Akhi
JF-Expert Member
- Jul 12, 2021
- 3,380
- 5,906
hya kalale sasaPhew!!! nimeusoma uzi Usiku kucha.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hya kalale sasaPhew!!! nimeusoma uzi Usiku kucha.
Jamaa bado ana roho ya wizi. Kma ambavyo aliiba laptop na akataka kuiba simu arusha. Na anaendelea kuiba story ya watu kwa mujibu wa masimulizi yake😁Nawewe ipeleke ukapige pesa. Muhusika kaamua kuitoa free we unaumia nini!!??
Wapi ameandika kwamba alitaka kuiba simu Arusha?!Jamaa bado ana roho ya wizi. Kma ambavyo aliiba laptop na akataka kuiba simu arusha. Na anaendelea kuiba story ya watu kwa mujibu wa masimulizi yake😁
Yaah sure....Mara nyingi huwa wanasimulia wakiwa successful. Ukiwa bado failure story zako zitakuwa takataka. I hope now is successful
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Joan unapenda utamu weweMkuu nia yako Nini haswa?Unataka utamu uishie njiani?
na vyeti walishampiga moshi unahisi itaishiajeNatamani kusikia mwisho wa stori imeishia happy ending au ndio bado anapuyanga.
Kweli kabisa mkuuNi very frustrated. Hata thinking yake haipo vizuri kwa wakati huo
[emoji23][emoji23]Haiwezi kua hivyo maana story itakua fupi. Kuongeza matukio ndio story sasa
Alitaka kuiba simu full stop anauzuga tu hapa,huyu ni mwiziWapi ameandika kwamba alitaka kuiba simu Arusha?!
Let we wait the endYaah sure....
Hatari na nusu. Mwagilia moyo mtu wangu. UmetishaSEHEMU YA KUMI NA TISA
Ilipoishia,,,,,,,,,,,,,
Nikakaa pembeni ya mto pale nikamalizia vitunda vyangu, nikanywa maji tena nikajiskia fresh sasa, nikavuka ule mto nikaendelea na safari yangu, nikatembea mpaka msitu ukaisha nikatokea kijijini,
Endelea,,,,,,,,,,,,,,,,
Nikatembea mpaka nikafika kwenye nyumba moja hivi ya udongo, nje kuna watu watu pale wanapiga ulabu, wakawa kama wananishangaa ila mi sikujali, nikanyoosha mpaka kwa mzee mmoja ambaye nilimwona ndo anahudumia pale, nikamsalimia, nikamwambia mzee samahani naomba nisaidie maji ya kunywa, basi mzee akazama ndani akatoka na jagi la maji na kikombe kikubwa, akataka kunimiminia nikamwambia usijali,nikachukua lile jagi na kile kikombe nikaenda kukaa kwenye jiwe pale pembeni nikapiga vikombe vyangu viwili nikatulia,
Basi nikakaa pale nafikiria maana ingawa nilikunywa maji ila kiukweli nna njaa, basi kumbe wale watu bado wananicheki tu, yule mzee akaja akaniuliza vipi we ni mgeni eneo hili, nikamjibu ndio, akauliza umetokea wapi, nikaogopa kumwambia nimetoka jela, nikamwambia nimetoka tabora nimekuja kutafuta kazi, mzee akacheka sana, akasema sasa huku yenyewe vijana hawana kazi na wewe tena unakuja kutafuta kazi, nikamwambia kila mtu na bahati yake, akasema kwaiyo saivi unaelekea wapi, nikamwambia sina mwelekeo wowote,
Basi tukapiga stori na mzee pale nikamweleza jinsi maisha yalivyo magumu kijijini kwetu mpaka nikaamua kuja huku kutafuta kazi, mzee akaniambia kazi za pale kijijini nyingi ni kilimo, mzee ana roho nzuri sana , sijui alijua nna njaa, akamwagiza kijana wake aniletee ugali, kweli mzee ukaja ugali na mboga za majani pale nikapiga, nikanywa na maji nikajiskia nina nguvu sasa,
Nikamwomba mzee nikae pale kwake siku chache wakati natafuta muelekeo, mzee hakuwa na hiyana ila pa kulala ndo shida, akasema kama nitaweza kulala jikoni sawa, nikamwambia mzee haina shida mi nalala fresh tu,basi akamwita mzee mwingine pale akamwelezea, yule mzee nae akaniuliza maswali maswali nikamjibu nikaona katulia, badae nilikuja kujua kumbe yule ndo mwenyekiti wa kijiji,
Nikakaa kwa mzee pale nikawa nasaidia saidia kazi pale nikishirikiana na kijana wake,mzee hana mke, anajishughulisha na kilimo na uuzaji wa pombe za kienyeji, nikaja gundua mpaka gongo anauza ila kwa kificho sana,
Basi nilikaa kwa mzee kama wiki mbili hivi, nikiwa pale nikataka niombe simu nimpigie Sity au Da J ila namba zao kwani nazikumbuka hata!,
