Mhandisi Mzalendo
JF-Expert Member
- Aug 23, 2010
- 6,682
- 11,461
Kidagaa fala sana.....KIDAGAA akasema "Imeisha hiyoo"
🤣🤣🤣
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kidagaa fala sana.....KIDAGAA akasema "Imeisha hiyoo"
🤣🤣🤣
Acha upumbavu...potezea uziHuku mbele story inaanza kuvuja, nadhani uitimishe tu maana soon utakinga mwenyewe pale panapovuja.
Daah aisee nimepitia maisha ya kuanguka lakini yakwako ni balaa
SEHEMU YA KUMI NA TISA
Ilipoishia,,,,,,,,,,,,,
Nikakaa pembeni ya mto pale nikamalizia vitunda vyangu, nikanywa maji tena nikajiskia fresh sasa, nikavuka ule mto nikaendelea na safari yangu, nikatembea mpaka msitu ukaisha nikatokea kijijini,
Endelea,,,,,,,,,,,,,,,,
Nikatembea mpaka nikafika kwenye nyumba moja hivi ya udongo, nje kuna watu watu pale wanapiga ulabu, wakawa kama wananishangaa ila mi sikujali, nikanyoosha mpaka kwa mzee mmoja ambaye nilimwona ndo anahudumia pale, nikamsalimia, nikamwambia mzee samahani naomba nisaidie maji ya kunywa, basi mzee akazama ndani akatoka na jagi la maji na kikombe kikubwa, akataka kunimiminia nikamwambia usijali,nikachukua lile jagi na kile kikombe nikaenda kukaa kwenye jiwe pale pembeni nikapiga vikombe vyangu viwili nikatulia,
Basi nikakaa pale nafikiria maana ingawa nilikunywa maji ila kiukweli nna njaa, basi kumbe wale watu bado wananicheki tu, yule mzee akaja akaniuliza vipi we ni mgeni eneo hili, nikamjibu ndio, akauliza umetokea wapi, nikaogopa kumwambia nimetoka jela, nikamwambia nimetoka tabora nimekuja kutafuta kazi, mzee akacheka sana, akasema sasa huku yenyewe vijana hawana kazi na wewe tena unakuja kutafuta kazi, nikamwambia kila mtu na bahati yake, akasema kwaiyo saivi unaelekea wapi, nikamwambia sina mwelekeo wowote,
Basi tukapiga stori na mzee pale nikamweleza jinsi maisha yalivyo magumu kijijini kwetu mpaka nikaamua kuja huku kutafuta kazi, mzee akaniambia kazi za pale kijijini nyingi ni kilimo, mzee ana roho nzuri sana , sijui alijua nna njaa, akamwagiza kijana wake aniletee ugali, kweli mzee ukaja ugali na mboga za majani pale nikapiga, nikanywa na maji nikajiskia nina nguvu sasa,
Nikamwomba mzee nikae pale kwake siku chache wakati natafuta muelekeo, mzee hakuwa na hiyana ila pa kulala ndo shida, akasema kama nitaweza kulala jikoni sawa, nikamwambia mzee haina shida mi nalala fresh tu,basi akamwita mzee mwingine pale akamwelezea, yule mzee nae akaniuliza maswali maswali nikamjibu nikaona katulia, badae nilikuja kujua kumbe yule ndo mwenyekiti wa kijiji,
Nikakaa kwa mzee pale nikawa nasaidia saidia kazi pale nikishirikiana na kijana wake,mzee hana mke, anajishughulisha na kilimo na uuzaji wa pombe za kienyeji, nikaja gundua mpaka gongo anauza ila kwa kificho sana,
Basi nilikaa kwa mzee kama wiki mbili hivi, nikiwa pale nikataka niombe simu nimpigie Sity au Da J ila namba zao kwani nazikumbuka hata!,
Basi siku moja tupo pale, watu kibao wanapiga ulabu, kelele za kutosha, mzee akatuita mi na kijana wake kwa siri, akasema pale mzigo umeisha, tuchukie baiskeli tukimbie tukalete fasta ila tuwe makini huko njiani, mi hata sijui mzigo gani, basi tukachukua baiskeli na kidumu cha lita tano kwenye kisafleti tukaondoka hata sijui tunaenda wapi,
Kijana anagonga pedeli huyo!, Mara tukazama msituni, tunapita kwenye vichochoro huko msituni, tukafika sehemu tukakuta ule mto, tukaacha baiskeli sehemu, tukatembea kidogo kuingia ndani ndani, kufika nilishangaa sana, nilikuta majamaa yametengeneza mtambo huo wa kutengeneza gongo, wale jamaa ni wanasayansi sema hawajui, ile ni simple distilation kabisa, Basi yule kijana akaenda kuongea nao pale akawapa kile kigaloni tukawa tunasubiri,
