Usimchukie sana adui yako na kuwa mpofu ya uangamizo wako!

Usimchukie sana adui yako na kuwa mpofu ya uangamizo wako!

Hypersonic WMD

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2024
Posts
1,337
Reaction score
1,876
Kama una chuki na adui yako jitahidi chuki isizidi. Pindi chuki ikizidi inakupofusha kutoona uangamizo wako.
Yann ya kumtilia adui yako sumu kwene kisima ambacho wewe mwenyewe ndo unatumia maji??

HISTORIA YA SOMALIA NA JINSI NCHI KUBWA ILIVO ANGUKA CHUKI.

Wasomali walijikuta wametawanyika katika nchi tofauti za kenya,Ethiopia na Djibout..kutokana na mkoloni kugawa mipaka bila kuzingatia makabila .

Ni kama makabila kama ya wameru, masai,wakurya,Wajaruo walivo wengine wako kenya wengine tz.

Au wamakonde kat ya Tz na mozambique.Au Watuareg walivogawanyika Kati ya Niger,Mali,bukinafaso nk.

Hii ipogo dunia nzima.
Ukija mashariki ya kati kuna Wakurd ambao wamegawanyika wengine wako iran,iraq,Syria na Uturuki.

So madhara ya ukoloni ni haya.

Sasa wasomali kutokana na ukabila wa hali ya juu hawakuwai kukubaliana na hiki kitu.
Somalia baada ya uhuru ilikua taifa kubwa sana na nguvu kijeshi hii ilijumlisha somaliland ambayo ilitawaliwa na muingereza,na somalia iliyotawaliwa na muitaliano. Hawa wote waliungana baada ya uhuru kuwa nchi moja.

Wakiongozw na Kiongozi wa kisomali Saidi bare ambaye kiasilia alitokea Ogaden ambayo ilikua sehemu ya Ethiopia.

Watu watajiuliza ilikuaje Ogaden ikawa Ethiopia na ina wasomali.
Kiongozi wa Kipindi hicho kabla ya Haile aliweza kuwashinda wakoloni na kuwapiga na kisha kujipimia maeneo na kajimegea na hili eneo la ogaden.Ikumbukwe sehemu nyingine ya somalia ilikua chini ya mkoloni hivo wasomali walikua hawana nguvu wala maamuzi maana wao walimilikiwa na kama bidhaa ya muitalia na muingereza.

Alichofanya kiongoz wa Ethiopia n kuweka mikataba na kutambua mipaka ya Ethiopia na kutambulisha nchi yake na mipaka yake na ikafahamika dunia nzima mipaka yake wakat wasomali wakiwa watumwa wa wazungu




ITAENDELEA
 

Attachments

  • FC330F5A-5879-4883-A127-7C482F22A51B.jpeg
    FC330F5A-5879-4883-A127-7C482F22A51B.jpeg
    47.1 KB · Views: 5
  • BC5F3286-95CD-474E-852E-F5042D1132EF.jpeg
    BC5F3286-95CD-474E-852E-F5042D1132EF.jpeg
    1.1 MB · Views: 3
BAADA YA KUPATA UHURU

Baada ya somalia zote mbili kupata uhuru Somalia ilikuja kutwaliwa na saidi bare kwa njia ya mapinduzi na huyu jamaa anataka kutimiza kutu ambacho kitaenda kuitesa somali kwa zaidi ya miaka 40.

Kitu chenyewe ni Great Somalia.
Wasiofahamu Concept ya great Somalia ni wazo la kuunganisha maeneo yote yanayokaliwa na wasomali.

Yaan wamege eneo la Kenya , na Ethiopia kuyafanya sehemu ya somalia

Juhudi zikaanza wakati huo Somali ilikua inapata support kutoka nchi ya kisoviet na ilikua ndo nchi mshirika mkubwa wa sera za kisocialism na ilipata support kubwa kuliko nchi yote Kusini mwa jangwa la sahara.

Ethiopia yenyewe ilikua ina supportiwa na marekani.Katika mwendo huu rais wa Ethiopia anapinduliwa na mkuu wa majeshi aliyeitwa mariam meningstu na kusababisha tafran kubwa .
Wakat huo ilikua na mgogoro na watu wa Eritrea ambao pia walikua wanataka kujitenga, lakini pia uasi mkubwa dhidi ya serkali mpya iliyoingia kimababu wananchi wengi walikua hWakuabaliani nayo.

Ni katika kipindi hiki kigumu Marekan iliacha kuwasupport Waethiopia kulingana na mapinduzi haya na Kiongozi mpya alikua anakinzana na sera za marekani.

Hivo Ethiopia ilikua haina mshiriki na Somalia alikua mshirika wa kisovieth alipewa silaha,pesa na utaalam
Ni wakat huu ndipo Ethiopia nayo taratibu ikawa inajisogeza kwa nchi za kisoviet maana ilikua haina mshirika mwenye nguvu.