Basi siku moja tupo pale, watu kibao wanapiga ulabu, kelele za kutosha, mzee akatuita mi na kijana wake kwa siri, akasema pale mzigo umeisha, tuchukie baiskeli tukimbie tukalete fasta ila tuwe makini huko njiani, mi hata sijui mzigo gani, basi tukachukua baiskeli na kidumu cha lita tano kwenye kisafleti tukaondoka hata sijui tunaenda wapi,
Kijana anagonga pedeli huyo!, Mara tukazama msituni, tunapita kwenye vichochoro huko msituni, tukafika sehemu tukakuta ule mto, tukaacha baiskeli sehemu, tukatembea kidogo kuingia ndani ndani, kufika nilishangaa sana, nilikuta majamaa yametengeneza mtambo huo wa kutengeneza gongo, wale jamaa ni wanasayansi sema hawajui, ile ni simple distilation kabisa, Basi yule kijana akaenda kuongea nao pale akawapa kile kigaloni tukawa tunasubiri,
Tukiwa tumesimama pale tunasubiri hatuna lile wala hili ghafla tukaskia sauti nyuma " mpo chini ya ulinzi, mikono juu, asikimbie mtu" , kumbe ni polisi mzee!!, wale jamaa wakatoka nduki kwenye vichaka huko, tukabaki mimi na yule kijana tumeduwaa pale hatujui cha kufanya,
Tukakamatwa pale tukapigwa mitama tukakaa chini, tukafungwa mashati, wakamwaga ile pombe iliyokuwa kwenye pipa ambalo ndo wametengenezea ule mtambo, wakachukua lile pipa na vifaa vingine, kumbe walikuja na gari wamelipaki mbali kidogo, tukatembea paka kwenye gari tukatiwa ndani, wakapakia na yale mamtambo chuma ikaamsha,
Niko kwenye gari nna waza hiki ni nini tena, nikasema yaleyale yanaanza tena, huu mzimu wa mikosi utaniandama mimi mpaka lini, nikimwangalia yule dogo hana hata wasiwasi, sijui ameshazoea yale mambo!,
Basi ndinga ikatembea mpaka kituo cha polisi majengo, wakati tunashuka nawaza hivi hawa askari si watanikumbuka tena mimi, Tukaingizwa ndani tukachukuliwa maelezo, ikabidi nidanganye jina ili wasije nikumbuka, Tukasweka ndani kwenye kile kiselo, tukakuta masela wengine humo ndani,
Tulikaa mule ndani mpaka usiku ukaingia, tukalala selo, Kesho yake Asubuhi tukaitwa, kutoka tukakuta mzee kaja kaleta na chai pale tukapiga, Basi mzee akafanya mpango pale tukaachiwa, tukatoka nje,mzee anatupa pole anasema ndo maisha hayo ya kumjenga mwanaume, kimoyo nikasema lait angejua kwangu hichi ni cha mtoto, niliyopitia ni makubwa kuliko hili,
Basi tulipotoka pale nje kile kituo hakipo mbali na barabara kubwa, nikawa naona mabasi yanapita,malori yanapita nikasema ile barabara itakuwa ya kwenda dar, nikakumbuka sana dar, mzee akasema pandeni baiskeli twendeni, nikamwambia mzee mi sirudi tena kule, nataka nikatafute gari nirudi nyumbani, mzee akasema sawa hamna shida ,safari njema, basi wakagonga pedeli wakasepa,
Mi nikatembea mpaka pale barabarani nikamuuliza mtu hii barabara inaenda wapi, akasema huku inaenda moshi stand huku inaenda njia panda na dar nikasema asante, nikashika ile ya kwenda dar, nikasema leo ntaenda dar hata kwa miguu, maana huu mji umenikataa, watu wa huku makatili sana,
Nikatembea nafata barabara tu huku nawaza mambo mengi kichwani , nikafika sehemu miguu inauma sasa, nikasikia jamaa mmoja anaongea na simu anasema " ndo nipo kiboroloni hapa nataka nipande town mara moja" , basi nikajua ile sehemu panaitwa kiboroloni, mbele kidogo kulikuwa na semitrailer limepaki pembeni, nikafika pale milango ya gari imefungwa, lengo langu ni kuwa kama linaenda dar niombe lift,
Basi akili ikanituma nisubiri pale mpaka dereva aje, nilikaa pale mpaka giza likaanza kuingia, nikasema sasa hata akija akikataa itakuwaje, ni bora nitafutet sehemu kwenye hili gari nijibanze hivyohivyo, basi nikapanda pale katikati ya tela na kichwa nikakaa, mtu anaweza asinione maana ilikuwa imebeba kontena lile kubwa,
