Habari wanajamii, natumai mko njema.
Naomba kujuzwa hatua za kufuata ili kufungua file la usimamizi wa mirathi. Kwa maana vitu gani vinahitajika ili kuweza kuwa msimamizi na wapi anatakiwa kwenda alieteuliwa kuwa msimamizi ili kutambulika kisheria.
Natanguliza shukrani
Taratibu za Mirathi kwa ujumla zina anza na KIKAO CHA UKOO
Kikao cha ukoo kinahusisha mke/mume wa marehemu, watoto, wazazi wa marehemu na ndugu wa karibu wa marehemu na watu wengine muhimu wanye kujua kuhusu maremu nk
Ili kikao kiwe rasmi kitakua na mwenyekiti na katibu ambaye atahakikisha maamuzi ya kikao yanaandikwa kwenye MUKTASARI WA KIKAO CHA UKOO na wajumbe wote wa kikao watasaini kukubali maamuzi ya kikao
Mambo MUHIMU kimahakama yanayotakiwa kuwepo kwenye Muktasari wa Kikao cha Ukoo ni
FAMILIA YA MAREHEMU
kikao kitawatambua mke/mume na watoto wote wa marehemu.. hawa ndio beneficiaries
MALI ZA MAREHEMU
kikao kitazitambua na kuziorozesha mali zote za marehemu
MSIMAMIZI WA MIRATHI
Kikao kita mteua msimamizi wa mirathi ya marehemu
Baada ya hapo aliyeteuliwa kuwa maimamizi wa Mirathi atakwenda mahakani sasa kufungua shauri la mirathi ili sasa mahakama imteue rasmi kuwa msimamizi(Taratibu zaidi atapewa mahakamani, ila ni lazima awe na muktasari wa ukoo na cheti cha kifo)
Ikumbukwe kwamba kikao cha ukoo kina mpendekeza msimamizi kisha mahakama ina INAMTEUA RASMI kuwa msimamizi ikiwa hakuna pingamizi
Baada ya mahakama kusikiliza shauri na kumteua rasmi msimamizi atarudi kwa familia ya marehemu kusikiliza matakwa yao
Je wanataka kugawana?
Je hawagawani ila usimamizi utakuaje nk nk
Mchakato utakao kubaliwa na familia ya marehemu ndio msimamizi ATAUSIMAMI
So
Kuna mchakato wa kutuliwamsimamizi
Na kuna mchakato wa nini kifuate