Pre GE2025 Usingeweza kumkuta Hayati Magufuli akiacha upuuzi huu wa tuzo zisizo na maana kufanyika

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hata huyo Magufuli wako hiyo PhD yake ni ya mchongo,watu walivyoanza kumzongazonga aeleze vizuri wengine wamepotea hadi leo hata hawajulikani walipo.
 
Hakuna mpenda kusifiwa kama Magufuli.
 
Wanawake ukiwapa sifa unadhani wanaweza kujali chochote ndio huyo mama yenu.hakuna kitu maisha yake ni tuzo tu.
 
Ila kiukweli hii ni hasara tumekula. Trump kakata misaada yeye anakula bata badala ya kupunguza anasa
 
Rais asiye makini anapokea tuzo.yy anachoangalia ni sifa tu,hata kama mtaharibikiwa ilimradi yy kasifiwa kama mwanamke.
 
fanya kazi ndugu hayo unajichosha tu fuata mambo yak unajitafutia pressure bure
 
Nimezungumzia hii ya kuitwa dk Kikwete, dk msukuma, dk Samia.
Sio kila tuzo na shahada kuwa ni udaktari.
Yawezekana Nyerere na mkapa walipewa tuzo na shahada kwa mambo mengine ila sio udaktari.
 
Mkuu, ni mahaba tu au ni fact?
Kivipi?! Kwani uliwahi kusikia mkapa au Mzee Mwinyi wakiitwa Dr Benjamin mkapa au Dr Ali Hassan Mwinyi?!
Au kama waliombwa kupewa heshima hizo wakakataa hilo hatuna ushahidi nalo Mimi nilichoeleza ni kwamba Rais wa kwanza kupewa udaktari wa heshima hapa Tanzania ni mh Jakaya Kikwete.
Kuhusu mahaba Mimi siwezi kusema mh Kikwete ninampenda au ninamchukia !
Ninachothibitisha ni kwamba ninamheshimu kwakuwa ni rais wetu mstaafu.
 
Hakuna mpenda kusifiwa kama Magufuli.
Siyo kweli!
Magufuli alikuwa mtu wa kazi na hakuwa mtu wa sifa!
Ile kusema HAPA KAZI TU alikuwa anamaanisha .
Mara nyingi watu wavivuwavivu ndio hupenda kusifiwa wakifanya japo jambo dogo la kawaida .
Lakini mchapa kazi hata akifanya makubwa yeye hujiona bado hajafanya chochote kutokana na ile ari na tamaa ya kufanya makubwa zaidi.
 
Nimezungumzia hii ya kuitwa dk Kikwete, dk msukuma, dk Samia.
Sio kila tuzo na shahada kuwa ni udaktari.
Yawezekana Nyerere na mkapa walipewa tuzo na shahada kwa mambo mengine ila sio udaktari.
Mkapa na Nyerere walipewa hizo hizo za udaktari wa heshima, lakini KISOMI zapaswa kutajwa mwisho wa jina tu, naona maprofesa wa vyuo vyetu wameamua kuwa mabubu UKWELI hawausemi ! !
 
Wazazi lazima kwanza kutafuta dawa ya hili Tatizo la baadhi ya vyama kulazimisha wanafunzi kuacha masomo na kwenda kwenye sherehe za vyama ,sijui tumefikaje apa, huu ni ujinga mkubwa sana, naambiwa leo DODOM shule katikati ya jiji wanafunzi hawakuendelea na masomo eti wanaenda kwenye sherehe za ccm.

Wazazi tuamuke ccm inataka kufanya watoto wetu kuwa madondocha,

Chama ni imani na haki ya mtu kuamua anakua chama gani kwa akili zake timam sio kulazimisha watoto kwenda kwenye sherehe ili hali sio matakwa yao , wala hawajawa na uwezo wa Pembua ni chama kipi wawe wafuasi , hii inatakiwa tafutiwa dawa mapema sana
 
Nimezungumzia hii ya kuitwa dk Kikwete, dk msukuma, dk Samia.
Sio kila tuzo na shahada kuwa ni udaktari.
Yawezekana Nyerere na mkapa walipewa tuzo na shahada kwa mambo mengine ila sio udaktari.
Acha uvivu wa kusoma.
Nimeweka hapo link.
Nyerere alipewa shahada za udaktari (PhD) nyingi tu...

Hata Mkapa alitunukiwa nyingi tu.

Za Nyerere baadhi hizi hapa chini:-

▪︎ Claremont University Centre (United States of America) - Doctor of Laws for Claremont graduate School California (17th May 1997)

▪︎ Universities of Philippines (Philippines) - Honorary Doctorate of Humanities (12th July 1991)

▪︎ Havana University of Cuba (Cuba) - Honorary Degree of Doctor Of Philosophy (30th Sept 1985)

▪︎ Pyongyang University (Korea) - Honorary Doctorate of Philosophy (28th March 1985)

▪︎ Ljubliana (Yugoslavia) - Honorary Doctoral of Law (26 March 1985)

▪︎ Manila (Philippines) - Honorary Doctor Degree (12th October 1992)

▪︎ Sokoine University of Agriculture (Tanzania) - Doctor of Philosophy Honoris Causa (28th November 1997)

▪︎ University of Fort Hare (South Africa) - Doctor of Laws Honoris Causa (23rd April 1998)

▪︎ Makerere University Kampala (Uganda) - Honorary Doctor of Laws (29th January 1993)

▪︎ nk
 
Mkapa na Nyerere walipewa hizo hizo za udaktari wa heshima, lakini KISOMI zapaswa kutajwa mwisho wa jina tu, naona maprofesa wa vyuo vyetu wameamua kuwa mabubu UKWELI hawausemi ! !
Ningekuelewa kama ungesema mkapa na Nyerere walipewa kama hizohizo wakakataa!
Na Mimi nimemaanisha ule uhalisia kuwa rais wa kwanza kupewa udaktari wa heshima na heshima hiyo ikatajwa kabla ya kutaja jina lake ni mh rais wa awamu ya nne JK!
Baada ya hapo ndiyo imefika sasa hadi watu wa darasa la saba wanapewa heshima hiyo na kutajwa kabla ya kutaja majina yao kama vile Dr Joseph Msukuma!
 
Naona nyingi alitunukiwa akiwa keshang'atuka!
Lakini mzee alistahili hizo sifa asee. Kaandika sana vitabu vya falsafa na uongozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…