Usilogwe ukaondoka nyumbani na kwenda usipopajua kwa kigezo cha kutafuta maisha

Nchelenge
Polish_20220527_192534615.jpg
 
Yaani anachopitia huyu bwana mdogo ni ile slogan ya UTAPATA TAABU SAANA! Ikinanakshiwa na KUFA HUFI ILA CHA MOTO UTAKIONA.

Lakini Akili Sina kuna fursa pia naziona kupitia hii story, kwakuwa inavuta hisia na kusisimua, inaweza ikanunuliwa na vituo vya radio na kusimuliwa kwenye kipindi kama njiapanda ya clouds fm.
Au
Ikatengenezewa movie kama ile ya Nairobi HalfLife.

SIKU ZOTE CHENYE THAMANI NI KILE KILICHODHARAULIKA.

Unaweza ukasema unapiga tu story kujifurahisha na wanajamvi lakini ya Mungu mengi, anaweza akajitokeza mtu akakushika mkono, hii story ikakulipa mpaka ukashangaa.
Ikikaziwa na "UTAJUA HUJUI"
 
Naam hatimaye story imefika mwisho big up sana kiongozi.kwa maoni yangu ni kuwa hii story inaukweli 70% ,30% iliyobaki ni chai na vitumbua vyake.
story ya kweli ilishia pale jamaa anatoka polisi moshi na kuingia kwenye kontena la lori linaloelekea dar huku kwengine chai nyingi kuliko ukweli.hasa kwenye story yake ya kimahusiano.but anyway you're a good storyteller mkuu keep it up.
 
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA

Ilipo ishia,,,,,,,,,,,,

Basi nikamaliza pale, nikatafuta sehemu nikaenda kupiga maji maana nna siku kadhaa sijaoga, Tukarudi kwenye gari abduli akanipa kadeti yake nyeusi na t-sheti nikavaa kidogo na mimi nikaonekana mtu, akaniambia wanasubiri mida ya saa kumi hivi jua likipungue waamshe, kumbe yule jamaa mwingine na yeye ni dereva gari lake kapaki nyuma ya lile, basi tukakaa ndani ya gari tunaendeleza stori, safari ya msewe ndo ikaishia hapo,

Endelea,,,,,,,,,,,,,,,

Mida ya jioni hivi jua limepungua chuma ikainga road, nimekaa kushoto mzee naona Abdul anavyocheza na gear basi naona raha kweli, natamani na mimi ningeweza, Chuma ni kubwa lakini anavyoendesha utazani anaendesha gari ndogo, anavyokwepa magari kwenye foleni utazani nyuma hana kitu kumbe ana bonge la tanki huko nyuma,

Basi bana tukapambana na foleni ya ubungo palee mpaka tukatoboa, tukakamata morogoro road nikaona kidaraja chetu kile cha kwenda msewe, nikakumbuka mbali sana, Basi chuma hiyo inaambaa mzee, Kisoda ananikumbusha stori zake za shule pale ili mradi stori ziendelee,

Basi nikawa kama utingo sasa, tukikaribia mizani chuma inapaki pembeni tunaanza kuikagua, maana kisoda aliniambia mizani wanazingua kichizi, tairi ikiwa haina upepo au umepungua, au busta haina upepo au gari ikidondosha mafuta faini ni dola elf 2, basi nipo na tambara langu nikiona hata dalili ya mafuta nafuta, gonga gonga matairi yote yapo freshi, cheki busta ziko freshi basi ngoma ikaingia mizani vigwaza pale, nikashuka nikapeleka kadi dirishani akaniuliza mnaenda wapi nikamwambi kongo, akaniprintia risiti pale tukaamsha zetu,

Kwaiyo hiyo ndo ikawa kazi yangu, tulipofika mikese giza limeshaingia tayari, tukakuta ile mizani haifanyi kazi siku ile jamaa wakatuambia tuamshe basi kisoda akatia gia tukatambaa,

Morogoro tukaingia kama saa mbili mbili hivi, kisoda akaniambia tusogee tukalale melela nikamwambia poa , Basi chuma inaamsha tu , huko ndani inapiga mziki basi ni burudani a/c kama yote, yaani ile chuma mule ndani hata geto halifikii,

