Usimamizi wa mirathi

Sio kweli
 
Mnakaa kikao wana familia mnamchagua msimamizi wa mirathi.

It's a process kiasi utataka hata kuwa na mwanasheria
 
Vikiwepo hivyo naanzia wapi
Unatakiwa kuwa na;
1. Kibali cha mazishi
2. Muhutasari wa familia.Minute iwe na uteuzi waa msimamizi wa mirathi, orodha ya mali za marehemu na majina ya wategemezi wa marehemu. Usiandike mgao wa mali humo. Muhutasari uwe na muhuri wa mtendaji wa kijiji/mtaa
3. Kama msimamizi ni mwanandoa uwe na cheti cha ndoa. Kama mtoto uwe na cheti cha kuzaliwa.
4. Uwe na details za marehemu na msimamizi
Vyote hivyo unapeleka RITA. Utajaza kwenye mfumo taarifa zote za marehemu pamoja na msimamizi hapo RITA. Utalipia elfu 7. Ndani ya mwezi watakupa cheti cha kifo (death certificate).

Baada ya hapo peleka mahakama ya mwanzo hicho cheti cha kifo, cheti cha ndoa, kibali cha mazishi na muhutasari wa familia. Usiende mahakamani bila barua ya utambulisho wa wewe na wadhamini wawili kutoka kwa mtendaji. Pale mahakamani kuna form utajaza na kuonana na hakimu pamoja na wadhamini wako.

Atakupa tangazo la wito wa kusomwa shauri la mirathi ukapandike eneo la makazi ya marehemu. Kwenye hiyo tarehe mtahudhuria wewe na ndugu hasa wanufaika wa mirathi. Kama hakuna gogoro msimamizi atagawa mali na kutoa taarifa mahakamani
 
Yeah uko sahihi Kaka, na kingine Kama hakuna vitu vingi wanaweza maliza kwa utaratibu nzuri Kama waki elewana.
 
Yeah uko sahihi Kaka, na kingine Kama hakuna vitu vingi wanaweza maliza kwa utaratibu nzuri Kama waki elewana.
Yeah, kama hana mali zitakazohitaji documents za mahakama. Mfano pensheni, viwanja vyenye hati, fedha benk, TRA kubadili kadi nk. Tofauti na hapo hataweza kupata. Ukienda ardhi kubadili hati, NSSF, benk watakwambia lete docs za mahakama.
 
Yeah, kama hana mali zitakazohitaji documents za mahakama. Mfano pensheni, viwanja vyenye hati, fedha benk nk. Tofauti na hapo hataweza kupata. Ukienda ardhi kubadili hati, NSSF, benk watakwambia lete docs za mahakama.
Yap, Sema mahakamani Wana mizunguko, mfano awe na pension, dah inaeza chukua hata miezi 6
 
Mkuu unaweza kushare link
Mkuu, mzigo huu hapa
 
Kazanazo Uzi huu wenye majibu ya kina.
 
Mnakaa kikao wana familia mnamchagua msimamizi wa mirathi.

It's a process kiasi utataka hata kuwa na mwanasheria
Kikao tushakaa na tushachagua msimamizi, sio kuwa tunataka kuuza hapana ila tunataka kutambulika kisheria
 
Ahsante sana mkuu

Hiki kibali cha mazishi kinapatikana wapi maana marehemu kafa kitambo kidogo

Then hatutaki kuuza tunataka kutambulika kisheria kwa ajili ya kuwekeza
 
Samahan mkuu utaratibu mzuri kivipi tunaelewana tu ni kuwa tunataka kutambulika kisheria ila hatuuzi urithi
Mkuu kama kuna kiwanja tu, hapo mna eza kubaliana kwa maandishi kuwa mmiliki ni Huyu na huyu.

Maana Kuna mirathi ya kisheria na Ile ya zamani..

Kama Kuna pension, nyumba, mna fata utaratibu tu
 
Nenda mahakamani ya mwanzo , ukifika pale wapo wale waheshimiwa yaani wapo tu, mwombe mmoja pembeni uongee naye akushauri, hope utamwachia ya ku brash viatu
 
Ahsante mkuu nimepata kuelewa baadhi ya maswali niliokuwa nayo
 
Mkuu kama kuna kiwanja tu, hapo mna eza kubaliana kwa maandishi kuwa mmiliki ni Huyu na huyu.

Maana Kuna mirathi ya kisheria na Ile ya zamani..

Kama Kuna pension, nyumba, mna fata utaratibu tu
Ni kweli mzee haukuacha vitu vingi sana ni just mashamba na nyumba

Tunahitaji kutambulika kisheria kwakuwa tunataka kuwa na mfuko(bank) ya familia kwa ajili ya kuhifadhi rasilimali pesa za familia sasa kule hawatoi account mpaka msajiliwe na kusajiliwa ni mpaka muwe na msimamizi wa mirathi

NB: hatutaki kuuza wala kugawana tunataka kutambulika kisheria ili tuweze na kukopa fedha bank n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…