Tukiwa tumesimama pale tunasubiri hatuna lile wala hili ghafla tukaskia sauti nyuma " mpo chini ya ulinzi, mikono juu, asikimbie mtu" , kumbe ni polisi mzee!!, wale jamaa wakatoka nduki kwenye vichaka huko, tukabaki mimi na yule kijana tumeduwaa pale hatujui cha kufanya,
Tukakamatwa pale tukapigwa mitama tukakaa chini, tukafungwa mashati, wakamwaga ile pombe iliyokuwa kwenye pipa ambalo ndo wametengenezea ule mtambo, wakachukua lile pipa na vifaa vingine, kumbe walikuja na gari wamelipaki mbali kidogo, tukatembea paka kwenye gari tukatiwa ndani, wakapakia na yale mamtambo chuma ikaamsha,
Niko kwenye gari nna waza hiki ni nini tena, nikasema yaleyale yanaanza tena, huu mzimu wa mikosi utaniandama mimi mpaka lini, nikimwangalia yule dogo hana hata wasiwasi, sijui ameshazoea yale mambo!,
Basi ndinga ikatembea mpaka kituo cha polisi majengo, wakati tunashuka nawaza hivi hawa askari si watanikumbuka tena mimi, Tukaingizwa ndani tukachukuliwa maelezo, ikabidi nidanganye jina ili wasije nikumbuka, Tukasweka ndani kwenye kile kiselo, tukakuta masela wengine humo ndani,
Tulikaa mule ndani mpaka usiku ukaingia, tukalala selo, Kesho yake Asubuhi tukaitwa, kutoka tukakuta mzee kaja kaleta na chai pale tukapiga, Basi mzee akafanya mpango pale tukaachiwa, tukatoka nje,mzee anatupa pole anasema ndo maisha hayo ya kumjenga mwanaume, kimoyo nikasema lait angejua kwangu hichi ni cha mtoto, niliyopitia ni makubwa kuliko hili,
Basi tulipotoka pale nje kile kituo hakipo mbali na barabara kubwa, nikawa naona mabasi yanapita,malori yanapita nikasema ile barabara itakuwa ya kwenda dar, nikakumbuka sana dar, mzee akasema pandeni baiskeli twendeni, nikamwambia mzee mi sirudi tena kule, nataka nikatafute gari nirudi nyumbani, mzee akasema sawa hamna shida ,safari njema, basi wakagonga pedeli wakasepa,
Mi nikatembea mpaka pale barabarani nikamuuliza mtu hii barabara inaenda wapi, akasema huku inaenda moshi stand huku inaenda njia panda na dar nikasema asante, nikashika ile ya kwenda dar, nikasema leo ntaenda dar hata kwa miguu, maana huu mji umenikataa, watu wa huku makatili sana,
Nikatembea nafata barabara tu huku nawaza mambo mengi kichwani , nikafika sehemu miguu inauma sasa, nikasikia jamaa mmoja anaongea na simu anasema " ndo nipo kiboroloni hapa nataka nipande town mara moja" , basi nikajua ile sehemu panaitwa kiboroloni, mbele kidogo kulikuwa na semitrailer limepaki pembeni, nikafika pale milango ya gari imefungwa, lengo langu ni kuwa kama linaenda dar niombe lift,
Basi akili ikanituma nisubiri pale mpaka dereva aje, nilikaa pale mpaka giza likaanza kuingia, nikasema sasa hata akija akikataa itakuwaje, ni bora nitafutet sehemu kwenye hili gari nijibanze hivyohivyo, basi nikapanda pale katikati ya tela na kichwa nikakaa, mtu anaweza asinione maana ilikuwa imebeba kontena lile kubwa,
Nikakaa sana pale, nikahisi mkojo umebana, basi nikashuka chini nikazunguka nyuma ya gari nikakojoa, kumbe lile kontena lipo wazi mlango mmoja, nikapata wazo nipande niingie ndani ya lile kontena, basi nikajivuta nikapanda, nikaingia, nikacheki kama kuna mtu kaniona nikaona kimya, nikakaa mwishoni mwa ule mlango ulofungwa kwenye kona kabisa kiasi kwamba ni ngumu mtu kuniona, nikakaa mpaka usingizi ukanipitia,
Nilipo kuja kushtuka nikakuta ngoma inatembea, imechanganya kinyama, nikasema weweiyaa!!!, Shida sijui sasa inaenda wapi, potelea mbali itakavyokuwa ndo hivyo hivyo, ila nikajipa matumaini ilikuwa imepaki kuelekea dar,
