Peter Mwaihola
JF-Expert Member
- Jun 23, 2022
- 276
- 460
Kuna dhana imejengeka miongoni mwa jamii kuwa haifai kwa mwanaume kuoa mwanamke aliyekutana nae maeneo ya starehe kama vile Bar, klabu na kwingineko.
Watu wengi wamekuwa wakiwahusisha wanawake hao na tabia zisizofaa ikiwemo ulevi, umalaya na udanganyifu hivyo huwatenga kuwa hawafai kuolewa.
Kwa jamii ya sasa kuna kundi lingine la wanawake na wanaume ambao pia huzungumziwa kwa ubaya inapofika suala la uchaguzi wa ndoa iwe kuoa ama kuolewa.
Sio ajabu kusikia kuwa haifai kuoa mwanamke au mwanaume wa kukutana nae kwenye mitandao ya kijamii kama vile WatsApp, Facebook, X na kwingineko.
Imejengeka kuwa hakuna mapenzi ya kweli kwenye mitandao ya kijamii bali kudanganyana na tamaa ya pesa au ngono.
Hata hivyo hakuna sehemu iliyoanzishwa kuwa maalumu kwa ajili ya kupata wanawake au wanaume bora.
Ubora wa mwanaume au mwanamke upo kwenye moyo wake na matendo yake binafsi haijalishi anatoka kwenye familia ipi, jamii ipi au kabila gani.
Unaweza kukutana na mwanamke kanisani ukaamini kuwa huyu ndiye, lakini ukaangua kilio baada ya kukutana na mambo mabaya kumuhusu.
Wapo waliowahi kuoa wanawake wadangaji wa Bar lakini ndoa zao zipo imara mpaka leo.
Pia wapo waliokutana na wakapendana kupitia mitandao ya kijamii wakaoana na mpaka leo wanaishi vizuri pasipo na tatizo lolote.
Unaweza kupata mume au mke bora kanisani, kijiweni, mtandaoni na bar.
Hakuna mipaka ya kupata mwenza bora bali fanya utulivu kuchagua aliyebora kwa ajili yako na utakayeweza kumudu kubadilisha madhaifu yake kumfanya awe bora zaidi ya ulivyomkuta.
Usioe au kuolewa na mtu ambaye huwezi kumvumilia na kumbadilisha kwaadhaifu aliyonayo mtashindwana.
Tembea na vipaumbele vyako huku ukitambua kuwa mke au mume bora anaweza kupatikana popote.
[emoji2398] Peter Peter Mwaihola