kWa tathimini ya harska 100k litres inaweza isha kwa muda gani
Eli hizo ltrs zishe unahitaji kuwa na average sales ya ltrs 3400 per day, iwe Disiel na petrol, Changamoto kubwa ya Hii biashara ni jinsi ya kupata wateja wengi Kwa siku , Kadri mauzo yanapokuwa makubwa ndio unaweza pata Faida kubwa. Hii biashara Ina fixed cost nyingi sana ambazo hazitegimie umeuza au hujauza ,. Mfano leseni ya Ewura, Fire, OSHA, Salary ya manager, pump attendant watatu Hadi wanne, walinzi, Umeme, Maji, Kuna hao Jamaa wanaofunga vimashine vya risiti, Kuna TRA, Kuna services levy, Kuna nssf.
Eli Uwezi kupata Faida nilaxima uzee kuanzia. Ltrs 4990-5000 per day hapo kidogo utakuwa huru, Kuna short za wafanyakazi, Kuna wafanyakazi kuchanganya Mafuta kwenye magari. Kuna short za Mafuta zinazokuja na magari yaliyoleta Mafuta hizi zipo aina. Mbili:- ya kwanza utaiona Juu ya gari wakati unapima Mafuta yaliyoleta utaona tofauti kwenye stick ya gari. Aina ya pili ya short Hii utaikuta chini ya tanki lako unashusha Mafuta ltr 5000 halafu ukipims ndani ya kisima vhako unakuta inasoma ltrs 4500 hapo unakuwa umepoteza ltrs 500 ukimkuta dereva smart anakuruka anasema yeye hahusike na short ya tanki lako! Hii short ya chini inaletwa na madereva wajanja wanatengeza stick ama wanaweka kitu kwenye sehemu ya kupimia Mafuta kwenye gari Mafuta yanapanda Juu, wewe unaona yapo sawa kumbe amechota ltr 500, piya inaweza kuletwa na pump kuzidisha Mafuta bila wewe kujuwa insdhauriwa kufanya pump test Kwa Kutumia kipimo cha ltr 20 ambacho kipo specially mara mbili Kwa mwezi, au Kuna kuvuja Kwa pump under ground or tank kuvuja au tank kuchezea.
Eli Uwezi kufanya biashara Hii vizuri jitahidi kupata wahudumu wakarimu na wazoefu, Sumu namba moja ogopa mabasi makubwa hao ni wakopani number Moja, anakopa ni agent akisindikiza basi alete Hela risk ya kutokulipwa ni kubwa, Wateja wazuri ni Daladala, fudo tipper na malori, gari ndogo, pikipiki, Kuna njia za kudeal na madereva nazo ni kuwapa punguzo ama kuwa Salio mwisho wa mwezi. Ila hizo njia zote mbili ni njia hatari ambazo wafanyakazi wako watazitumia kukupiga bao/ kukuibia wewe.
Kwa ushauri zaidi na maelezo unaweza kunitafuta nikakusadua mbinu mbalimbali za kudhibiti wexi kutoka Kwa wafanyakazi wako