Usimfanye mtoto wako kuwa mtoto wa kambo alelewe na baba au mama ambaye si wake. Atakosa amani, uhuru na furaha kwa miaka yake yote ya utoto

Kuna watu watakuja hapa kupinga ila ambao tuna uchungu wa kulelewa na baba na mama wa kambo tunajua machungu yake!! Inauma sana, inaumiza sana sana!!

Siku ikitokea bahati mbaya nikachana na mke wangu watoto wangu hawatapitia machungu niliyopitia, nitawalelea mwenyewe kwa mikono yangu, sitaoa tena, nitawapa furaha angalau nikiwaona wao wanafurahia machungu yangu ndo yanaisha!!

Narudia tena ambao hawajapita hawawezi kuelewa!!
 

Pole Sana Mkûu.
Siô kîla Mtu anaweza kuhisi Wengine wanavyohisi hasa Watu weñye Ubinafsi
 
Mkuu, bandiko lako limenigusa sana, kama hukupitia malezi ya aina hiyo basi upeo wako ni mkubwa!
Mimi nimelelewa na mama wa kambo tangu nilipokuwa mdogo sana, sasa mimi ni mtu mzima lakini bado kuna vitu sina uhuru wa kuvifanya pale nyumbani, naona kwa watu wengine wakiwakalipia, kuonya na kuwakosoa mama zao,lakini kwangu mimi siwezi kufanya hayo direct kwa mama wa kambo; kwa kufanya hivyo kunatafsiriwa kama 'jaribio la kutaka kumpiga au kumfanyia kitu kibaya!'

Ikiwa kuna jambo lolote la kumpinga mpaka nitafute 'namna' nzuri ya kufanya hivyo, vinginevyo inatafsiriwa kama nimemdharau kwa kuwa yeye sio mama mzazi!
Nikiwaadhibu wadogo zangu (watoto aliowazaa yeye sasa) hilo bifu asikwambie mtu! yaani yeye hawachukulii kama wadogo zangu, na kitendo cha kuwaadabisha anaona kama vile nafanya revenge! hahah

Ndg, usiombe mwanao ayapitie haya, ni mateso ya muda mrefu sana
 
super!
 

Mkuu Pole Sana
Watu lazima Kabla hawajafanya maamuzi yoyote Waangalie matokeo ya Muda mrefu zaidi kuliko kufikiri Kwa mihemko
 
Robert Mrungu na akujenjee..mwana una akili weee..nimejikuta tu naongea kipare..Mungu awabariki waliokuzaa..Umeongea vyema na ukweli mtupu..

Nahavame Mkûu, Mrungu mjenja atujenje vose. Uman'je tuendwa turonge vindu vyedi ambu hei isanga turavecha na mburi ja hii isanga jikonda ngoro jetu
 
Kwa baadhi ya jamii kule kanda ya ziwa Nyanza, mtoto ni mtoto as long as yupo chini ya dari lako nawe ndiye umemtolea mama yake mahari. So ni mwanao. Huwezi mbagua.

Hii concept ya mtoto wa kambo inachagizwa na ubinafsi wa uzungu tunaouiga.

Mimi nimeona washkaji wanakua na hawajui hata kama wao ni watoto wa kambo.
Hamna namna ya ku-notice.
Huu ni utamaduni mzuri.
 

Tulishakataa Ukabila
Kukataa Ukabila ni Uzungu. Tulikubaku Uzungu Kwa kukataa Ukabila, Mila na desturi zetu. Haya NI matokeo.
 
Umeandika mambo ya msingi sana. Tunapenda starehe, ila hatutaki kuwajibika kwa matokeo ya starehe zetu.

Na kuna wale waliotelekezwa kwa bibi na babu au ndugu🙆🙆
I second you Atoto sijui why nakufatilia yaan najikuta nikiona coment yako nakuwa delighted.
 
Ni mazuri ukihadithiwa ila tunaojua undani wake hatujui tuipindue vipi meza..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…