Nchi hii/dunia hii ina sikukuu nyingi sana kiasi kwamba zingine hazipo kwenye orodha za sikuku za kitaifa/kidunia na watu huzisherehekea wajuavyo si kosa. Hakuna mtu anayelazimishwa kusherehekea sikukuu yoyote aijuae na asiyoijua. Babu krismasi/santa claus yupo tangu karne nyingi, si wakristo wote wana utamaduni wa babu krismas hususani afrika. Huyo santa claus ni maarufu huko amerika, ulaya na asia, huku afrika wengine hawana utamaduni huo na hawajui kitu kinachoitwa babu krismasi/santa claus zaidi ya kuona kwenye matangazo ya biashara kwenye televisheni. All in all inaweza kutumika kama alama ya msimu wa krismasi tu na si ibada