Usingizi baada ya chakula cha mchana husababishwa na nini???

Usingizi baada ya chakula cha mchana husababishwa na nini???

Bill of Quantity

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
1,233
Reaction score
406
Wakuu! Habari zenu??
Mimi mwenzenu hapa nasumbuliwa sana na usingizi baada ya kupata chakula cha mchana.
Tatizo ni nini hasa?
Kuna solution ya hili tatizo wakuu??
 
Wakuu! Habari zenu??
Mimi mwenzenu hapa nasumbuliwa sana na usingizi baada ya kupata chakula cha mchana.
Tatizo ni nini hasa?
Kuna solution ya hili tatizo wakuu??

Utakuwa unakula vyakula vizito, huku kazi unayofanya haitaji ufanye hivyo. Jaribu kula msosi mwepesi na matunda kidgo. Maji muhimu pia.
 
Hata mimi ninahiyo hali hapa nilipo nasinzia tu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hiyo Ipo Kwa Wengi, Ila Sifahamu Sababu Labda Kama Kuna Wataalamu Watueleze Ni Kwa Nini?
 
Wakuu! Habari zenu??
Mimi mwenzenu hapa nasumbuliwa sana na usingizi baada ya kupata chakula cha mchana.
Tatizo ni nini hasa?
Kuna solution ya hili tatizo wakuu??

nami uwa na tatizo ilo siku moja nikamuuliza mtu akanijibu ni shauri ya kula chakula cha moto sana na maji ya baridi sa sijui kuna ukweli ndani yake ama ni fix tuu.
 
Hii inatokana na zoezi la mwili ku-digest chakula. Inashauriwa kupata japo dk 5 za kupumzika (siester) ili kuupa mwili nafasi ya kazi hiyo.
 
Wakuu! Habari zenu??
Mimi mwenzenu hapa nasumbuliwa sana na usingizi baada ya kupata chakula cha mchana.
Tatizo ni nini hasa?
Kuna solution ya hili tatizo wakuu??

Pole sana aisee,mi pia lilikuwa ni tatizo langu ila kuna mtu alinishauri nisinywe kinywaji chochote wakati,au baada ya kula mpaka ipite nusu saa au lisaa,imenisadia kwa kweli ebu jaribu,mi nimeshasahau usingizi wa mchana labda niwe naumwa..
 
Pole sana aisee,mi pia lilikuwa ni tatizo langu ila kuna mtu alinishauri nisinywe kinywaji chochote wakati,au baada ya kula mpaka ipite nusu saa au lisaa,imenisadia kwa kweli ebu jaribu,mi nimeshasahau usingizi wa mchana labda niwe naumwa..

asante sana tommie. naanza rasmi dozi kesho.
 
Ukila chakula then ukanywa kahawa, chai, coca cola, pepsi au red bull unauwa nutrients zote zinazopatikana kwenye chakula kwani kwenye kahawa kuna caffeine, chai kuna theophilyne, coca na pepsi kuna cocaine na red bull kuna taurine na kuhusu kusinzia ukishakula ili digestion ifanye kazi kiasi kikubwa cha damu kinashuka tumboni kwa ajili ya kazi hiyo ndo maana mtu anakuwa lazy na kusinzia ila ukila light food au matunda hupati shida kama mtu aliyekula heavy meal.
 
mkuu kahawa ya aina gani? wataalam wanadai kahawa ina madhara makubwa sana kiafya.
cc MziziMkavu
Kahawa kama utakunywa kiasi haina madhara kwa afya yako ila kama utakunywa kwa wingi sio nzuri .

UKWELI KUHUSU UNYWAJI KAHAWA







Kahawa ni miongoni mwa vinywaji maarufu sana duniani. Mamilioni ya watu hunywa kahawa kila siku, ama wakiwa nyumbani, ofisini au matambezini. Ladha nzuri na uchangamfu anaoupata mtu baada ya kupata kikombe kimoja au viwili, ndiyo sifa pekee na kubwa iliyonayo kahawa.

