Usilogwe ukaondoka nyumbani na kwenda usipopajua kwa kigezo cha kutafuta maisha

Mtoa story kama ni story ya ukweli basi mtoa mada ni msimulizi mzuri na mwandishi hodari, kama niyakutunga mmsimulizi ni mwerevu sna , kama kakopy mahali basi mtoa mada anajua watu wanataka nini na anafaa kuwa kiongozi hodari.[emoji122]
Kuna daadhi ya mambo amehadithia mtoa mada hayawezi kuwa chumvi, kama mazingira huko moshi majengo, kwa namna anavyoyazungumzia mtoa mada napafahamu vizuri
 
SEHEMU YA ISHIRINI

Ilipoishia,,,,,,,,,,,,,,,

Daah! sasa ntatokaje tena humu ndani, hili mbona balaa jingine tena, nikichungulia naona ma mbwa yanazunguka zunguka humo ndani, aisee hiki kimbembe tena, nikasema hapa polisi pananihusu tena, nikiulizwa nimeingiaje humu ndani nitasemaje, na nilikuwa natafuta nini

Endelea,,,,,,,,,,,,,,

Nilikaa sana ndani ya lile kontena nikiwaza ni jinsi gani nitatoka mule ndani, changanya na njaa nliyokuwa nayo, yaani tumbo ni linawaka moto kwa njaa maana sikuwa nimeweka kitu tumboni toka nimekunywa chai pale kituo cha polisi, nikawaza niende nikawaombe wale walinzi nitoke ila wakiniuliza nimetokea wapi nitajibu nini, na nimeingiaje mule ndani nani atanielewa si ndo kupelekana polisi huko na nilivyo na nyota ya kirungu kupendwa na polisi,

Istoshe pia mule ndani kuna ma mbwa yanatembea tembea inamaana nikitia mguu chini tu nnalo, si ndo kuitwa mwizi tena huko,

Nikawa sina jinsi zaidi ya kutulia tu kule ndani ya kontena nikisubiri kudra za mwenyezi Mungu, mpaka giza linaingia bado nipo mule ndani, njaa ndo imechachamaa huko tumboni asikwambie mtu,

Muda ukiwa umeenda, sijui hata ilikuwa sa ngapi, nikiwa nimejikunyata ndani ya kontena mara nikasikia nje watu wanaongea, kupiga jicho nikaona wanakuja kwenye lile gari wana tochi inamulika, Wakafika pale nyuma ya gari wakasimama wakawa wanaongea, nikasikia mmoja anasema " inabidi uwahi maana kibali kina expire saa sita " , mwingine akauliza " kwani linashukia wapi? " Akajibu " Fantuzi", Mwingine akasema akasema " Kagua kontena kabisa kama lipo safi wasije wakakuzingu, mi staki mambo ya kupigiana simu usiku",

Moyo ukadunda kichizi, nikajua sasa hapa ndo nakamatwa mzee, basi jamaa nikamsikia " kontena ni safi halina shida " huku wana mulika ndani ya kontena, uzuri nilikuwa nimejibana kwenye kona ya ule mlango uliofungwa kwaiyo ilikuwa si rahisi kuniona labda aingie kabisa ndani ya kontena, basi wakaondoka , angalau moyo ukapumua,

Sjakaa sana nikasikia chuma imewaka, nikasema linatoka nini!!, Kweli likaanza kuondoka kuelekea getini, kufika getini likasimama, walinzi wakapigapiga tochi ndani ya kontena ila nao hawakuniona , wakafungua geti chuma ikatoka, nikasema daaah Mungu kweli kasikia maombia yangu,

Chuma ikakamata road, ikachanganya kama kawaida yake, ila nikasema sifanyi tena ule ujinga, saivi hata iweje naruka, basi nikatoka kabisa nikachuchumaa mlangoni natafuta chance ya kuruka, ila gari imechanganya mzee! Ikipunguza mwendo nikitaka kuruka unakuta nyuma kuna gari inakuja speed, nikasema leo!!!

Basi chuma ikakata Tazara kama inaelekea bandarini , mwendo ni uleule, ilipofika sokota ikaacha lami ikaingia rough road, kidogo ikawa hafadhali maana likawa haliendi speed sana, mbele mbele kidogo likasimama, nikaruka, kumbe pale ni foleni kubwa ya malori yamebeba makontena, basi pale ndo nikajua kumbe lilikuwa linaenda kushusha lile kontena bandarini,

Sasa basi usiku umeingia, njaa inauma, sina hata mia mfukoni, nafanyaje, nakula wapi, nalala wapi! Nikawa natembea tu kurudi barabarani, ila wazo likanijia, sasa hivi ni usiku, huku sokota mida hii si kuzuri kabisa, kama sitakutana na polisi basi nitakutana na vibaka wanifanyie uhuni, nikaingia kwenye kibanda kimoja cha wale mama ntilie wanaouza chakula pembeni mwa barabara, nikakuta kuna viroba kule chini,nikatandika nikalala, ila ukiwa na njaa usingizi hauji kabisa, nikawa nawaza kesho itabidi niende msewe kwa Da J,

Sijui nilipitiwa saa ngapi na usingizi, ila nilikuja kushtuka karibu kunapambazuka, wale mama ntilie wameshaanza kufungua vibanda vyao, basi nikatoka mule ndani haraka wasije wenyewe wakanikuta, nikaaza kutembea kurudi barabara kubwa, kukakucha kabisa watu wakaanza kuwa wengi pilikapilika zikaanza,

