Usilogwe ukaondoka nyumbani na kwenda usipopajua kwa kigezo cha kutafuta maisha

Usilogwe ukaondoka nyumbani na kwenda usipopajua kwa kigezo cha kutafuta maisha

Nauli ya tabora au Dar? Ngoma ni kama 25 hadi 35 kipindi hicho, bwana jela atoe wapi ? Tena ampe mtu asiyemjua

Labda angeweza kupewa buku, angedandia magari kibishi ya kwenda Arusha, kwenye kile kiwanda cha A to Z angeweza kupata tena kazi kisha nauli ya home ajipange upya
Huwa wanasaidiwa nauli, iwapo nauli ikiwa kubwa huwa wanaombewa msaada wa kusafirishwa kwa Polisi Trafic.

Nimewahi kuona Jinsi Trafic wanavyowaombea lift watu kwenye Mabasi ya mikoani, wanasema huyu ni Askari mwenzetu, kama hakuna siti anaombewa akae pale mbele karibu na Dereva. Huwa Madereva Hawakatai ombi likitoka kwa Polisi.

Mimi mwenyewe kuna ndugu yangu ni Trafik ameshawahi kunisafirisha kwa staili hii bila kulipa nauli.
 
Hii story unatakiwa uchangiwe bundle wenzako wana make pesa sana. Kwa kuwa yule jamaa wa Whatsapp yeye anaitoa bure wewe anzisha group wenzako huwa wanapata pesa. Na si lazima useme yalikutokea hapo lazima watu watakushtukia unajua wadada wengi wanapenda stories. Kuna jamaa naye anakuja ana copy kwako anaenda irusha instagram anapata pesa yake vizuri kujiunga tsh 3000 na watu wanalipa.

Wewe unatoa whatsapp unaleta JF. Yeye anatoa JF anapeleka insta sema tu yeye ana akili anawatoza watu pesa na anapata. Ndo mjini palivyo.
Acha shobo. Tuliza kalio.
 
He is so negative minded! Kila Binadamu Ana mapito yake na Mitihani yake kwenye hii Dunia. Hata hao Mitume wa Mungu walipitia Mitihani mizito.
That mindset discussed in details in Bible katika kitabu Cha Ayubu, hakutenda kosa lakini mabalaa yakamukuta. Rafiki zake walikuwa wanamwambia atafakari alichimukisea Mungu, maana waliamini hayawezi mkuta bila dhambi. But haikuwa hivyo. Na hakuwa na dhambi Wal kosa lolote
 
He is so negative minded! Kila Binadamu Ana mapito yake na Mitihani yake kwenye hii Dunia. Hata hao Mitume wa Mungu walipitia Mitihani mizito.
Wamekariri na ndio Hawa wanaibiwa na waganga ama wachungaji kuwa njoo uombewe ama usafishwe nyota ili Mambo yako yanyooke. Ivi wee una akili mtu yakinyooka hakuna magari ,simu, nyumba nzuri Mana shida ndizo zinazofanya mtu anakasirika anawaza kutafuta njia ya kutatua ishu fulani.kila mtu awe na ndege kweli. Yaani haufanyi kazi hujawahi uza hata nyanya halafu unataka uende Japan ukajaze meli magari yako ulete utuuzie eti miujiza. Uliona wapi
 
Huwa wanasaidiwa nauli, iwapo nauli ikiwa kubwa huwa wanaombewa msaada wa kusafirishwa kwa Polisi Trafic.

Nimewahi kuona Jinsi Trafic wanavyowaombea lift watu kwenye Mabasi ya mikoani, wanasema huyu ni Askari mwenzetu, kama hakuna siti anaombewa akae pale mbele karibu na Dereva. Huwa Madereva Hawakatai ombi likitoka kwa Polisi.