Kweli bana tukafika melela pale kuna parking kubwa tu malori mengi hasa ya mafuta yanapaki pale sikujua kwa nini,
Basi tukapaki gari pale tukaanza kutafuta msosi, tukapiga msosi tukarudi, pale kuna bar wanaonyesha mpira tukakaa pale tunacheki gemu ya man u na chelsea, muda ukafika tukarudi kwenye gari tukalala, ile gari ina vitanda viwili cha juu na cha chini,

Basi kesho yake saa kumi na moja alfajiri chuma ikakamata road, ni mpera mpera tu, sema uzuri wa ile gari huchoki humo ndani, basi tukapita mikumi tukaona wanyama, swala kama wote, punda milia, twiga, simba tu ndo sikubaatika kuona, basi kazi yangu ndo ikawa ileile tulipofika mzani wa mikumi, tukapita pale chuma inatambaa usiseme, basi chuma ina lala na kona balaa, kisoda akaniambia ukisikia kona za iyovi ndo hizi, mabasi yanaanguka sana kule,

Haya bana tukafika kitonga, mi nlikuwa napasikia tu kumbe pana tisha sana ukichungulia huko chini, gari ikawa inapanda mdogo mdogo, naambiwa ni kilomita 8 tu lakini magari mengine yanaweza kupanda kuanzia asubuhi paka jioni,

Tukasimama ruaha mmbuyuni pale tukapiga lunch, tukamaliza ngoma ikaamsha hiyo, tukaingia makambako jioji jioni hivi, Kisoda akasema tulale hapa ili kesho tukate pasport hapa, nikasema sawa,

Tukalala pale, baridi kishenzi yani, Asubuhi tukaenda ofisi za uhamiaji pale kukata passport ila mtandao ukawa unasumbua, tukakaa sana pale mwisho tukasema tuondoke tutakatia mbele, basi chuma ikaamsha, tukaingia tunduma jioni hivi, tukapaki sehemu mmoja paitwa uzunguni,

Basi kesho yake Kisoda akanipa hela niende vwawa ndo kuna ofisi za uhamiaji nikakate pasport, yeye akaenda castum kufatilia documents, basi nikapanda dala dala paka vwawa, nikaulizia nikafika hapo uhamiaji, nikafanikiwa kupata passport, nikageuza mpaka uzunguni, Nikamkuta kisoda pale tukaenda kupiga menyu pale fresh,

Kesho yake akasema inabidi twende boder ili nikakate chanjo, basi tukapanda daladala tukaenda, basi tukaingia mule ndani ya ule mjengo pale custom, tukafanya process zetu pale fresh, basi ikatakiwa nikachome sindano nikaelekezwa chumba kimoja hivi, kisoda nikamuacha pale ananisubiri,

Nikachomwa pale, nikapewa na cheti changu cha chanjo, sasa wakati natoka ule mjengo ni mkubwa sa sielewi tena njia ya kutokea, nikasema haina shida si kuna vibao vya exit, nikawa nafata vile vibao, kweli nikafanikiwa kutoka nje,

Sasa ile naondoka mara mlinzi mmoja akaniita, nikaenda pale kwenye chumba chao, akaniambia we umetokea mlango gani, nikamwambia ule pale, akasema unajua kazi ya ule mlango, nikamwambia mi sijui, nimeona mshale unanionesha kutoka mi nikatoka,

Ebwanaee!! Acha wanicharukie, wakasema unajua maana ya ule mlango wewe, ule ni mlango wa dharura , yaani ukifungua tu ule mlango alarm inalia hadi kwa mkurugenzi, sa mi nikawaambia mi nlikuwa sijui, na kama ni wa dharura mbona haujaandikwa, basi wakasema we unajifanya una kiburi eeh, kwanza kaa chini, nikaona isiwe shida nikakaa, kuna kamlinzi kadada hako ndo kamenicharukia balaa, we utaenda kutusaidia kujibu kwa mkurugenzi wewe, basi mi nikakaa kimya tu nawaacha wanabwabwaja pale,

Wakawa sasa wanataka hela ili waniachie, nikawambia hapa nilipo sina hata mia mbovu, wakasema we unakiburi wewe basi utakaa sana hapo, basi mi nikakaa, nawaza kisoda atakuwa kanitafuta sana,