Nikafika sehemu nikakaa kwanza maana nisingeweza kutembea mpaka ubungo na njaa yote ile, Nikawaza niombe hela wapita njia ninywe hata chai maana niliona nitakufa,

Nikatoka pale nikaanza kuomba hela wapita njia, wengine hawataki hata kuniangalia nikianza tu kuomba unaona huyo anakula kona, nikasema daah watu hatupendani, wengine nahisi walijua mi ni kichaa au tapeli,

Basi mzee mmoja tu ndo alinipa buku nikasema si mbaya, nikazama kibanda kimoja nikaagiza chai na chapati za ile hela, nikapiga pale nikanywa na maji, kidogo ikawa afadhali,

Nikatoka pale saivi nina nguvu, nikashika barabara kubwa ya kuja tazara, lengo langu niende msewe kwa Da J , Nikatembea nikapita tazara, nikafika buguruni nikakumbuka zile mishemishe zangu za usiku kipindi nasoma, nikamkumbuka Jane, nikasema ingekuwa ni usiku ningeenda kumtafuta Jane, ila kwa jinsi nilivyochoka anganikubali kweli!, au ndo angevunga hanijui, maana wale wanaangalia hela, wapo kibiashara zaidi,

Nikapita zangu nikaendelea na safari yangu, nikafika tabata nikawa napita pembeni kwenye malori yamepaki pembeni, kichwani nna mawazo kedekede, hivi Da J nitamwambia nini, nitamwambia niketokea wapi, hivi nitamwambia madhila yote yaliyonikuta moshi, banaee!! nitajua nikifika,

Nikiwa katikati ya lindi la mawazo mara nikashtuliwa na sauti ya mtu ananiita kutoka kwenye yale malori yaliyopaki pembeni ya barabara, nikageuka kumcheki anaye niita, nikamwona jamaa yupo ndani ya lori ananiita, nikajiuliza haraka haraka huyu jamaa ni nani, nikavuta kumbukumbu nimemwona wapi lakini siipati picha yake,

Basi nikasema niende kumsikiliza, nikafika pale akanipa hi, ebwana vipi!!, Nikamjibu poa, akaniambia ebu zunguka hivi mcheki suka anakuita, basi nikazunguka upande wa dereva,

Ebwanaaee!! Sikuamini, kumcheki jamaa kumbe ni Abduli kisoda tulisoma nae pugu, Daah basi akashuka kwenye gari tukasalimiana, akasema amenicheki muda toka nikiwa mbali akadhani kanifananisha, nikamwambia hujanifanisha ndo mimi mwenyewe akili sina,

Basi tukaenda sehemu kuna ka grosari tukakaa tukaanza kupiga story, tukapiga stori sana, za pugu tulipokuwa tunasoma, stori za mabomu daah tulifurahi sana kuonana,

Akaniambia yeye baada ya matokeo kutoka yakawa si mazuri akaamua kujichanganya kwenye magari,maana anko wake ni dereva, basi akatembea na anko wake mpaka akawa dereva, saivi ,yupo pale wamepakia diseli wanaenda kongo, daah mi nikaona jau kumwambia kuwa nilienda chuo, mi nikamwambia nilipotoka pale nikaanza biashara biashara sema mambo hata hayakukaa poa,

Akaniuliza kwaiyo saivi unakaa wapi, ikabidi nimpe ukweli tu kuwa mi sina makazi maalumu nipo tu naranda randa mtaani, Kisoda alisikitika sana ukitegemea tulikuwa washkaji sana pindi tunasoma, akasema kama vipi nijichanganye na mimi kwenye magari, nikamwambia nikipata hiyo chance mbona nitashukurua sana, akasema tunaweza kwenda mpaka kongo, huko njiani nitajifunza kuendesha gari, nikamwambia ila mimi pasport yae kusafiria sina ntaendaje huko kongo, akasema kuna za muda mfupi tutakata huko njiani, nikasema kama inawezekana ni sawa mi nitashukuru sana maana atakuwa amenipa zaidi ya msaada,

Basi mchana ulikuwa umeshaingia akaagiza msosi ugali samaki tukapiga pale, Nikimcheki kisoda nikajilaumu sana , kwa nini na mimi nisingejiingiza huku kwenye magari mapema, maana kisoda kanawiri, kapiga pamba safi, yaani mimi na yeye tofauti sana, nikajilaumu kwenda chuo, vyeti vyenyewe hata sina tena,

Basi nikamaliza pale, nikatafuta sehemu nikaenda kupiga maji maana nna siku kadhaa sijaoga, Tukarudi kwenye gari abduli akanipa kadeti yake nyeusi na t-sheti nikavaa kidogo na mimi nikaonekana mtu, akaniambia wanasubiri mida ya saa kumi hivi jua likipungue waamshe, kumbe yule jamaa mwingine na yeye ni dereva gari lake kapaki nyuma ya lile, basi tukakaa ndani ya gari tunaendeleza stori, safari ya msewe ndo ikaishia hapo,

Itaendelea
 
Sema mwanangu una mbwela sana
Kwa siku ungewapa wadau hata episode 2
 
Back
Top Bottom