Usimuache mtoto peke yake kwenye gari. Joto linaweza kumuua

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Haushauriwi kumuacha mtoto mwenye umri mdogo akiwa peke yake kwenye gari huku madirisha yakiwa yamefungwa hasa wakati wa jua kali au baada ya kuendesha gari husika umbali mrefu. Hali inayoitwa Heat Stroke inaweza kutokea.

Hutokea baada ya mifumo ya mwili kushindwa kudhibiti ongezeko la ghalfa la joto kubwa linaloweza kufikia hadi zaidi ya 41°C ndani ya dakika 10-15 za mwanzo.

Heat Stroke inaweza pia kusababisha kupoteza kwa fahamu, kuweweseka, kuzunguzungu, kiu kali, degedege pamoja na kufeli kwa viungo vya ndani ya mwili.

Baadhi ya watoto hasa wale wasiopatiwa msaada wa haraka wanaweza kupoteza maisha au hata kupatwa na changamoto za kudumu kwenye maisha yao hivyo ni muhimu sana kuwapekela hospitalini mapema baada ya kutokewa na changamoto hii.

Aidha, epuka kumuacha mtoto akiwa peke yake kwenye gari katika mazingira yaliyo tajwa hapa

Chanzo: Kids Health
 
Dar walikufa watoto kadhaa mwaka 2005 kutokana na hii kitu
 
Back
Top Bottom