Wakaniweka pale kama masaa manne hivi , walipoona nimekomaa sina hela wakaniambia pita pale usepe, nikapita getini pale nikatokea barabara ambayo ndo magari yanavuka kuingia zambia,

Sasa hii ishakuwa balaa , sina simu na hata ningekuwa na simu namba ya kisoda sikuchukua,

Niikatembea mpaka round about, nikasema sasa hapa nitembee mpaka uzunguni maana ningekuwa na hela ningepanda daladala, wakati natembea nikapata wazo, kwanini nisiombe lift, nikaona lori linakuja taratibu, nikamwomba suka , naomba niache uzunguni broo, kweli akasimama nikapanda, nikafika mpaka uzunguni, nikafika kwenye gari nikamkuta kisoda pale yupo na yule dereva mwimgine aliyeniita pale tabata ,

Kisoda akasema ulipotelea wapi tena, nimekutafuta mule ndani mpaka nikachoka, nikajua labda umekuja kwenye gari nako haupo, nikamweleza masahibu yaliyonikuta, akasema wale wahuni tu walitaka kukuchomoa hela , ila kwa vile umefanikiwa basi fresh, kesho tuta vuka,

Nikakuta kanunua mazaga zaga ya kupika huko njiani, unga, mchele, dagaa, samaki, nyanya, vitunguu yaani vitu chungu nzima , nikasema kweli hii safari,

Kesho yake tukapanda tena daladala tukaenda kule, akaenda kwenye ofisi za agent wao akachukua documents, tukaenda kugonga passport, tukarudi uzunguni chuma zikawashwa tukaondoka, tukafanikiwa kuvuka boda, chuma zikaamsha, sema tulipoingia zambia hapo mwanzoni barabara ni mbaya kishenzi, nikasema sasa kwa mwendo huu tutafika kweli!!

Tukafika mbelembele tukaacha barabara ya mpika, tukakata kulia tukakamata barabara ya mbala, kumbe ile barabara mbaya ni pale mwanzo tu, basi chuma zikakamata road, zinaambaa hizo, yule dereva mwingine jina lake Anko yupo hapo nyuma na gari yake anafata moto,

Tulitembea , tulitembea sana, tukafika mahali vyuma vikapaki, tukashusha jiko la gesi tukaangusha ugali na samaki, tukala tukamaliza, nikaosha vyombo pale vyuma vikaamka tena,

Tukafika sehemu panaitwat Kasama, wakasema tuvungeni pale kesho tutaendelea, basi tukavunga pale , jioni tukaangusha tena ugali, tukalala pale,

Saa kumi alfajiri ngoma zikaamka, maeneo nnayo yakumbuka tulipita ni mansa, kawambwa hayo ni baadhi nayakumbuka, ila kuna down za hatari sana huko, tulifika sehemu kuna down paka unaona kama gari inaangukia mbele vile, we fikiri unakuta down inakona alafu ina daraja, kibao chenyewe kimechorwa fuvu alafu speed umeandikiwa 10km/h ndo ujue ni hatari,

Basi bana tulitembea mpaka tukafika sehemu panaitwa Nchelenge, hapo nchelenge ndo kama mji wa mwisho kabla hujakuta boda ya kuingia kongo, Pale kuna yard kubwa magari yanayoenda kongo yanapaki pale,

Hapo nchelenge kuna ziwa kubwa sana, wakazi wa pale ni wavuvi, pale tulikula samaki balaa, yaani samaki wa kwacha 20 sawa nae elf 2 ya huku unapewa samaki sufuria limejaa,

Pale ndo kuna ofisi za migration kwaiyo processes zote za kuvuka boda zinafanyikia pale, huko boda kuna ofisi ndogo tu ambazo ni za kupokea documents tu, Pale nchelenge tulifika ijumaa jioni, ofisi zimeshafungwa, kwaiyo inabidi tukae pale mpka jumatatu ndo tuanze process,

Basi tukalala pale, sasa bana kesho yake paka kucha, tukatoka tukawa tunatembea tembea huko mtaani kuangalia maisha ya wenzetu, kule hawaongei kiswahili kabisa, ni kilugha chao na kingereza tu,

