Usilolijua ni hili, zaidi ya askari 100 wametumika kumlinda Boniface Jacob Mahakamani

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Taarifa ikufikie Popote ulipo kwamba pamoja na Boniface Jacob kuachiwa kwa Dhamama kulikuwa na Jambo la kustaajabisha kidogo lililojitokeza Kwenye Mahakama ya Kisutu.

Sisi wengine kwenye mambo Makubwa huwa pia tunaangalia mambo madogo madogo, Jicho letu limeangazia idadi ya Askari waliomiminwa Mahakamani ili kuhakikisha Bonny Dongo hafurukuti, Idadi hii inatajwa kuzidi hata ile ya Askari waliomkamata Osama Bin Laden kwenye mapango.


Hesabu ya Haraka inaonyesha kwamba kwenye kizimba cha Mahakama alipokuwa Bonny alizungukwa na Askari wenye sare zaidi ya 25, Juu ya Paa kulikuwa na Askari zaidi ya 20, kwenye Geti la kuingilia kulikuwa na zaidi ya Askari 18, Huku ndani ya Mahakama wakijazwa zaidi ya Askari 50 waliovaa Kiraia.


Hoja yetu ni hii, Sababu ya Kumpaisha huyu jamaa kiasi hiki ni nini hasa, Ana Ugaidi upi wa kuitisha Mamlaka kiasi cha kukodi hata Askari wa akiba wa Mikoa ya Jirani?

Angalizo letu ni hili hapa.

 
Ni jambazi au asitoroke.
 
Mungu muache aitwe Mungu,kuna muda anaruhusu mambo yafanyike!,Wakadhani wanammbomoa ndio wanampa kujulikana zaidi!
 
Nasikia siku ya kumkamata pale sinza ulipigwa mkono kama van dame,polisi wawili walivunjika taya mwingine nyonga haifanyi kazi yuko moi,ndio maana dhamana ilichelewa wakihofia yule wa moi asije kufa
 
Wana mbwembwe tu.Wakiagizwa majukumu ya akili nyingi wanatepeta kama chai kwa juisi ya bamia. Hopelesses!
 
Nasikia siku ya kumkamata pale sinza ulipigwa mkono kama van dame,polisi wawili walivunjika taya mwingine nyonga haifanyi kazi yuko moi,ndio maana dhamana ilichelewa wakihofia yule wa moi asije kufa
Ni kweli, ila yule wa Taya kawekewa waya, yule wa Nyonga kachomekwa Chuma, wote wako hai na Wameruhusiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…