Kutokana na umaarufu na matumizi yake kuwa makubwa kiasi hicho, tafiti kadhaa za kisayansi zimefanyika na zinaendelea kufanyika ili kujua faida na hasara za kinywaji hiki katika afya ya binadamu.

Baada ya tafiti nyingi kufanyika, ukweki umedhihirika kuwa kahawa inapotumika kwa wastani, haina madhara kiafya bali ina faida. Wastani unaozungumziwa hapa, ni ule wa kunywa vikombe vya ukubwa wa watsani visivyozidi vinne mpaka vitano kwa siku.

Aidha, mwongozo uliotolewa hivi karibuni na Wakala wa Viwango vya Vyakula wa nchini Uingereza, umependekeza kuwa wanawake waja wazito wasinywe kahawa zaidi ya vikombe viwili kwa siku, sawa na miligramu 200.

Katika muongozo huo, imetahadharishwa kutokuzidisha kiwango cha ‘caffein'e mwilini kwa kunywa vinywaji vingine pia ambavyo vina kiasi kikubwa cha ‘caffeine' ikiwa ni pamoja na vinywaji baridi kama Coca-Cola, Chai, Chokoleti na vinywaji vingine vya kuongeza nguvu.

UHUSIANO WA SARATANI NA KAHAWA

Utafiti na makala nyingi zilizoandikwa kuhusu ugonjwa wa Saratani, zinaonesha kuwa binadamu tunaweza kujiepusha kwa asilimia 35 na magonjwa mbalimbali ya satarani, kwa kuzingatia lishe bora na kubadili mtindo usiofaa wa maisha.

Kila mwaka, zaidi ya watu milioni 10 duniani hupatwa na Saratani na zaidi ya watu milioni 6 hufariki dunia kutokana na magonjwa mbalimbali ya Saratani. Tafiti mbalimbali zimefanyika kuhusu unywaji wa Kahawa na uwezo wa kahawa kuzui au kusababisha Saratani.

Matokeo ya utafaiti huo, umeonesha kuwa unywaji wa Kahawa hauna athari mbaya zinazohusiana na ugonjwa wa Saratani na badala yake kuna uwezekano mkubwa wa kahawa kutoa kinga kwa aina kadhaa za saratani.

Aina za Saratani zilizofanyiwa utafiti kwa kuoanisha na matumizi ya kahawa ni pamoja na Saratani ya Kizazi (Ovarian Cancer), Saratani ya Kibofu cha Mkojo (Bladder Cancer), Sratani ya Tumbo (Bowel Cancer), Saratani ya Ini (Liver Cancer) na Saratani ya Kongosho (Pancreatic Cancer).

Katika hitimisho lao, jopo la wataalamu kutoka Mfuko wa Dunia wa Utafiti kuhusu Saratani, wapatao 21 ambao wanahehsimika duniani, baada ya kupitia na kutathmini tafiti 7000 kuhusu matumizi ya vinywaji pamoja na kahawa, walihitimisha kwa kusema kuwa ni dhahiri kahawa haihatarishi mtu kupatwa na saratani ya kongosho wala figo.

Zaidi ya hayo, taarifa zilizopo za kisayansi zinaonesha kuwa unywaji wa kahawa siyo sababu ya mtu kupatwa na saratani ya aina yoyote katika mwili, bali kahawa imeonesha kuwa kinga ya baadhi ya saratani, hususani Saratani ya Ini, Saratani ya Utumbo mdogo na Saratani ya Kizazi. Muhimu mtu azingatie kiwango.

 
mkuu MziziMkavu nashukuru sana kwa tathmini yako na report hiyo juu ya kahawa.
Kahawa naiogopa sana kwa sababu nilikuwa najua inasababisha High BP, nimeelimika leo.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu utakuwa una nyota ya chatu...hahahahahha...natania,ila jamaa hapo juu wameeleza vyema
 
Io inatokana na tokana ukisha kula chakula damu nyingi huenda kwenye tumbo na hapo sehemu nyingne kama kichwani hupungukiwa damu nakufanya kuanza kusikia usingizi hali hii hutokea akat ukiwa umekaa tuu.hio ndo knowledge ndugu by Dr.Oscar
 
Back
Top Bottom