Sasa bana kumbe Anko ni mtu wa mademu sana, katika pitapita zake huko akafumania demu wa kizambia sisi hata hatujui, basi jioni tukapika wali wetu na samaki tukala, tukamwachia anko maana toka tumeondoka ule muda hajarudi,

Kwenye mida ya saa mbili hivi tukiwa tunajiandaa kulala mara mlango unagongwa, kufungua ni mlimzi, akaongea kwa kingereza chake hakieleweki vizuri, ila alituambia twendeni mwenzenu kazua ugomvi huko,

Tukatoka mi na kisoda na yule mlinzi haoo mpaka kwenye gest moja hivi, Kumbe bana Mchana Anko alikuwa na demu mmoja wa kizambia, wakala maisha fresh, sasa jioni Anko kafumania mademu wa kikongo wawili, akaenda nao pale gesti kuwaburuza wote wawili, sasa kumbe yule demu wa kizambia kapata habari, akaenda mpaka pale gest, akagonga kile chumba cha kina Anko,

Walipofungua akazama ndani akaanzisha timbwili kwamba wale mademu wamemuibia mme wake, hapa na pale wale mademu wakampa kichapo yule demu wa kizambia, akaondoka akaenda kuwaita majamaa ya kizambia yakaja pale kwaiyo ikawa fujo,

Ndo yule mlinzi akaja kutushtua tukamwokoe mwenzetu, basi bana tukafika pale tukakuta varangati la kufa mtu, wale jamaa wanataka kuondoka na Anko, tulipofika pale tukawaamshia, tukawaamshia, tukamchukua Anko tukasepa, jamaa wenyewe walevi walevi tu hata hutumii nguvu,

Tukarudi kwenye magari tukaanza kupiga stori, kumbe wale jamaa wameenda kujikusanya limekuwa kundi kubwa wamekuja pale yard wanataka wafunguliwe waingie lasivyo wanavunja geti, wapo na mawe, mapanga, mafimbo, basi ikawa fujo pale, kesi ikawa kwamba Wakongo wameshirikiana na Watanzania kuwapiga wazambia, fujo zilipozidi wale walinzi ikabidi wapige simu polisi, Polisi wakaja pale wakapewa maelezo na wananchi na wale walinzi, wakaja kwenye magari wakatuchukua,

Itaendel
Kadri navoendelea kuishi, naendelea kugundua kwamba wanawake ni chanzo cha matatizo mengi sana kwa sisi wanaume mfano

1.kule moshi ulienda jela kisa mwanamke alietoa ushahidi asiokuwa na uhakika nao

2.Anko nae hapo kaingia kwny ugomvi kisa mwanamke,,sasa ugomvi umekuzwa mpaka umekuwa wa kitaifa (waTZ vs wamalawi)

3.kuna story ya mpwayungu village ye alifukuzwa geto usiku kisa demu

4.huyo huyo mpwayungu akaenda huko mkoani akafukuzwa kijijin kwa sababu alitaka mbususu ya kabint ka mwalimu

Asee naomba huduma ya RISUG ifike bongo fasta mana hawa wanawake watamaliza sana watu
 
kashawatia mkosi wenzake safari mimekuwa ngumu
Asa apo kamtia mkosi nani? Kwan anko si alienda mwnyw kutafta mbususu? Mbna unalazmisha jamaa aonekane kama yy ndo tatzo? Yeye anahusikaje apo?
 
I am soo happy for u my brother. Jamani Sity[emoji24][emoji24][emoji24] roho imeniumaaaa dah

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
Script ilivo ilikua lazima Sity atoweke kwenye maisha ya jamaa kwa namna moja au nyingine. what if Sity angekua hai. Happy ingekuwaje na tayari alikua kesha muahidi kumuoa na pia alishamzalia.
 
Akili sina akushike mkono na yeye kama wewe tu anakula dagaa wa Nyasa huko malizia story mwisho kabisa
[emoji23][emoji23][emoji23] ila kama jamaa ameweza kupata access ya kusimuliwa story kama hii na Engineer means asingekuwa anakula dagaa nyasa saivi.
 
