Usioe au kuolewa sababu unamhurumia huyo mtu. Oa au olewa sababu unampenda

Wapo mamilioni ya watu walio oana kwa huo msingi wa kupendana na bado wakaangukia pua ,na wapo wengine ambao walioa na kuolewa bila ya kuangalia kigezo hicho ulicho kisema na bado ndoa zao zikadumu na zikawa na amani.

Ni kweli hutakiwi kuoa au kuolewa na mtu kwa kumuonea huruma, lakini pia hutakiwi kumuoa au kuolewa na mtu kwa kigezo cha kumpenda tu bali pia awe mtu anaye sitahili na atakaye kufaa kwenye maisha yako na watoto wako utakao wazaa.

Moyo huwa unapenda popote pale bila kujali ni kuzuri au ni kubaya,na ndio maana huwa unaambiwa kuwa kitu chochote kinacho husiasa na msitakabali wa maisha yako hutakiwi kufanya uamuzi kwa kufuata hisia za moyo wako bali tumia akili.

Moyo una weza kukufanya ukapempenda mtu ambaye hana sifa ya kuwa mme au mke na ambaye hakufai kwenye maisha yako, sasa ww jitie kumuoa eti kisa una mpenda huuone moto wake.
 
Point sana hii.
Ila hapo kwenye ubinafsi na kujitoa, wanawake ni tatizo sana.
 
Kuna ujinga unakuta mtu anasema naoa au naolewa sababu namhurumia huyo mtu ninayemuoa au ninayeolewa naye

Usioe au kuolewa sababu unamhurumia huyo mtu, oa au olewa sababu unampenda huyo mtu

Kigezo kikubwa kiwe upendo sio huruma
Uzuri wa upendo uwe bidirectional, sasa usiombee wewe unapenda mwenzako hakupendi hasa kwa wanaume, wanawake wengi tulio nao wapo na sisi sababu ya fedha.

Upendo ukiwa bidirectional utainjoy, la sivyo bora uwe single tuu.
 
Sahihi
 
Kuna ujinga unakuta mtu anasema naoa au naolewa sababu namhurumia huyo mtu ninayemuoa au ninayeolewa naye

Usioe au kuolewa sababu unamhurumia huyo mtu, oa au olewa sababu unampenda huyo mtu

Kigezo kikubwa kiwe upendo sio huruma
Kwaiyo wakati anamtongoza alikuwa anamhurumia?
 
Upendo nao hupungua. Mambo yanabadilika. Unawezamoenda mtu Leo akafanya jambo upendo ukayeyuka. Au hapa unaongelea upendo gani?
 
Anayeoa kwa kuhurumia na anayeoa kwa kupenda, hawana utofauti wowote.
Oa kwa sababu huyo mwanamke ataweza kukuzalia na kukulelea wanao vizuri hata wakati ambao hautakuwepo chini ya jua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…