umeweka kidogo sana kukoleza story, lkn kwa mtoto wa kijijini kama mm na nimekuja soma udsm pia, nimekuelewa.

Endelea na maisha na ishi maisha yako...ila Mungu yupo, jikabidhi kwake maana majsha flani huwa yanarudi ghafla ukaja leta story tena.....
 
Script ilivo ilikua lazima Sity atoweke kwenye maisha ya jamaa kwa namna moja au nyingine. what if Sity angekua hai. Happy ingekuwaje na tayari alikua kesha muahidi kumuoa na pia alishamzalia.
Kwahiyo unataka kusema ahadi yake kwa Happy ndio sababu ya kifo cha Sity ?
 
Kwa hivyo mkuu unataka kusema jamaa amempoteza sity kwa kusema amekufa ili story yake ikae usawa na asipokee lawama hapa jukwaani?
Is that make sense kwanini asiseme alikuta kaolewa?..
Nadhan amemaanisha kuwa ahadi aliyoitoa kwa mpnz wake Happy ndio sababu ya kifo cha Sity,imagine Sity angekuwepo Happy asingeolewa
 
Duuuuuuhh umenikumbusha Kijiji Cha Chabutwa niliwahi pita mwaka 2014 namkumbuka Mzee Kapongwa mwalim Mstaafu.
 
Nilizaliwa mwishoni mwa miaka ya themanini katika kijiji cha chabutwa wilaya ya Sikonge mkoa wa Tabora, nilifanikiwa kupata elimu yangu ya msingi hapo kijijini, shuleni nilikuwa vizuri sana, si walimu tu bali hata wanafunzi walinipenda. Familia yetu ilikuwa ya maisha ya kawaida sana kwani baba na mama wote ni wakulima wadogo wadogo tu, kwetu tulizaliwa wawili tu mimi na mdogo wangu wa kiume.

Basi baada ya kumaliza shule ya msingi nilichaguliwa kujiunga na shule ya skondari Chabutwa iliyopo pale katani. Kwa vile nilikuwa John kisomo basi maisha ya shule hayakuwa mabaya ki ufaulu, Paka namaliza form four nilikuwa naongoza pale shuleni, Baba yangu alipenda kunihusia kuwa nisipende kujionesha kwa watu kuwa nina akili maana si wote wanapenda kuona watoto wao hawafanyi vizuri alafu watoto wa wengine wanafanya vizuri

Basi nilijitahidi sana kufata ushauri wa mzee ingawa kama unavyojua haya mambo hayafichiki, Kata nzima ilikuwa inanifahamu, kwenye vikao vya shule ndo usiseme maana niligeuzwa sample space (Sehemu ya wengine kujifunzia).

Basi nikamaliza four pale na Mungu si Athumani nikafaulu vizuri na kuchaguliwa kujiunga na shule ya Pugu Secondary kwa ajili ya five na six. Mzee wangu alifurahi sana si kwa sababu ya kufaulu tu bali nilichaguliwa shule ya mbali na pale nyumbani maana mzee alikuwa hana amani kabisa na majirani wa pale katani

Basi bana, siku ya siku nikatimba shule ya baba wa taifa, Askwambie mtu nilikutana na life la kibabe sjawahi kuona
Picha linaanza shule haina maji, Maji utajua pa kuyapata, kama utaenda mtaani kununua utajua mwenyewe, Ukitaka uzame pondi ( Huko bondeni kuna visima wanatumia wanakijiji ila maji yake yana magadi na fangasi wa kutosha)

Kufupisha story sitaelezea sana life la Pugu, ila kiukweli lilikuwa la kiume, Miongoni mwa vitu sitavisahau ni bweni letu la Mapinduzi 3 ambalo ndo lilikuwa linaaminika bweni la watu wakorofi shule nzima, pia nikiwa bado mgeni nilikaribishwa kwa kupigwa nguo zangu zote nikabaki na nliizokuwa nimevaa tu, yaani siku hiyo nimetoka pondi nimefua nguo zangu nikaanika kwenye ukoka, nikaondoka kwenda kutembea majohe, kurudi jioni nakuta ukoka unanikodolea tu hakuna nguo yaani Hadi boxer walichukua wahuni wale.

Kingine sitasahau ni tukiwa karibu kumaliza six, tumebakiza paper ya practical ya chemistry, siku hiyo ilikuwa jioni ki giza ndo kinaingia, nimetoka kupiga zangu nguna maharage, najisogeza taratibu naelekea kwenye kipindi cha dini, Mara ghafla naona watu wanakuja wengi wanakimbilia eneo la shule, Wa baba, wa mama wengine wana watoto, nikajiuliza kimoyomoyo haya maandamano ya nini tena, nikiwa bado nashangaa ghafla nikaona kitu hicho ndo kilifanya nione hii issue ni serious, nikamwona teacher wetu wa darasa nae anakuja mbio, tena mbaya zaidi ana kitambi sasa akikimbia balaa, na alikuwa na spidi maana ilikuwa kawaida yake kila asubuhi anatukimbiza ambao hatuendi assemble.

