Unatakiwa kuwa na;
1. Kibali cha mazishi
2. Muhutasari wa familia.Minute iwe na uteuzi waa msimamizi wa mirathi, orodha ya mali za marehemu na majina ya wategemezi wa marehemu. Usiandike mgao wa mali humo. Muhutasari uwe na muhuri wa mtendaji wa kijiji/mtaa
3. Kama msimamizi ni mwanandoa uwe na cheti cha ndoa. Kama mtoto uwe na cheti cha kuzaliwa.
4. Uwe na details za marehemu na msimamizi
Vyote hivyo unapeleka RITA. Utajaza kwenye mfumo taarifa zote za marehemu pamoja na msimamizi hapo RITA. Utalipia elfu 7. Ndani ya mwezi watakupa cheti cha kifo (death certificate).
Baada ya hapo peleka mahakama ya mwanzo hicho cheti cha kifo, cheti cha ndoa, kibali cha mazishi na muhutasari wa familia. Usiende mahakamani bila barua ya utambulisho wa wewe na wadhamini wawili kutoka kwa mtendaji. Pale mahakamani kuna form utajaza na kuonana na hakimu pamoja na wadhamini wako.
Atakupa tangazo la wito wa kusomwa shauri la mirathi ukapandike eneo la makazi ya marehemu. Kwenye hiyo tarehe mtahudhuria wewe na ndugu hasa wanufaika wa mirathi. Kama hakuna gogoro msimamizi atagawa mali na kutoa taarifa mahakamani