Hatumkufuru Mwenyezi Mungu kwa uumbaji ila kusema ukweli wanaume wenye makalio makubwa wana shida sana, kila saa akili zao zipo matakoni,

Imagine mwanaume anasimulia msoto wa maisha yake na kutoa funzo kwa wengine lakini kuna jitu limeng'ang'ana na vitu vya ajabu ajabu tu, mara sijui nn

kufikia 2030, wanaume tutakua tumebaki wachache sana, wengi watakua wenye uume tu,
Kuna watu wa ajabu sana. Afu huyo anayejifanya kuhoji ndo unamkuta yupo kwny huu uzi saa24. Si aende kwny nyuz zngne huko ambako anaona ni za kweli? Qmmk zao
 
SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI

Ilipoishia,,,,,,,,,,,,,

Tukarudi kwenye magari tukaanza kupiga stori, kumbe wale jamaa wameenda kujikusanya limekuwa kundi kubwa wamekuja pale yard wanataka wafunguliwe waingie lasivyo wanavunja geti, wapo na mawe, mapanga, mafimbo, basi ikawa fujo pale, kesi ikawa kwamba Wakongo wameshirikiana na Watanzania kuwapiga wazambia, fujo zilipozidi wale walinzi ikabidi wapige simu polisi, Polisi wakaja pale wakapewa maelezo na wananchi na wale walinzi, wakaja kwenye magari wakatuchukua,

Endelea,,,,,,,,,,,,,,

Tukapelekwa Kituo cha polisi Nchelenge, Tukatoa maelezo pale, kweli ikaonekana tumewashambulia wazambia, halafu sisi ni wageni, polisi wakatutisha pale kuwa hii kesi ni kubwa na kama itaenda mahakamani lazima tufungwe, kwaiyo tuangalie mifuko yetu hii mambo iishie pale,

Wao wakawa wanataka kila mtu atoe kwacha elf moja sawa laki moja ya kibongo, Kisoda akasema hiyo hela sisi hatuna, sisi tutatoa kwacha hamsini hamsini kama haifai bora twende huko mahakamani,

Wakajitafakari pale ,wakasema leteni hiyo hela, kweli Kisoda na Anko wakatoa hiyo hela , Wale polisi wakatupa escort mpaka kwenye magari yetu tukarudi tukalala,

Kesho yake jumapili tukafua fua pale, na mimi nikafua maana nguo zangu ni zile alizonipa Kisoda na zile nlizokuwa nimevaa mwanzo,

Jumatatu asubuhi tukaenda kwenye zile ofisi za migration na ZRA, tukafanya process pale tukamaliza, tukarudi kwenye magari, wenyeji wa pale wakatuambia kutoka pale mpaka ufike Pweto boda ni kama km 100 hivi ila barabara ni mbovu kichizi, yaan ukitoka hapo asubuhi unafika boda jioni,kwaiyo tukaona kwa huo muda tutachelewa bora tulale tuanze safari asubuhi, Siku hiyo tukalala,

Asubuhi tukaamka tukajaza maji kwenye madumu maana huko tuliambiwa maji ni shida, kumbe yale mafuta yanaenda mgodini huko kongo kijiji kimoja kinaitwa kapulo, Tukalipia parking pale tukaondoka, tukafika sehemu lami ikaisha ikaanza barabara ya vumbi, yaani huko magari kupita ni nadra sana, hadi watu wanashangaa magari yakipita, barabara yenyewe kama za mtaani jinsi ilivyo mbovu, basi ikawa ni mdogo mdogo, gari unaibembeleza kuingia kwenye korongo usije ukapasua busta,

Tukawa tunaambaa ambaa na mwambao wa lile ziwa, tukafika sehemu mvua acha ianze kupiga, ikapiga mvua balaa, barabara haipitiki, tukatafuta sehemu tupaki magari mpaka mvua ikate, kabla hatujapata gari ya anko ikateleza ikaingia mtaroni, piga resi pale kuitoa haitoki, hiki kisanga kingine tena, mvua ndo imechanganya kichizi, tukasimama tukazima gari katikati ya barabara maana tungesema tupaki pembeni na sisi tungeingia mtaroni, tukatulia kwenye gari mpaka mvua ikate, ikanyesha wee mpaka ikaamua kukata, sasa mtihani ni kuitoa ile gari ya Anko, hatuna rope wire hatuna nini!,

