Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,421
Kudeka ni tabia ya mtu kutaka kupata kila anachokitaka kwa wakati anaotaka, kufanyiwa kila kitu bila kujishughulisha sana, kubembelezwa kila wakati na kutoambiwa kwamba amekosea. Mtu anayedeka pia ni kng'ang'anizi, yaani hupenda kuona akikaguliwa na kutazamwa mara kwa mara . kwa ujumla mtu wa kudeka ni mfanyiwaji na siyo mfanyaji na mpokeaji na siyo mtoaji. Inapotokea mtu akaoa au kuolewa na mdekaji kuna uwezekano kwa ndoa hiyo kuwa ya mashaka makubwa.
Labda tu pale mdekaji anapokuwa anajua kwamba anadeka na mwenzake akajua kuwa ameoa au kuolewa na mdekaji. Kujua na kukiri juu ya tatizo au kasoro yoyote ni hatua ya awali ya kupata ufumbuzi wa tatizo hilo. Kwa hiyo wanandoa wanapojua wote kuhusu tatizo hili wanakuwa kwenye nafasi nzuri ya kutatua matatizo yote yatakayotokana na udekaji huo. Lakini wasipojua kitakachotokea ni kukatika kwa mawasiliano mara kwa mara. Mtu anayedeka anataka kuona mwenzake akimjali katika kiwango ambacho ni vigumu kwa mwenzake huyo kumudu. Kudeka kuna maana ya mtu kutokuwa tayari kutazama upande wa pili, yaani kumtazama mpenzi wake, bali yeye tu ndiye atazamwe.
Jambo hili kwenye uhusiano huchosha haraka, kwani upendo ni kama njia mbili zinazopishana, huyu akifanya hiki na mwingine afanye kile. Ikishakuwa ni ya upande mmoja, upendo hunyauka haraka. Anayedeka anataka kuona anachokitaka anakipata au kinatekelezwa, kwani ndivyo alivyozoeshwa utotoni, kwamba hata akililia mwezi anapatiwa. Kwenye uhusiano anapolia na kuona hajibiwi kwa kupata anachotaka hudhani kwamba upendo umekwisha au haupo. Kuna wale wanaume au wanawake ambao hata katika mazingira magumu vipi wakitaka kitu, ni lazima wapewe iwe ni mali au hata hisia. Ni jambo la kawaida sana kwa mtu anayedeka kushindwa kuiona hali halisi katika uhusiano.
Mara nyingi anachokiona ni yeye, yaani hujiona mwenyewe na utashi au mahitaji yake, kamwe hamuoni mwenzake. Hii ina hatari zake, kwani kwa upofu wake hukanyaga na kupondaponda yale mambo au hali ambazo ndizo zingesababisha kujenga uhusiano mzuri na mwenzake. Kwa kawaida, uhusiano na mtu anayedeka hukera sana kwa sababu matarajio ya mdekaji siku zote yako kinyume na hali halisi. Mdekaji yeyote huwa haridhiki na upendo anaopewa au kuonyeshwa. Haridhiki kwa sababu hadekezwi wakati kudekezwa kwake ndiyo upendo.