Usingizini huo ndio muda ambao unakuwa dhaifu kuliko muda wowote katika maisha yako

Usingizini huo ndio muda ambao unakuwa dhaifu kuliko muda wowote katika maisha yako

stabilityman

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2024
Posts
857
Reaction score
1,810
Unapokuwa usingizini huo ndio muda ambao unakuwa dhaifu kuliko muda wowote katika maisha yako, unapolala mtu yeyote anaweza kukudhuru kwa namna yoyote ile na usiweze kujitetea. Hakikisha unapolala usingizi kama kuna mtu pembeni yako basi awe ni mtu ambaye unamuamini na unamfahamu vizuri, Usilale na mtu ambaye mmekutana tu barabarani hujui lolote kuhusu yeye, kama ni mwanamke anayejiuza hakikisha mnamalizana mapema aondoke zake akuache umelala peke yako, wengi wameibiwa, wengi wamepoteza maisha kwa kupitia huu udhaifu tunaokuwa nao pindi tumelala. Usiishi kwa mazoea! Kuna mtu unaweza kukutana naye ukahisi mmeonana tu kwa bahati mbaya kumbe ni mtu anayekuwinda muda mrefu uingie kwenye anga zake amalizane na wewe, Kuna wadada pia unaingia chumbani ukilala tu anawapigia simu masela wake waje kubeba vilivyo vyao, ukiachwa salama shukuru Mungu wako maana huwa hawataki kuacha ushahidi!
 
kwa kweli sisi zetu ni dua tu. ilisikika sauti ya bwana mmoja aliekua amevaa msuri na barakashia
 
Usilale na mtu ambaye mmekutana tu barabarani hujui lolote kuhusu yeye, kama ni mwanamke anayejiuza hakikisha mnamalizana mapema aondoke zake akuache umelala peke yako,
Yote hii ni kuchelewesha hatima?
 
Lakini wataalamu wanasema japo kuwa umelala, sehemu fulani ya ubongo wako bado inafanya kazi. Anyway lakini malaika mlinzi huwa wanatulinda ili baya lisitupate
 
Lakini wataalamu wanasema japo kuwa umelala, sehemu fulani ya ubongo wako bado inafanya kazi. Anyway lakini malaika mlinzi huwa wanatulinda ili baya lisitupate
kuna watu hata wakilala wanajua kinachoendelea nje.
 
Umetoa ushauli mzuri sana kwa mtu aliyepitiwa na majanga ya kufokolewa nadhani atakuwa amekupata,mimi nikiwepo nilipata zombie nikaenda lala nae kumbe nilijaa kunye mfumo wake nashukulu nilibaki kuwa hai ila alichukua pesa na simu,
 
Pole sana ... Mtu wa design hiyo ni rahisi hata kukuua
 
Back
Top Bottom