Gol D Roger
JF-Expert Member
- Sep 16, 2023
- 2,316
- 6,082
Habariš
Kwa miaka mingi nilikiwa nikisikia huu usemi, sasa nimeuamini.
Usimkopeshe ndugu yako, hata kama anakuja kwa kuburuza magoti na machozi yanamtiririka.
Usimkopeshe ndugu yako, kama una hela, msaidie, aende zake, mbaki na amani.
Narudia tena usimkopeshe ndugu yako, kama ana shida bac msaidie kwa moyo mmoja, usimkopeshe.
Ukimkopesha ndugu yako, utapoteza hela yako na ndugu yako utampoteza, mtakuwa maadui bila sababu yoyote ya msingi.
Urafiki na undugu wenu, ni jambo la maana sana kuzidi hela, kamwe usikubali hela ikufarakanishe na marafiki zako, kamwe usikubali hela ikugombanishe na ndugu zako.
Ndugu yako akiwa na shida, msaidie, usimkopeshe ili wewe ubaki na amani.
Mm mwenzenu yamenikuta ndo maana nimeamua kuandika haya maneno.
Mara ya kwanza nilisema bahati mbaya, mara ya pili nikasema tena bahati mbaya, mara ya tatu sasa ndo akili imenijia kwamba ndugu hakopeshwi, anasaidiwa.
Usiponielewa kuna siku utanielewa.