Nikakaa sana pale, nikahisi mkojo umebana, basi nikashuka chini nikazunguka nyuma ya gari nikakojoa, kumbe lile kontena lipo wazi mlango mmoja, nikapata wazo nipande niingie ndani ya lile kontena, basi nikajivuta nikapanda, nikaingia, nikacheki kama kuna mtu kaniona nikaona kimya, nikakaa mwishoni mwa ule mlango ulofungwa kwenye kona kabisa kiasi kwamba ni ngumu mtu kuniona, nikakaa mpaka usingizi ukanipitia,
Nilipo kuja kushtuka nikakuta ngoma inatembea, imechanganya kinyama, nikasema weweiyaa!!!, Shida sijui sasa inaenda wapi, potelea mbali itakavyokuwa ndo hivyo hivyo, ila nikajipa matumaini ilikuwa imepaki kuelekea dar,
Basi ngoma ina amsha , mi nalala nashtuka nalala nashtuka chuma inaambaa tu, basi nilipokuja kushtuka kumeanza kupamba zuka chuma bado inaamsha, tukafika sehemu ikapaki, ni kwenye kamji hivi kamechangamka, tukakaa pale kama masaa mawili hivi, mara chuma ikaamsha tena, tukafika sehemu ikasimama tena, nahisi pale walisimamishwa na trafiki, nikasema nichungulie nje kidogo nikaona jengo limeandikwa TRA Segera, nikajua kumbe tumefika segera,
Basi ngoma ikaamsha tena, jamaa sijui alikuwa anawahi wapi maana hapotezi muda, Huwezi amini nilikuja kushtukia mataa ya ubungo haya hapa, nikasema khaah! Sasa hapa nishuke niende zangu msewe kwa Da J,
Ila gari haisimami sasa, yaani ikisimama kidogo nafikiri nifoleni ile nasema nitoke sasa chuma inang'oa daah! , Mara Tazara hii hapa, nikajua itasimama maana najua tazara kunakuwaga na foleni lakini wapi, ngoma ikaunga kama inaenda uwanja wa ndege, nikasema hii hatari sasa, kama vipi nitulie tu mpaka itakapo simama,
Basi nafkiri ilikunja jeti pale maana badae sikuiona tena ile barabara ya nyerere, Chuma ikatembea mpaka ikafika sehemu kuna geti ikazama ndani, ikaenda ikapaki, nikachungulia huko nje naona malori mengi kama yard vile, alafu kuna geti na walinzi wa kk, ukuta wa hiyo yard ni mkubwa na kuna nyaya zile zenye umeme zimepita juu ili mtu asiruke,
Daah! sasa ntatokaje tena humu ndani, hili mbona balaa jingine tena, nikichungulia naona ma mbwa yanazunguka zunguka humo ndani, aisee hiki kimbembe tena, nikasema hapa polisi pananihusu tena, nikiulizwa nimeingiaje humu ndani nitasemaje, na nilikuwa natafuta nini,
Itaendelea
Nimeshaandaa pop corn za kutosha namuwinda Akili SinaMara kwa Mara nachungulia hii thread kama kuna muendelezo😜
Anagusia vitu muhimu story akiandika mpk ukaguzi af asionwe c ndo mtadai Ni chai af wewe c ndo choko lile la juu libishi au wewe choko mpya??
Dah, ngoja nianze mwanzo kabisa maana imekuwa ishanipita.Stephen Chelu hii sitaki ikupite brother
mzuka wa kuandika ukishapanda mtu anaweza kuandika usiku mzima na asichoke.Kichwa cha habari hii kimejitosheleza. Bado ulienda kusikojulikana. Ila Kuna mijitu ina comment upuuzi kwanza Mimi sisomi ni mwendo wa......
ilipoishia...Sasa endelea....itaendelea
Kwa sababu asikuambie mtu, bwana, kuandika vizuri kawa flow ya stori hivi ndg engineer amejitahidi. Lkn nawaza hwa watoa stor hivi mnafsnyaje huko behind the scenes,huwamnazi hariri Sana? Unatumia dakika au Muda Gani kuandika episode. Mnaokoment hovyo Pana kitu mnakosa sana
kwa nini walimpiga arusha na alifungwa? kwa mujibu wa mtunzi wa hii hadithi.Wapi ameandika kwamba alitaka kuiba simu Arusha?!
Mkuu unajidhalilisha sana kama unaweza jaribu kusoma kimyakimya bila kuchangia chochote maana kupitia story hii nimegundua wewe ni mweupe sana kichwani.kwa nini walimpiga arusha na alifungwa? kwa mujibu wa mtunzi wa hii hadithi.
sana nina mvi.... ni mweupe. wewe mwekundu? wewe mbona hujasoma kimya kimya? kuchangia ni haki yangu maana kama ameweka public ina maana ni kwa watu wote nmegundua wewe ni mweusi kwenye ubongo wako .... huna kitu. 😂Mkuu unajidhalilisha sana kama unaweza jaribu kusoma kimyakimya bila kuchangia chochote maana kupitia story hii nimegundua wewe ni mweupe sana kichwani.