Tukenda kwa wanakijiji kuazima jembe na beleshi tukaja kuchimba, jaribu kuitoa lakini wapi, zama huko chini chimba weee, tukajaza majani lakini ngoma haitoki,hapo tumechafuka matope balaa, tukapambana pale mpaka jioni ilkaingia lakini wapi, ajabu ile njia magari hamna kabisa, yaani tumepaki katikati ya barabara lakini hakuna hata gari moja iliyofika pale,

Basi tukawa hatuna jinsi, ni kulala tu mpaka kesho , tukaomba kuni kavu pale kijijini tukawasha moto tukatafuta vijana wawili wa pale kijijini tukasaidiana kulinda magari,

Tukakaa pale mpaka kukakucha, tukaendelea na mchakato wa kutoa gari, uzuri kulikuwa kumenyauka kwaiyo tukachukua belt, tukaikunja, kisoda akarudisha gari yake nyuma, tukaifunga ile gari ikavutwa ikatoka, ikabidi twende ziwani kuoga maana tulikuwa tumechafuka sana, tuliporudi safari ikaendelea,

Tulifanikiwa kufika pale boda ya Pweto kwenye saa nne hivi, tukapeleka documents pale tukaruhisiwa kuvuka, tukatembea kama kilomita mbili hivi tukakuta migration ya upande wa kongo, kuna kulipia pale na process nyingine, nao wakaturuhusu kuendelea na safari,

Barabara ya huku kidogo ilikuwa na afadhali maana ilikuwa na moramu, ngoma zikatembea, kuonesha kule ni nadra magari kupita basi watoto wanatoka kwenye vinyumba vyao wanakuja kushangaa magari yakipita,

Hatimae tukafika pale kapulo kwenye ule mgodi, tukaingia huko ndani tukaoneshwa sehemu ya kuegesha magari, tukapaki, kwa vile ilikuwa jioni tayari ikabidi tufanye mpango wa msosi pale, tukala tukaoga usiku ukaingia tukalala,

Kesho yake tukashusha mafuta, tukapewa documents safari ya kurudi ikaanza, Kweli tulirudi salama mpaka dar hakukuwa na shida yoyote,

Chuma ikaenda service, mi nikatumia muda huo kwenda msewe kwa Da J ila sikufanikiwa kumkuta, nilikuta milango imefungwa nyumba nzima haina mtu,

Basi safari nyingine tukaenda tena kongo lakini sasa hivi tukaenda Lubumbashi, tulipitia mpika, serenje, kapiri, ndola, tukaingia kasumbalesa, tukaingia 114( kasumbalesa upande wa zambia), siku hiyo hiyo tukafanikiwa kuingia 200( kasumbalesa upande wa kongo) tukalala pale,

Kesho yake tukatimba mpaka lubumbashi kampuni moja inaitwa Kongo petrol ndo tukaenda kushusha mafuta hapo, Basi wakati wa kurudi upande wa zambia magari ni machache hivyo kisoda akawa ananifundisha kugonga gear, yale madude ni matamu asikwambie mtu,

Basi tukaenda safari kadhaa, Lusaka, ndola, lubumbashi ndo zilikuwa safari ndefu, Nilipata hela nikanunua smart phone kongo maana ni bei poa sana, Niliingia facebook nikamtafuta Sity, nikamtumia messej lakini hakunijibu,

Basi nikaingia kwenye email yangu, kwenye zile post za kazi nilikuwa natumaga, nikadownload vyeti vyangu, nika apdate cv yangu, nikaanza kutuma maombi ya kazi mitandaoni,

Nikawa nikipata nafasi naenda kwa Da J ila nakuta hayupo, nilipoulizia pale nikaambiwa alishahama, nikasema poa,

Siku moja tumetoka kongo, nipo geto ( maana ilibidi nikae geto kwa kisoda), mara simu ikaita namba ngeni, kupokea akaongea sauti serious kidogo, " Naongea na Akili sina", nikajibu ndio, " Ulituma maombi kampuni deshi deshi nafasi ya desh desh Manager ? " nikajibu ndio, " Jumatatu unahitajika kwenye interview kwenye ofisi zetu zilizopo posta",