Duuh, nlipoona hivyo na mimi nikaliunga tukaanza kukimbia, kuna sehemu wanafunzi wanapenda kuangalia tv nikakuta nao wamesepa wameacha tv pale, Daaah sasa wote tunakimbia halafu hatujui tunakimbia nini, Sasa wakati naendelea kukimbia nikakutana na mlemavu mmoja yupo kwenye kiti chake cha matairi (Maana ile shule ina wanafunzi walemavu pia),. Sasa hana mtu wa kumsukuma na kile kiti chake, kila mtu anaokoa nafsi yake, basi huruma ikaniiingia nikaanza kunsukuma huku tunakimbia, ebwanaeeh tumekimbia mwisho nikaona hapa nafeli, maana watu wanazidi kukimbia kuelekea bondeni huko alafu kelele zimekuwa nyingi, nikaona usintanie nikamwacha yule mlemavu nikaanza kukimbia mwenyewe.

Nikakimbia hatimae nikafika pondi, pale kidogo nikakuta watu wamerundikana kidogo,wanaulizana ni nini ila hakuna anaejua, ila juu angani anga limegeuka rangi, limekuwa jekunduuu kama vile jua lataka kushuka, alafu kelele kama vile watu wanapiga mabati huko angani au kama vile msitu unaungua sasa zile kelele za miti, daah hapo nikajua ndo mwisho wa dunia huu, wakati nageuka huku na kule mara namwona yule mlemavu ila saivi hayupo kwenye kiti bali anatambaa chini, nikajiuliza huyu kakimbia au kabebwa? Nikabaki nimestaajabu ila nikajichanganya asije kuniona akasema huyu broo ana roho mbaya, maana jinsi anga lilivyo jekundu yaani Hadi watu mna onana kabisa

Basi bana kelele zikazidi, watu woga ukaongezeka basi mbio zikaanza , tukapanda juu tukatokea Barbara kubwa ya pugu kajiungeni, Barabara imejaa watu wanakimbia, magari ndo usiseme, basi tukawa tunakimbia kelele zikizidi ukitazama juu unaona kama kimondo cha moto kinakuja hivyo unalala chini, kikipita unaamka tena unaaza mbio, Basi tukafika njia panda ya kisarawe na chanika, tukala kulia kuelekea kisarawe, mbio mbio unafika mahali unakutana na mdada anakimbia kanga inaanguka anabaki na chupi lakini hana muda wa kuokota kanga,ni kukimbia tu, mi pia sikuwa hata na hamu ya kutazama hayo mambo, maana unakimbia ukilala chini unasali ili likimondo lipite, basi ni kukimbia na kusali tu

Basi mara tukafika shule ya secondary Minaki , kulikuwa na wanafunzi pale nao wakaungana na sisi kukimbia, tukakimbia mara tukatoboa kisarawe,hapo ni usiku hata siijui saa ngapi, Basi pale kisarawe tukakuta watu wengi kinyama, yaanii pale ndo ikawa kama makutanio, watu wanaulizana ni nini,lakani hakuna anaejua dhahiri ni kitu gani kimetokea, Basi wakati tunashangaa pale mara ule mwanga na yale makelele yakawa takekaribia tena, watu wakaanza kuondoka kuendelea mbele,

Daah kwa jinsi nlivyokimbia na miguu ilivyokuwa inauma nikasema mi skimbii tena, kama kufa nife tu, basi nikaona cruzer moja imejaza watu nyuma inaondoka, nikaikimbilia nikaidaka, nikadandia yenyewe ikachanganya, sasa wakati natafuta sehemu ya kuweka mguu nikakosa, mikono ikachoka kubembea nikarudisha miguu kwenye lami, acha niburuzwe, nikaskia watu wanasema umeuaaaa, gari ikasepa nikaamka kujiangalia, nilikuwa nimevaa jinsi lakini ililiwa na lami paka ikakutwa Ngozi, nilichubuka vibaya, damu zinatoka balaa vidole vinatoa damu, ndala Sina maana zulikatika toka huko nikiwa nakimbia

Basi, mara nikaona cruiser moja imechorwa msalaba mwekundu, watu wanaikimbilia, na mimi nikazama, sasa wakati nazama kuna mama mmoja alikuwa mbele yangu, nikamvuta nyuma mi nikazama ndani, kumbe ni mke wa yule dereva anae endesha lile gari

Itaendelea

SEHEMU YA PILI

SEHEMU YA TATU

SEHEMU YA NNE

SEHEMU YA TANO

SEHEMU YA SITA

SEHEMU YA SABA
Duuuuuh umenikumbushaaa mbali Kijiji Cha Chabutwa niliwahi pita huko 2014 namkumbuka Mzee Kapongwa mwalim Mstaafu sijui yupo alikuwa na uwalaza kidogo.
 
Nadhani atakwepo maana si miaka mingi sana imepita
 
😂😂 acha kupotosha maboya, hii story ni yako.

Graduates wanapitia mengi sana aisee, halafu kuna ticha yuko hapa jf anawaambia ni wazembe, hawajui kutumia fursa, inabidi wajiajiri, hawajui kuomba kazi, hawana cv nzuri, hawajui kujibu maswali ya interview.

Kuna watu wanahustle sana kitaa, ni vile tu bahati haiko upande wao.
 
[emoji23][emoji23] acha kupotosha maboya, hii story ni yako.

Ameen
 
Stori si yangu mkuu, Ngoja kuna nyingine ntaileta hapa nayo utasema tena ni yangu
 
Back
Top Bottom