Hi guys!!!
Mwenzenu kilichonipata,[emoji23] [emoji23]
Tareh 15 mwezi uliopita nilimwacha aliyekuwa mpenzi wangu.
Sasa basi tarehe 28 mwezi uliopita ilitakiwa nisafiri kwenda mwezini ( kwa wakubwa tuu wataelewa).
Siku imefika safari haijaanza, nikasema labda kesho, kesho yake wapi ndiyo kwanza hata dalili sioni[emoji17] [emoji17] .
Ikafika tarehe tatu nikasema hapa baby nimemwacha ukute nina chata yake tayari sijui nitafanyaje, kwa kuwa alikuwa bado ananibembeleza nikasema ngoja ninunue preg test nipime kama ipo nimsamehe kama haipo nimlime total ban.
Nikanunua kipimo nikapima kikaonyesha sina, ila sikuamini maana hofu tayari ilishanifanya nihisi nina dalili za ujawepesi[emoji12] .
Nikahisi nimekosea kupima, nikaenda kununua vingine viwili, na kile cha mwanzo vikawa vitatu nikapima majibu yakaja yale yale.
Mpaka Jana asubuhi ikawa bado.
Nikaingia Google nikagundua vile vipimo huwa havisemi ukweli % zote.
Nikaamua kununua vingine vi 3 makampuni tofauti, majibu yakawa yale yale,
Hapo nimeshaanza kuchart na ex naelekea kumsamehe, nisije mwacha kumbe Nina mtoto wake mtoto wangu aje akose baba bure!!!.
Mchana nikaenda hospital kupima cha ajabu nao kipimo wanatumia vya aina ile ile.
Nikarudi nyumbani nimesinyaa.
Hapo tumbo linauma siku mbili kama naingia hedhi lakini siingii ila nikaambiwa ni dalili moja wapo ya ujauzito.
Nikafika nyumbani nikalala kuamka mwezi huo hapo nauona[emoji14] [emoji14] [emoji14] [emoji14] .
Ilibaki kidogo nizikumbatie yaani niliruka ruka kama vile nimeshinda BIKO yani.
Ila sasa hela nilizotoa kununua hivyo viupuuzi zinaniumaje[emoji34] [emoji34] [emoji34] [emoji34] .
Nani mwingine aliwahi kukutwa na hii kitu??
Wale team watakatifu wa "kwa nini ulizini kabla ya ndoa", sitaki ushauri jamani sitaki kupangiwa matumizi. Na sijakoma japo niliahidi kukoma.