Usiombe kukutana na mpenzi mdekaji!

Usiombe kukutana na mpenzi mdekaji!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
Kudeka ni tabia ya mtu kutaka kupata kila anachokitaka kwa wakati anaotaka, kufanyiwa kila kitu bila kujishughulisha sana, kubembelezwa kila wakati na kutoambiwa kwamba amekosea. Mtu anayedeka pia ni kng'ang'anizi, yaani hupenda kuona akikaguliwa na kutazamwa mara kwa mara . kwa ujumla mtu wa kudeka ni mfanyiwaji na siyo mfanyaji na mpokeaji na siyo mtoaji. Inapotokea mtu akaoa au kuolewa na mdekaji kuna uwezekano kwa ndoa hiyo kuwa ya mashaka makubwa.

Labda tu pale mdekaji anapokuwa anajua kwamba anadeka na mwenzake akajua kuwa ameoa au kuolewa na mdekaji.
Kujua na kukiri juu ya tatizo au kasoro yoyote ni hatua ya awali ya kupata ufumbuzi wa tatizo hilo. Kwa hiyo wanandoa wanapojua wote kuhusu tatizo hili wanakuwa kwenye nafasi nzuri ya kutatua matatizo yote yatakayotokana na udekaji huo. Lakini wasipojua kitakachotokea ni kukatika kwa mawasiliano mara kwa mara. Mtu anayedeka anataka kuona mwenzake akimjali katika kiwango ambacho ni vigumu kwa mwenzake huyo kumudu. Kudeka kuna maana ya mtu kutokuwa tayari kutazama upande wa pili, yaani kumtazama mpenzi wake, bali yeye tu ndiye atazamwe.

Jambo hili kwenye uhusiano huchosha haraka, kwani upendo ni kama njia mbili zinazopishana, huyu akifanya hiki na mwingine afanye kile. Ikishakuwa ni ya upande mmoja, upendo hunyauka haraka. Anayedeka anataka kuona anachokitaka anakipata au kinatekelezwa, kwani ndivyo alivyozoeshwa utotoni, kwamba hata akililia mwezi anapatiwa. Kwenye uhusiano anapolia na kuona hajibiwi kwa kupata anachotaka hudhani kwamba upendo umekwisha au haupo. Kuna wale wanaume au wanawake ambao hata katika mazingira magumu vipi wakitaka kitu, ni lazima wapewe iwe ni mali au hata hisia. Ni jambo la kawaida sana kwa mtu anayedeka kushindwa kuiona hali halisi katika uhusiano.

M
ara nyingi anachokiona ni yeye, yaani hujiona mwenyewe na utashi au mahitaji yake, kamwe hamuoni mwenzake. Hii ina hatari zake, kwani kwa upofu wake hukanyaga na kupondaponda yale mambo au hali ambazo ndizo zingesababisha kujenga uhusiano mzuri na mwenzake. Kwa kawaida, uhusiano na mtu anayedeka hukera sana kwa sababu matarajio ya mdekaji siku zote yako kinyume na hali halisi. Mdekaji yeyote huwa haridhiki na upendo anaopewa au kuonyeshwa. Haridhiki kwa sababu hadekezwi wakati kudekezwa kwake ndiyo upendo.
 
Dingi:
Kupenda kufanyiwa kila kitu bila kufanya ni UVIVU
Kutaka unavyotaka hata kwenye mazingira magumu ni UBINAFSI
Raha ya KUDEKA ni KUDEKEZANA, u give some u get some.
Spoiled brat sio sawa na anayedeka...
Mwanangu mie huwa nadeka kisirisiri, wala mama yenu hajui kuwa nadeka........................LOL
 
Heshima yako baba,kwakweli kudekezwa raha sn,ila inapendeza mnapodekezana wote means kila mtu aonje hiyo raha!mambo ya mahusiano yasiyokua na kudekezana as if tuko jeshin binafsi cyataki kbs aisee!
 
tatizo lao kubwa wanapenda dekezwa tu kamwe wao hawadekezi wapenzi wao...yaani always do stuff for them but thy will never do anything in return
 
kudeka raha, na raha ya kudeka umpate anayejua kudekeza lolz.
ila me nasikia wanaume wanapenda wanaweke wanao deka na sio wale wanaojitia madume jike et! na kudeka kusipitilize kunakuwa kero ss! na iwe two way traffic yan mnadekezana.
 
hehehe, kwani unadhani hatujui baba?
ila kuna mijitu inadeka afu mibinafsiiii! anajihisi anastahili peke yake!
ila mie mkweo akishindwa kunidekeza narudi kudeka home afu atajibebaaa!:A S embarassed:
Mwanangu mie huwa nadeka kisirisiri, wala mama yenu hajui kuwa nadeka........................LOL
 
Mpenzi wangu anapodeka huniweka active! Ila kwa maelezo ya hapo juu, huyo si mdekaji kwa maana ya kudeka kwa mpenzi, ni mvivu, mbinafsi, mchoyo nk nk nk.............
 
mtu anaedeka bila kiasi mie hata simtaki.

Hata kama ni rafiki wa kawaida nitamkimbia maana atakua na umimi mwingi
 
Mimi sidekezi mtu, kwani tumekuwa watoto wa miezi sita.
 
ila wewe siku ya kukucheza ngoma inabidi tuhamie gereza la ukonga miezi sita!
tukuchemshe na viungo hadi ukolee, msitu wa mabwe pande utamalizika, kha!
kupika hujui:smash:, kudekeza sifuri!:rant:
Umenikumbuisha, ngoja nikamdekeze sasa hivi
Maana jana nilideka mie
 
Back
Top Bottom