Usioe au kuolewa sababu unamhurumia huyo mtu. Oa au olewa sababu unampenda

Usioe au kuolewa sababu unamhurumia huyo mtu. Oa au olewa sababu unampenda

Wapo mamilioni ya watu walio oana kwa huo msingi wa kupendana na bado wakaangukia pua ,na wapo wengine ambao walioa na kuolewa bila ya kuangalia kigezo hicho ulicho kisema na bado ndoa zao zikadumu na zikawa na amani.

Ni kweli hutakiwi kuoa au kuolewa na mtu kwa kumuonea huruma, lakini pia hutakiwi kumuoa au kuolewa na mtu kwa kigezo cha kumpenda tu bali pia awe mtu anaye sitahili na atakaye kufaa kwenye maisha yako na watoto wako utakao wazaa.

Moyo huwa unapenda popote pale bila kujali ni kuzuri au ni kubaya,na ndio maana huwa unaambiwa kuwa kitu chochote kinacho husiasa na msitakabali wa maisha yako hutakiwi kufanya uamuzi kwa kufuata hisia za moyo wako bali tumia akili.

Moyo una weza kukufanya ukapempenda mtu ambaye hana sifa ya kuwa mme au mke na ambaye hakufai kwenye maisha yako, sasa ww jitie kumuoa eti kisa una mpenda huuone moto wake.
 
Katika utayari mtu anakwenda beyond emotions.

Kwa kwenda beyond emotions anakuwa ametumia maturity kufanya reasoning ili kujua kama ana utayari wa kukubali kwamba kwenye ndoa anapaswa kufikiria kama yupo tayari kuachana na ubinafsi, yupo tayari kuchangia katika kuijenga na kuiimarisha taasisi ya ndoa badala ya kufikiria kama sehemu ya kuvuna, kama yupo tayari kuelewa ndoa ndiyo chimbuko na asili ya watoto wake na ndiyo kwao, siyo kwa babu au bibi.

Utayari wa kujinyima kutumia muda mwingi na marafiki na watu wengineo na mambo mengine, na kuruhusu Utayari wa kutumia muda mwingi na mwenza na kuwa muwazi.

Utayari wa kuona kwamba kupenda siyo kitu pekee cha kiangalia, bali anapaswa kujiuliza na kuona kama huyo ampendaye atafaa. Upendo unapaswa ku add value katika maisha badala ya kuwa chanzo cha mateso, majuto n.k, hivyo ni muhimu sana baada ya kupenda mtu akajiuliza kama ampendaye atamfaa.

Kwa uchache ni utayari katika hayo.
Point sana hii.
Ila hapo kwenye ubinafsi na kujitoa, wanawake ni tatizo sana.
 
Kuna ujinga unakuta mtu anasema naoa au naolewa sababu namhurumia huyo mtu ninayemuoa au ninayeolewa naye

Usioe au kuolewa sababu unamhurumia huyo mtu, oa au olewa sababu unampenda huyo mtu

Kigezo kikubwa kiwe upendo sio huruma
Uzuri wa upendo uwe bidirectional, sasa usiombee wewe unapenda mwenzako hakupendi hasa kwa wanaume, wanawake wengi tulio nao wapo na sisi sababu ya fedha.

Upendo ukiwa bidirectional utainjoy, la sivyo bora uwe single tuu.
 
Utajuaje unampenda mtu?

Ukiweza mvumilia katika matukio anayokupiga na bado huoni sababu ya kumuacha basi huyo Umempenda.

Ukiona matukio anayokupiga huyawezi,huyamudu, basi songa mbele kama injili tafuta uliempenda Umuoe/Akuoe.

Tunaoa/kuolewa na tunaowapenda na sio wanaotupenda.

Ukiweza Penda utaweza vumilia aina zote za matukio/maisha na hapo ndipo penye upendo.
Sahihi
 
Kuna ujinga unakuta mtu anasema naoa au naolewa sababu namhurumia huyo mtu ninayemuoa au ninayeolewa naye

Usioe au kuolewa sababu unamhurumia huyo mtu, oa au olewa sababu unampenda huyo mtu

Kigezo kikubwa kiwe upendo sio huruma
Kwaiyo wakati anamtongoza alikuwa anamhurumia?
 
Upendo nao hupungua. Mambo yanabadilika. Unawezamoenda mtu Leo akafanya jambo upendo ukayeyuka. Au hapa unaongelea upendo gani?
 
Anayeoa kwa kuhurumia na anayeoa kwa kupenda, hawana utofauti wowote.
Oa kwa sababu huyo mwanamke ataweza kukuzalia na kukulelea wanao vizuri hata wakati ambao hautakuwepo chini ya jua.
 
Back
Top Bottom