Mzee simu ilipokata sikuamini eti, nikajiuliza naota nini!!, Kisoda akaja nikamsimulia, akaniambia sasa hayo mambo utayaweza kweli mambo ya kisomi hayo!, Nikamwambia mi sindo mambo yangu haya nimesomea, akaniuliza umesomea wapi, kumbe nilikuwa nimeshasahau kuwa nilimdanganya kwamba sikuendelea na chuo bali nianza biashara ndogo ndogo, basi pale ikabidi nimchane live, nikamwambia nilijiskia aibu tu kukwambia kuwa nilisoma chuo kwa ile hali niliyokuwa nayo,

Basi Kisoda akanisaport pale, nikaenda kutafuta nguo za interview na viatu, maana nguo zangu nyingi yalikuwa majinsi, Nikawa najiuliza sijawahi kufanya interview toka nimezaliwa, hii itakuwaje? Nikawa naingia google nacheki maswali yanayoendana na ile position na majibu yake,

Kweli siku yae siku nikatimba kwenye interview, nilijua nitakuwa peke yangu ila nikakuta tupo kama saba hivi, tukaanza kuitwa mmoja mmoja, ilipofika zamu yangu nikazama, nikakuta panel ina watu watano, wabongo watatu wazungu wawili,

Wakajitambulisha pale, wakaanza maswali yao, mwanzoni niliingiwa upepo ila kadiri muda ulivyozidi kwenda nikazoea yale mazingira, wakaniuliza maswali mengi sana ila nikayajibu yote, wakataka waone vyeti vyangu orijino, hapo ndo ikawa kimbembe, ikabidi nidanganye kuwa viliungulia ndani ila kwa sasa nipo kwenye process ya kupata vingine,

Interview ikaisha, nasubiri majibu sasa, lakini kila nikipima sioni nafasi yangu kuchaguliwa, maana nilikuta wana pale wamekuja na magari, mtu kapiga suti yupo smart sembuse mimi hata vyeti sina,

Siku zikaenda tukaendelea na mishe zetu, siku tupo njiani tunaenda zetu ndola, tukiwa mafinga pale tunapiga msosi mara simu ikaita, nikapokea , nikasikia " Ndugu akili sina" nikajibu naam, " Unaongea na flani flani kutoka kampuni flani flani, napenda kukupongeza kwa kupita kwenye interview , nikutaarifu kuwa kesho saa mbili asubuhi unatakiwa uwepo hapa kwa ajili ya mambo mengine" simu ilipokata nikajisachi kwanza, hivi ni kweli au naota,

Kisoda akauliza ni nini nikamwelezea pale, Akaniambia ndo ushakula shavu ivyoo mzee, nikawa siamini, sasa itabidi mi safari yangu iishie pale, ikabidi tufanye mchakato wa usafiri muda uleule nigeuze dar, kweli nikapata, kisoda akanipa kama elf 70 hivi akasema hizi zitakusukuma, nikachukua na ufunguo wa geto nikawaaga pale nikadandia gari kurudi dar, kwenye saa tano hivi usiku nipo dar tayari, nikafika geto nikaoga nikalala,

Kesho asubuhi nikatimba pale kampuni, nikapokelewa, nikapelekwa kwa director, nikakuta ndo yule mzungu, tukaongea pale, nikapewa mkataba niusome, ila wakasema huu mkataba hutasaini kwa sasa, kwa sasa utafanya kama intern kwanza kwa miez sita, wakiridhika na performance ndo nitasaini mkataba wa kudumu, na kipindi cha intern ntalipwa mshahara nusu, akaniuliza kama nipo tayari , nikamwambia yes sir!!

Basi nikapelekwa kwa hr ni mmoja kati ya wale wabongo wa siku ya interview, kuna documents za kujaza jaza na nyingine natakiwa kuleta,

Kazi ikaanza hvyo, nikapewa ofisi yangu pale iko poa, nikaambiwa nitafute leseni kuna gari la kampuni nitapewa, basi mambo yakawa byee,

Mwisho wa mwezi zikaingia M kadhaa kwenye account, nikasema huu ndo nusu mshahara au wamekosea?

