Usimseme mkeo au mumeo vibaya kwa watu.

Usimseme mkeo au mumeo vibaya kwa watu.

Au mmekosana then kilamtu anaanika madhaifu ya mwenzie....
Mnapatana,sisi waja tunakuwa tunawachora tu.Wekeni maji kwa kinywa,haipunguzi chochote
 
Usikae na mavitu moyoni ni heri useme usaidiwe mawazo..watu wanawasema mpk mama na watoto zao..sembuse binadamu mliyekutana ukubwan

NB:USISEME TU ZILE SIRI ZA KIBAILOJIA MFANO MAMBO YA MAPENZI AU KUNUKA UCHI ILA MENGINE MFANO KAMA ANA MATUMIZI MABAYA YA PESA AU ANAGAWA VITU OVYO UNAWEZA KUSEMA KWA MTU MZIMA AKAKUPA NJIA
KWENYE HII FAMILIA KUNA TATIZO MAHALI
 
Kuongea yanayokusibu inasaidia kutoa nyongo mwilini. Hata ukikaa kimya kama solutuon haipo ni haipo tu.
Nafikiri ni busara kama unaona mambo magumu ni bora kuachana tu kuliko kusambaza maneno...ni jambo baya sana!
Ni mawazo yangu!
 
Sijaoa,
Ila kuliko kukaa kimya ba kununa bora useme ns mjadiliane.
Talk,talk talk usikae kimya
 
Nafikiri ni busara kama unaona mambo magumu ni bora kuachana tu kuliko kusambaza maneno...ni jambo baya sana!
Ni mawazo yangu!
Sio kusambaza kwa watu. Yupo tu mtu wangu wa karibu nitamwambia. Na nitakachosema ni cha ukweli na sio uongo
 
Au mmekosana then kilamtu anaanika madhaifu ya mwenzie....
Mnapatana,sisi waja tunakuwa tunawachora tu.Wekeni maji kwa kinywa,haipunguzi chochote
Kuanika madhaifu nakubaliana na nyie ila kanikosea sijui kafanya nini aisee nitasema tu kwa mtu wangu wa karibu
 
Kusemeana mabaya nje maana ake upendo umeisha chuki imeeingia apo tayari
 
Ndoa nyingi zinaharibika kwasababu mke au mume kumsema mwenzie kwa watu hovyohovyo.Ni vizuri kuongea nyie wawili panapotokea kutokuelewana.Ugumu unatoka wapi,mbona mnavuliana nguo na kushiriki tendo la ndoa?Acheni hii tabia
Huijui dunia wewe. Siyo kila mwenza yuko tayari kwa majadiliano. Kuna wengine akili zao wanazijua wenyewe.
 
Hasa hilo la kutoa taarifa za ndani kwa watu wengine ndilo hasa janga kwa ndoa za kileo, unakuta eti mwenzako ansema kwa wazazi humkazi vizuri,na hzo taarifa unazipata,je ndoa itaacha kuvunjika?
 
Mtu ukiwa na Imani yako kwa mungu,uwezi kumuongelea ovyo mkeo au mmeo kwa watu, wafanyao hivyo hawana ofu ya mungu.
 
Mambo ya ndani yanatokaje nje?
Ila kuna watu hawana vifua kabisa.
Yaani tatizo dogo anaenda kuyasema nje, kuna wengine ataanza kuguna guna mpaka umuulize kuna nini?
Ndio kama ume start engine
Atafunguka yote
Hao mimi huwa wakianza tu kufungua mdomo nawaambia, ishia hapo hapo
Kwani hukuja kuomba ushauri bali unoko tu

Hili mpaka wengine wanawasema ndugu zao wa damu kabisa kwa watu baki
Ni tabia mbaya sana hii
Ni kweli kama unavosema mkuu, hiyo ni tabia mbaya.

Lakini ningependa ufahamu jambo Moja.

Hiyo siyo tabia ambayo Hata wao wanapenda Kuwa nayo, hauwezi amini Kuna wakati wanapokaa pekee Kisha wakianza kuwaza juu ya waliyoongea Huwa wanajutia na kuapa kutorudia kusema hovyo bila Mipaka Lakini hujikuta wakifanya Tena na Tena.