Mimi mwenyewe kuna ndugu yangu ni Trafik ameshawahi kunisafirisha kwa staili hii bila kulipa nauli.
Sasa huyo ni ndugu yako ambaye ni trafiki.
Askari kukupa hela ambayo haipo kwenye bajeti ni ngumu mno, kwanza yeye anakuwinda na kukubambikza kesi ili akukamue hela
 
That mindset discussed in details in Bible katika kitabu Cha Ayubu, hakutenda kosa lakini mabalaa yakamukuta. Rafiki zake walikuwa wanamwambia atafakari alichimukisea Mungu, maana waliamini hayawezi mkuta bila dhambi. But haikuwa hivyo. Na hakuwa na dhambi Wal kosa lolote
Tena ndio wanaopewaga mateso ili watoke huko waje kwa shetani. Man ahadi ya Mungu ni uzima wa milele na peponi Bata batani
 
SEHEMU YA KUMI NA TISA

Ilipoishia,,,,,,,,,,,,,

Nikakaa pembeni ya mto pale nikamalizia vitunda vyangu, nikanywa maji tena nikajiskia fresh sasa, nikavuka ule mto nikaendelea na safari yangu, nikatembea mpaka msitu ukaisha nikatokea kijijini,

Endelea,,,,,,,,,,,,,,,,

Nikatembea mpaka nikafika kwenye nyumba moja hivi ya udongo, nje kuna watu watu pale wanapiga ulabu, wakawa kama wananishangaa ila mi sikujali, nikanyoosha mpaka kwa mzee mmoja ambaye nilimwona ndo anahudumia pale, nikamsalimia, nikamwambia mzee samahani naomba nisaidie maji ya kunywa, basi mzee akazama ndani akatoka na jagi la maji na kikombe kikubwa, akataka kunimiminia nikamwambia usijali,nikachukua lile jagi na kile kikombe nikaenda kukaa kwenye jiwe pale pembeni nikapiga vikombe vyangu viwili nikatulia,

Basi nikakaa pale nafikiria maana ingawa nilikunywa maji ila kiukweli nna njaa, basi kumbe wale watu bado wananicheki tu, yule mzee akaja akaniuliza vipi we ni mgeni eneo hili, nikamjibu ndio, akauliza umetokea wapi, nikaogopa kumwambia nimetoka jela, nikamwambia nimetoka tabora nimekuja kutafuta kazi, mzee akacheka sana, akasema sasa huku yenyewe vijana hawana kazi na wewe tena unakuja kutafuta kazi, nikamwambia kila mtu na bahati yake, akasema kwaiyo saivi unaelekea wapi, nikamwambia sina mwelekeo wowote,

Basi tukapiga stori na mzee pale nikamweleza jinsi maisha yalivyo magumu kijijini kwetu mpaka nikaamua kuja huku kutafuta kazi, mzee akaniambia kazi za pale kijijini nyingi ni kilimo, mzee ana roho nzuri sana , sijui alijua nna njaa, akamwagiza kijana wake aniletee ugali, kweli mzee ukaja ugali na mboga za majani pale nikapiga, nikanywa na maji nikajiskia nina nguvu sasa,

Nikamwomba mzee nikae pale kwake siku chache wakati natafuta muelekeo, mzee hakuwa na hiyana ila pa kulala ndo shida, akasema kama nitaweza kulala jikoni sawa, nikamwambia mzee haina shida mi nalala fresh tu,basi akamwita mzee mwingine pale akamwelezea, yule mzee nae akaniuliza maswali maswali nikamjibu nikaona katulia, badae nilikuja kujua kumbe yule ndo mwenyekiti wa kijiji,

Nikakaa kwa mzee pale nikawa nasaidia saidia kazi pale nikishirikiana na kijana wake,mzee hana mke, anajishughulisha na kilimo na uuzaji wa pombe za kienyeji, nikaja gundua mpaka gongo anauza ila kwa kificho sana,

Basi nilikaa kwa mzee kama wiki mbili hivi, nikiwa pale nikataka niombe simu nimpigie Sity au Da J ila namba zao kwani nazikumbuka hata!,