Basi ikabidi niame pale kwa Kisoda nikatafuta nyumba kubwa inayoendana na meneja,

Nikaanza kumtafuta Sity, nikaenda kwa Ant yake mmoja madale alinipelekaga Sity, nikafika Anti akanipokea fresh, ila alichoniambia kilifanya nilie kama mtoto,

Akaniambia Sity alifariki, alipata ajali morogoro wakati anaenda kwao bunda, nililia sana, nikamwomba shangazi siku moja anipeleke huko bunda nikalione tu kaburi la Sity,

Siku kweli tukapanga tukaenda, tukafika mpaka kwao, tukamkuta mama yake Sity, ajabu akawa kama ananifahamu vile, aliponiona akaanza kulia, tukajikuta wote tunalia sasa, kumbe kwenye album ya picha za sity kuna picha tulipiga nae zipo kule ndo maana yule mama akawa ananijua,

Tukaenda kwenye kaburi la Sity ,nililia sana pale juu ya kaburi, nililia paka makamasi yakanitoka, nikawa kama nimefufua msiba upya, wote wanalia,

Tukatoka pale, tukaenda ndani, nikawapa pole sana, nikawasimulia jinsi Sity alivyokuwa msaada kwangu, nikamkuta mdogo wake pale wa kiume, ndo kamaliza four ila kafeli yupo nyumbani, Nikamwahidi mama nitamsomesha yule dogo mpaka chuo kikuu, pia nikamwambia nitamjengea nyumba pale pembeni yote ni kujaribu kulipa kwa sehemu tu fadhila zote alizonifanyia Sity, nikaondoka nikarud zangu town,

Kule kijijini kwetu nilitimba siku moja, hawakuamini, wakashangaa sana, wakasema walijua nimeshakufa zamani, mzee na mama walifurahi sana, nikakuta dogo ana watoto watatu sasa,

Nikakutana na Hapy, hakuamini kuniona, kwanza akajua nimeshaoa na sina hata time nae, nikamwambia nitamwoa nani na wewe ndo mke wangu umesahau nilikwambia,

hakuamini eti, nikakuta joyce kawa mkubwa nae shule ameshaanza , nikamwambia happy ajiandae nimekuja kumchukua, hakuamini mzee, pale home walifanya sherehe siku ile, nikalala siku moja, kesho yake nikawaaga maana mjini nipo kwenye kazi za watu,

Kesho yake nikamchukua Happy na Joyce tukaja zetu Dar kuanza maisha mapya,
Da J nilimtafuta mpaka leo sijamuona,

Mdogo wake Sity akarudi shule namsomesha na anaendelea vizuri, pia nyumba nimeshaanza kuijenga saiv ndo ipo kwenye lenta,

Na pale kwetu pia nimeshaanza msingi nataka niangushe mjengo pale,

Mshikaji wangu kisoda sijamuacha, mara nyingi naenda pale na nna mpa saport na yeye maana ana nyumba yake kigamboni anajenga kwaiyo nampa saport mara kwa mara,

Saiv nipo na happy mke wangu na tuna mtoto mwingine Anaitwa Angel maisha ni mazuri asee nakula hela ndefu kiasi, nna usafiri fresh yani,

Kwa wale tunaosota kitaa sababu ya ajira, niwatie moyo tu mlango wako upo, siku moja utafunguka, ila tu Sikushauri kujilipua na kwenda sehemu hukujui, huna ndugu, huna hela eti unaenda kutafuta maisha, siku shauri,

MWISHO

Na mimi Akili Sina nichukue nafasi hii kuwashukuru wote tuliokuwa pamoja kuanzia mwanzo hadi mwisho kwenye stori ya ndugu yetu huyu, Niwajuze tu huu mkasa haujanikuta mimi, nilihadithiwa tu na mtu na mimi nikaona niwasimulieni nyie, Karibuni Mbinga huku tule dagaa nyasa,

HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA, HAIRUHUSIWI KUKOPI WALA KU EDIT BILA IDHINI
Dah Asante kwa simulizi hii nzuri

Ukipata nyingine Leta vitu mkuu
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]hembu kwanza ncheke mie[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]ati mhusika wa stori sio ww?
 
Akili sina leta nyingine sasa ulio hadithiwa na mwingine,
Watu mshanogewa asali naona unamtuma jamaa akatuletee mzinga mwingne ili tuendelee kulamba asali[emoji28][emoji28]uyu jamaa ana kipaji cha uandishi knoma
 
Back
Top Bottom