IKO HIVI👇
Kuna aina KUU mbili za watu/hiba katika muktadha WA uongeaji (PERSONALITY TYPE)

Aina ya kwanza Ninapenda kuiita "Mto baridi"
Aina ya pili Ninapenda kuiita"Mto mchemko"

Mto baridi ni Aina flani ya maumbile ambayo watu Hawa Huwa na hifadhi kubwa ya mambo wanayoyapata kupitia milango yao ya fahamu.

KAMWE Hawa hauta sikia wakitoa taarifa ya kitu chochote walicho kiona, walicho kisikia au walicho Fanya.
Wao Wana Uwezo WA kuyapokea mambo mengi na kuyahifadhi bila kuyatoa, na Kwa wao Kuwa hivo ni sawa tu, sio waongeaji na unaweza ukasafiri nae safari ya dar to kigoma akiwa kimya tu, na ukimuuliza vp una tatizo nae atajibu hamna tatizo kwani umeona Nini.

Mara nyingi wao ni watu wa kujibu tu.

Mto mchemko, Hawa ni watu ambao hawana hifadhi ya mambo wanayoyapata kupitia milango yao ya fahamu.

Hawa Kila wanacho kiona, wanacho kisikia na wanachokifanya Huwa kinatoka kupitia midomo Yao, Hawa hawawezi kustaemili kuhifadhi mambo hayo.

Hawa wako tayari kutoa Hata Siri za ndani Kwa watu,
IKIWA hawatampata WA kumwambia watampigia MTU yoyote simu na kumueleza, "unajua nilicho kiona, unajua nilicho kisikia,"

Na ikiwa hawatampata WA kumwambia wanaweza Hata kujifungia ndani na kujiambia wao wenyewe.

Mara nyingi Mto baridi Huoa/kuolewa na Mto mchemko Kwa sababu couple Yao Huwa ya kuvutia sana.

Sasa Ikiwa wewe ni Mto baridi na ukaoana na Mto Mchemko basi utakua na wakati mzuri kwani hautawaza jinsi ya kuendesha mazungumzo kazi yako itakua kujibu Maswali na kutoa ushirikiano WA mmh, ndio, ok, ooh, sawa, kumbe n.k.

Na ikiwa Wewe ni Mto mchemko na ukaoana na Mto baridi utakua na wakati mgumu kwani utabwabwaja maneno muda wote wakati mwenzako yupo kimya na akikuunga mkono Kwa wakati mdogo.

Tafiti zinasema kuwa baada ya Miaka mitano ya Ndoa hiyo Mto mchemko anaweza kubadilika na Kuwa na Uwezo mzuri WA kuzungumza Kwa mpangilio mzuri unaoendana na mwenza wake.
Pia Mto baridi nae anaweza kubadilika na Kuwa muongeaji Kwa kiwango kinachompendeza mwenzi wake.

Lakini ili kufanikisha hili ni Hadi wawe wameamua kujifunza jinsi ya kuboresha mapenzi kwenye ndoa Kwa Kuelewa Lugha sahihi za kuwasiliana kimapenzi.

Kwani katika kujifunza huko Kuna mazoezi ambayo watayafanya ambayo yatabadili Hali zao.

#counselorMau
 
😂😂😂😂😂
Hapa watu wanatoa porojo tu. Asilimia 99 ya wanawake huadithia mambo yake na mume wake kwa watu, anaweza akamwambia rafiki yake au ndugu yake lakini kuongea na mtu ni kawaida sana.
 
Hapa watu wanatoa porojo tu. Asilimia 99 ya wanawake huadithia mambo yake na mume wake kwa watu, anaweza akamwambia rafiki yake au ndugu yake lakini kuongea na mtu ni kawaida sana.
Hata wanaume pia husimulia washikaji zao mambo yao na wake zao.
 
Ndoa nyingi zinaharibika kwasababu mke au mume kumsema mwenzie kwa watu hovyohovyo.Ni vizuri kuongea nyie wawili panapotokea kutokuelewana.Ugumu unatoka wapi,mbona mnavuliana nguo na kushiriki tendo la ndoa?Acheni hii tabia
kutoa siri za ufalme ya nguvu na udhaifu wako kwa watesi wako ni kitu mbaya na hatari sana maishani.

ni muhimu kuepuka hiyo ujinga my friends, ladies and gentleman katika ndoa, mahusiano na uchumba :NoGodNo:
 
Back
Top Bottom