Basi siku moja tupo pale, watu kibao wanapiga ulabu, kelele za kutosha, mzee akatuita mi na kijana wake kwa siri, akasema pale mzigo umeisha, tuchukie baiskeli tukimbie tukalete fasta ila tuwe makini huko njiani, mi hata sijui mzigo gani, basi tukachukua baiskeli na kidumu cha lita tano kwenye kisafleti tukaondoka hata sijui tunaenda wapi,

Kijana anagonga pedeli huyo!, Mara tukazama msituni, tunapita kwenye vichochoro huko msituni, tukafika sehemu tukakuta ule mto, tukaacha baiskeli sehemu, tukatembea kidogo kuingia ndani ndani, kufika nilishangaa sana, nilikuta majamaa yametengeneza mtambo huo wa kutengeneza gongo, wale jamaa ni wanasayansi sema hawajui, ile ni simple distilation kabisa, Basi yule kijana akaenda kuongea nao pale akawapa kile kigaloni tukawa tunasubiri,

Tukiwa tumesimama pale tunasubiri hatuna lile wala hili ghafla tukaskia sauti nyuma " mpo chini ya ulinzi, mikono juu, asikimbie mtu" , kumbe ni polisi mzee!!, wale jamaa wakatoka nduki kwenye vichaka huko, tukabaki mimi na yule kijana tumeduwaa pale hatujui cha kufanya,

Tukakamatwa pale tukapigwa mitama tukakaa chini, tukafungwa mashati, wakamwaga ile pombe iliyokuwa kwenye pipa ambalo ndo wametengenezea ule mtambo, wakachukua lile pipa na vifaa vingine, kumbe walikuja na gari wamelipaki mbali kidogo, tukatembea paka kwenye gari tukatiwa ndani, wakapakia na yale mamtambo chuma ikaamsha,

Niko kwenye gari nna waza hiki ni nini tena, nikasema yaleyale yanaanza tena, huu mzimu wa mikosi utaniandama mimi mpaka lini, nikimwangalia yule dogo hana hata wasiwasi, sijui ameshazoea yale mambo!,

Basi ndinga ikatembea mpaka kituo cha polisi majengo, wakati tunashuka nawaza hivi hawa askari si watanikumbuka tena mimi, Tukaingizwa ndani tukachukuliwa maelezo, ikabidi nidanganye jina ili wasije nikumbuka, Tukasweka ndani kwenye kile kiselo, tukakuta masela wengine humo ndani,

Tulikaa mule ndani mpaka usiku ukaingia, tukalala selo, Kesho yake Asubuhi tukaitwa, kutoka tukakuta mzee kaja kaleta na chai pale tukapiga, Basi mzee akafanya mpango pale tukaachiwa, tukatoka nje,mzee anatupa pole anasema ndo maisha hayo ya kumjenga mwanaume, kimoyo nikasema lait angejua kwangu hichi ni cha mtoto, niliyopitia ni makubwa kuliko hili,

Basi tulipotoka pale nje kile kituo hakipo mbali na barabara kubwa, nikawa naona mabasi yanapita,malori yanapita nikasema ile barabara itakuwa ya kwenda dar, nikakumbuka sana dar, mzee akasema pandeni baiskeli twendeni, nikamwambia mzee mi sirudi tena kule, nataka nikatafute gari nirudi nyumbani, mzee akasema sawa hamna shida ,safari njema, basi wakagonga pedeli wakasepa,

Mi nikatembea mpaka pale barabarani nikamuuliza mtu hii barabara inaenda wapi, akasema huku inaenda moshi stand huku inaenda njia panda na dar nikasema asante, nikashika ile ya kwenda dar, nikasema leo ntaenda dar hata kwa miguu, maana huu mji umenikataa, watu wa huku makatili sana,