Basi ngoma ina amsha , mi nalala nashtuka nalala nashtuka chuma inaambaa tu, basi nilipokuja kushtuka kumeanza kupamba zuka chuma bado inaamsha, tukafika sehemu ikapaki, ni kwenye kamji hivi kamechangamka, tukakaa pale kama masaa mawili hivi, mara chuma ikaamsha tena, tukafika sehemu ikasimama tena, nahisi pale walisimamishwa na trafiki, nikasema nichungulie nje kidogo nikaona jengo limeandikwa TRA Segera, nikajua kumbe tumefika segera,
Basi ngoma ikaamsha tena, jamaa sijui alikuwa anawahi wapi maana hapotezi muda, Huwezi amini nilikuja kushtukia mataa ya ubungo haya hapa, nikasema khaah! Sasa hapa nishuke niende zangu msewe kwa Da J,
Ila gari haisimami sasa, yaani ikisimama kidogo nafikiri nifoleni ile nasema nitoke sasa chuma inang'oa daah! , Mara Tazara hii hapa, nikajua itasimama maana najua tazara kunakuwaga na foleni lakini wapi, ngoma ikaunga kama inaenda uwanja wa ndege, nikasema hii hatari sasa, kama vipi nitulie tu mpaka itakapo simama,
Basi nafkiri ilikunja jeti pale maana badae sikuiona tena ile barabara ya nyerere, Chuma ikatembea mpaka ikafika sehemu kuna geti ikazama ndani, ikaenda ikapaki, nikachungulia huko nje naona malori mengi kama yard vile, alafu kuna geti na walinzi wa kk, ukuta wa hiyo yard ni mkubwa na kuna nyaya zile zenye umeme zimepita juu ili mtu asiruke,
Daah! sasa ntatokaje tena humu ndani, hili mbona balaa jingine tena, nikichungulia naona ma mbwa yanazunguka zunguka humo ndani, aisee hiki kimbembe tena, nikasema hapa polisi pananihusu tena, nikiulizwa nimeingiaje humu ndani nitasemaje, na nilikuwa natafuta nini,
Itaendelea
Jamaa. Mbona kasema wazi zaidi ya Sehemu 3 gari ilisimamishwa ikiwemo Eneo la TRA.Kwa mara ya kwanza gari inatembea moshi tu dar bila mtu kuchungulia kontena.ukaguzi unafanyika bila kuchungulia ata nyuma. Gari inafika dar hakuna mahali imesimama ata kwenye taa au foleni aisee. Simulizi imefika patamu
Kaibe na wewe tuendelee burudika kwani nani kakataa ilimradi burudani na mafundisho yapoUkichukua kitu cha mtu bila idhini yake ni wizi. Na yeye kumbuka hii story si yake.
Yaani ubungo hadi jet no trafick lights wala foeni na kontena lipo wazi? Story ilikuwa mzuri ila imeanza kuharibikia moshi. Tusome tu for funKwa mara ya kwanza gari inatembea moshi tu dar bila mtu kuchungulia kontena.ukaguzi unafanyika bila kuchungulia ata nyuma. Gari inafika dar hakuna mahali imesimama ata kwenye taa au foleni aisee. Simulizi imefika patamu
Uwe unaelewa ,sio kila sekta unajifanya unajua Ila ni kawaida yetu Mana diwani anamshauri Engineer,na mkurugenzi anamhukumu daktari.Kwa mara ya kwanza gari inatembea moshi tu dar bila mtu kuchungulia kontena.ukaguzi unafanyika bila kuchungulia ata nyuma. Gari inafika dar hakuna mahali imesimama ata kwenye taa au foleni aisee. Simulizi imefika patamu
Ivi mkuu ikiwa ukweli ama uwongo unapata faida gani Kwani ama umesikia kuwa utaombwa hela umsadie. Conserve huo ubongo uutumie kwenye masuala ya msingi wa maisha. Tunapenda uwe Kama bakheresa ama dangote ili utoe ajira kwa vijana wetu na ulipe Kodi shule hospital maji yafikie Taifa.please don't jaribu that energy of your brainYaani ubungo hadi jet no trafick lights wala foeni na kontena lipo wazi? Story ilikuwa mzuri ila imeanza kuharibikia moshi. Tusome tu for fun
Yaani unajua how dog fucks...😂😂😂😂Achana na huyo mbwa
Duh mwamba unasoma kweli? Kataja mpaka TRA, UBUNGO, TAZARA.Yaani ubungo hadi jet no trafick lights wala foeni na kontena lipo wazi? Story ilikuwa mzuri ila imeanza kuharibikia moshi. Tusome tu for fun
Umekosoa kwa machungu sana kama vile umetoza hela😅Kwa mara ya kwanza gari inatembea moshi tu dar bila mtu kuchungulia kontena.ukaguzi unafanyika bila kuchungulia ata nyuma. Gari inafika dar hakuna mahali imesimama ata kwenye taa au foleni aisee. Simulizi imefika patamu