Nchi ya kisoviet ingawa ilikua na ushirika mkubwa na Somalia ila ilivutiwa na Ethiopia kutokana na ukubwa wa nchi, idadi ya watu na hamu ya kuweza kuidhibit bahar nyekundu kabla Eritrea haijajitenga Ethiopia ilikua na Beach za bahar na bandari.
 
SOMALIA KUVAMIA ETHIOPIA
Kwakua Saidi Bare alikua na uhakika wa support ya Sovieth bas alianza kuwashambulia wale aliowaona ni maadui zake Ethiopia kwa kutumia Waasi wa Ogarden.

Ili wapa mafunzo na silaha kuteka maeneo.
Takriban Mwezi mmoja Jeshi la somalia na waasi walichukua maeneo makubwa ya kimbo la Ogarden.

Kufikia hapa Ethiopia pamoja na machafuko yake ya ndani iliamua kukusanya jeshi lake maelf na maelf kwa ajili ya vita. Vita vilianza kuchapwa sana wakati huo Ethiopia ilikua haina support ya US (sababu ya mapinduzi).

Hivo soviet ilizisaidia Nchi zote lakini nchi za kisoviet hazikufurahishwa sana na jambo la somalia kuvamia Ethiopia nchi ambayo mipaka yake ilitambulika kimataifa.

Machoni mwa jumuiya ya kimataifa Somalia ilionekana mvamizi na Ethiopia ilionekana inapigana kujilinda.


Bila kusahau Cuba ilikua upande wa soviet kuzisaidia hizi nchi.Nchi hizi mbili ziliishauri somalia kusitisha vita lakini saidi bare hakukubali.

Saidi bare na wanaharakat wengine wa somalia walikua wamezuzuka na tamaa ya kua na somalia kubwa yenye wasomali walioko kenya na ethiopia bila kujali kua vita hiyo ingewaingiz kwene anguko litalodumu zaidi ya miaka 30.

Kwa kua Saidi bare aliyekua anatawala kiditeta alikataa ushauri wa wakuu na watoa msaada ambao waliona vita haikua na tija kwani ilikua NI KINYUME CHA SOCILISM NA MAXISIM THEORY AMBAYO NDIO ILIKUA NDIO NGUZO YA ujamaa.

Waliamni vita ya somalia dhidi ya Ethiopia ilikua tamaa ya kuunda taifa kubwa la kabila moja na siyo katika misingi ya ujamaa.
Kifupi hiki kitu kilikua hakiendani kabisa na sera ya ujamaa ambayo Soviet na cuba walizinguka duniani kote kusupport nchi zenye mlengo huu.
 
SOMALIA YABAKI PEKEE YAKE BILA SUPPORT
Sasa baada ya kushindwana na Wasoviet nao walikata msaada wa kifedha,silaha na kitechnically ambao walikua wakitoa kwa jeshi la somalia.
Kufikia hapa said bare aliamua kuwatimua warusi wote wa kisovieth na cuba.


Baada ya kutimuliwa wote walienda wakatia maguu Ethiopia ambaye alionekana mshiriki mtiiifu.

Kilichofuata ni vita vikaanza kuwazidia wasomali. Bila msaada wa kijeshi wa utaalam,vifaa na fedha vita ikawa si rafiki .Ingawa mwanzo jeshi la somalia lilikua limechukua maeneo makubwa ya orgaden sasa likaanza taratibu kupteza maeneo na kurudishwa nyuma taratibu.

kufikia mwaka 1978 march Jeshi la somalia likawa limetolewa kabisa eneo hilo la ethiopia na likawa limeshindwa
Inakadiliwa raia 25000 walipoteza maisha.
 
MAISHA YA WASOMALI BAADA YA VITA
Baada ya Vita maisha yaligeuka magumu sana kulingana na hasra ya vita. Serikali ilibidi iongeze kodi kukabiliana na mtikisiko wa uchumi.

Hilo taratibu likaanza kuleta matatizo kama vile chuki za wananchi dhidi ya serikali yao.
Ndoto za somalia kuu zikawa zimeyeyuka hivo aina mpaya ya utawala wa kikooo ukaanzaa kuibuka.
Waasi dhidi ya serikali ya Saidi bare wakaanza kuibuka wakipinga uongozi wake,Udikteta, rushwa,mifumo mibovu,na hali ngumu ya maisha. Waasi hawa walikua wanadhamiria kumtoa Saidi bare madarakani.

Hapa serikali ya Saidi Bare kila ilipojalibu kupambana ndipo iliibua waasi wengine .
Waswahili wanasema tumbo tupu halina adabu
 
Back
Top Bottom