Nikatembea nafata barabara tu huku nawaza mambo mengi kichwani , nikafika sehemu miguu inauma sasa, nikasikia jamaa mmoja anaongea na simu anasema " ndo nipo kiboroloni hapa nataka nipande town mara moja" , basi nikajua ile sehemu panaitwa kiboroloni, mbele kidogo kulikuwa na semitrailer limepaki pembeni, nikafika pale milango ya gari imefungwa, lengo langu ni kuwa kama linaenda dar niombe lift,

Basi akili ikanituma nisubiri pale mpaka dereva aje, nilikaa pale mpaka giza likaanza kuingia, nikasema sasa hata akija akikataa itakuwaje, ni bora nitafutet sehemu kwenye hili gari nijibanze hivyohivyo, basi nikapanda pale katikati ya tela na kichwa nikakaa, mtu anaweza asinione maana ilikuwa imebeba kontena lile kubwa,

Nikakaa sana pale, nikahisi mkojo umebana, basi nikashuka chini nikazunguka nyuma ya gari nikakojoa, kumbe lile kontena lipo wazi mlango mmoja, nikapata wazo nipande niingie ndani ya lile kontena, basi nikajivuta nikapanda, nikaingia, nikacheki kama kuna mtu kaniona nikaona kimya, nikakaa mwishoni mwa ule mlango ulofungwa kwenye kona kabisa kiasi kwamba ni ngumu mtu kuniona, nikakaa mpaka usingizi ukanipitia,

Nilipo kuja kushtuka nikakuta ngoma inatembea, imechanganya kinyama, nikasema weweiyaa!!!, Shida sijui sasa inaenda wapi, potelea mbali itakavyokuwa ndo hivyo hivyo, ila nikajipa matumaini ilikuwa imepaki kuelekea dar,

Basi ngoma ina amsha , mi nalala nashtuka nalala nashtuka chuma inaambaa tu, basi nilipokuja kushtuka kumeanza kupamba zuka chuma bado inaamsha, tukafika sehemu ikapaki, ni kwenye kamji hivi kamechangamka, tukakaa pale kama masaa mawili hivi, mara chuma ikaamsha tena, tukafika sehemu ikasimama tena, nahisi pale walisimamishwa na trafiki, nikasema nichungulie nje kidogo nikaona jengo limeandikwa TRA Segera, nikajua kumbe tumefika segera,

Basi ngoma ikaamsha tena, jamaa sijui alikuwa anawahi wapi maana hapotezi muda, Huwezi amini nilikuja kushtukia mataa ya ubungo haya hapa, nikasema khaah! Sasa hapa nishuke niende zangu msewe kwa Da J,

Ila gari haisimami sasa, yaani ikisimama kidogo nafikiri nifoleni ile nasema nitoke sasa chuma inang'oa daah! , Mara Tazara hii hapa, nikajua itasimama maana najua tazara kunakuwaga na foleni lakini wapi, ngoma ikaunga kama inaenda uwanja wa ndege, nikasema hii hatari sasa, kama vipi nitulie tu mpaka itakapo simama,

Basi nafkiri ilikunja jeti pale maana badae sikuiona tena ile barabara ya nyerere, Chuma ikatembea mpaka ikafika sehemu kuna geti ikazama ndani, ikaenda ikapaki, nikachungulia huko nje naona malori mengi kama yard vile, alafu kuna geti na walinzi wa kk, ukuta wa hiyo yard ni mkubwa na kuna nyaya zile zenye umeme zimepita juu ili mtu asiruke,

Daah! sasa ntatokaje tena humu ndani, hili mbona balaa jingine tena, nikichungulia naona ma mbwa yanazunguka zunguka humo ndani, aisee hiki kimbembe tena, nikasema hapa polisi pananihusu tena, nikiulizwa nimeingiaje humu ndani nitasemaje, na nilikuwa natafuta nini,

Itaendelea
KIDAGAA akasema "Imeisha hiyoo"

🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom