Sielewi kwanini watumiaji wa iphone wanaonekana "wanajisikia" sana
Kama kigezo cha kuonekana malimbukeni sababu iphone ni GHALI......basi iphone sio simu ghali pekee, wapo akina Samsung Huwawei nk na wana bei ghali sana kwenye flag ship zao
Kwenye maisha kila mtu anavipaumbele vyake........hakuna raha kwenye maisha kama kufanya jambo unalolipenda na kuliamini wewe binafsi, ni raha zaidi kuliko kufanya mambo kwa mujibu wa "fomula"
Sio kila apendacho mwenzako lazima kilete maana kwako au ukitafsiri kwa mujibu wa ulivyo karirishwa maisha yanatakiwa kuwaje
Utakuta mtumiaji wa tekno labda anamtukana kweli mtumiaji wa iphone kwamba anachezea hela wakati amepnga kwa mtogole wakati yeye mwenye na tecno yake kapanga pia kwa mtogole, unabaki ujiuliza kwanini yeye asijenge masaki kwasababu anatumia tekno ya laki?
Jamani tutafuteni hela tushibishe matakwa ya nafsi zetu
Kama wewe unadhani kumiliki iphone ndio kukwamisha maendeleo yako hiyo ni wewe tu ujuaji wako, wenzako wanamiliki na wanapanda daladala kama wewe mwenye itel
Katika maisha yako hata siku moja usitumie umasikini wako kuharamisha matumizi ya vitu vizuri kwa wenzio
Kama wewe huwezi wenzio wana weza