Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,754
- 4,975
Wakati Rais wa nchi anakula maisha na private jet, Na kufurahia tuzo zisizokuwa na tija kwa watanzania ambao wengi bado wanaishi chini ya dola moja, jiji la Dar es Salaam lenye shule za sekondari za umma 179 zenye wanafunzi 250,000 zina vitabu elfu 82 tu vya somo la lugha ya kiingereza, somo la Civics lina vitabu elfu 50 pekee.
Kuna matundu ya vyoo yasiyozidi 4,000, shule zote zilizopo kwenye manispaa ya Ubungo zina laptops 19 tu, na zaidi ya wanafunzi 50,000 hawana meza wala kiti cha kukalia. Kesho matokeo yakitoka tukiambiwa kwenye darasa la wanafunzi 500 shule ya sekondari Taifa asilimia 95% wamepata division four na zero.
Cheo cha urais pekee kinatosha kumpatia hata mtu 'mwembamba' kuitwa 'mheshimiwa mnene' au mtu mfupi kuitwa 'mheshimiwa mrefu' na sifa zingine kedekede ambazo ukiamua kupachikwa utapachikwa tu kutokana na cheo chako, utaitwa Dr. hata kama haukwenda shule! Lakini ukiwa kama kiongozi wa kweli, unapaswa kujiuliza hato yote yana manufaa gani hali ya kuwa bado wananchi wako ni masikini?
Hawana uwezo kupata milo mitatu kwa siku? Ukiwa kiongozi ambaye si 'humble' utakumbatia hizo tuzo na kupokea sifa mwishowe zinakupofusha na kulewa madaraka. Kiongozi wa aina hii hafai katika jamii za kiafrika.
Nyerere, Mkapa kina Mandela katika uongozi wao kama wangetaka wangepokea zawadi, tuzo, vyeo vya Phd hata uprofesa pia. Lakini hawakutaka, kwa sababu zingekuwa na maana gani hali ya kuwa nchi zetu bado zina changamoto nyingi?
Pia soma
- Rais Dkt. Samia apewa Tuzo ya Gates Goalkeeper Award