Mambo ambalo watanzania wengi hatulifahamu Ni kuwa Ni ngumu kwa mwananchi wa kawaida kunufaika kwa namna yoyote na gas ya Mtwara maama matumizi yake Ni ngumu kwa mwananchi wa kawaida kuitumia.
Gas inayosindikwa kwenye mitungi Si hii tulionayo sasa. Gas inayosindikwa kwenye mitungi Ni petroleum gas ambayo Ni bi-product ya kuchuja crude oil kupata kerosine, petrol na diesel.
Gas tulionayo hapa kwetu Ni natural gas. Ni gas ambayo Ni ngumu kuwa compressed na kuhifandiwa kwenye mitungi. Na emdapo ukafanikiwa kuicompress, gharama ya kuisindika itakuwa juu mno Mara dufu ya bei ya kununua petroleum gas kutoka Iran.
Tutaitumije hii gas?
Kwa vile hii gas Ni ngumu kuisindika, njia pekee ya mtanzania kuitumia Ni kwa kutumia mabomba ya gas au kupitia Umeme.
Njia ya mabomba ya gas Ni njema zaidi maama gas itamfikia mwananchi moja kwa moja. ILA miundombinu ya mabomba ya gas Ni ngumu Sana kuiweka katika makazi yetu ambayo hayajapangiliwa vyema