Usipende kutoa siri za biashara yako kwa watu wasio wateja wako

Usipende kutoa siri za biashara yako kwa watu wasio wateja wako

CONTROLA

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2019
Posts
7,001
Reaction score
23,449
Katika vitu napataga shida ni kwenye kuchagua vichwa vya habari ya thread ninazoanzisha kwahiyo ndugu zangu tuwe tunasameheana inapotokea nimeandka kichwa cha habari halafu content inapishana hapo muwe mnanisamehe tu.

Leo bana kuna ishu moja nataka kuongea na wafanyabiashara/wajasiriamali sio kubwa ni kaishu kadogo sana lakini kanafelisha watu wengi,kanafanya watu warudishe frem,kanafanya watu wale mitaji,watu waone biashara ngumu,nk nk.

Mfano: Una duka la vipodozi au vifaa vya simu au Hardware au duka lolote Upo dukani kwako sasa hivi ametoka mteja muda si mrefu kuku uliza bei ya vitu vyako labda kaja kakuuliza dada/kaka una Fast charge ukamjibu ndio,ni bei gani? Unamtajia bei baada ya hapo anajiongelesha ongelesha kisha anakuuliza tena hivi hilo betri la simu ni sh ngapi? unamtajia,anageuka upande ule anakuuliza hivi hiyo mouse hapo sh ngapi nayo,unamtajia yani huyu mteja ndani ya dk 5 anakua kashakuuliza bei za bidhaa karibia zote unazouza dukani kwako.

akimaliza sasa mara nyingi anajibaraguza kukwambia kuwa atarudi badae kufata Fast Charge ile aliyokuuliza ya kwanzaaa,unamuitikia sawa unamkaribisha tena anaondoka,My dear kama umeshakutana na huyu mteja leo tambua leo ni moja ya siku ulizouza MECHI yani kama ni mpira uwanjani tayari ushapigwa 1-0 wanaita Moja Bila.

Halafu ubaya ni kwamba wakati unamtajia bei ulikua unamtajia bei rahisi rahisi ukiamini unamshawishi,kakuuuliza una fast charge ukamtajia bei sh 10,000 kaja kakuuliza una usb ukamtajia bei sh 4000 akaja akakuuliza una simu aina flani ukamtajia bei ndogo sana,yani katika kila alichouliza wewe ulikua unamtajia bei ndogo ndgo ili umvute mteja wako ashawishike,lakini mwisho wa siku mteja akaishia kukusifia "una bei nzuri kweliii" nitakuja badae basi kufata hiyo fast charge nimnunulie na bi mkubwa maana anashda kweli na charge.Hapo tena tunasema kama upo uwanjani ushatandikwa 2-0 yani mbili BILA.

Katika biashara unatakiwa uwe na uwezo wa kumtambua MTEJA na WINDOW SHOPPER (Kiswahili ya hiii mtanisaidia jamani) window shopper ni wale watu (siwaiti wateja) wanaokuja dukani au sehemu yako ya kazi kukuchimba na kukuchambua wewe na vitu vyako kujua bei ya vitu vyako,unauzaje,bei yako inapungua au haipungui,nk hawa ndio hao watu niliowatolea mfano huko juu.

ukiwa kwenye biashara yako ni lazima ujue huyu mtu ni mteja au ni mkusanya taarifa,watu wengi sana hukosa wateja na kukosa mauzo mazuri kwenye biashara zao kwasababu wamekua wakiuza siri za bidhaa zao kwa watu baki,mara nyingi hawa wakusanya taarifa wanakua ni wafanyabiashara kama wewe wanaotaka kufanya unachokifanya na mara nyingi wanakua wafanyabiashara wakubwa wasiokurupuka wana mitaji ambayo wako nayo makini sana wasiiipoteze ndio mana wanafanya wanachokifanya.

Huuyu mtu anapokuja dukani kwako akishajua bei zako zote utaona baada ya wiki wateja kwako wanapungua unajua kwanini? hili jamaa linaenda kufungua biashara kama yako mitaa hiyo hiyo yako na kwakua anajua bei zako zote yeye vitu vyake anauza chini kuliko wewe,ulimtajia fast charge 10000 yeye akifungua duka atauza fast charge 8000 ulimtajia simu ya nokia sh 50,000 yeye atauza simu za nokia 40,000 hivi kwanini wateja wasiende kwake?

kumbuka atakapofungua duka hatokupa taarifa kuwa kafungua wala kafungulia wapi wewe utaona tu picha day 1 mauzo yalikua LAKI utashangaa yanaporomoka yanakua 80,000 mara yanakujaa 50,000 yani biashara inaaanza kusua sua unajiuliza kwanini? inakuaje? hupati majibu kwasababu hujui kuwa vitu vyako bei ipo juuu kuna mwenzako huko anauza vitu bei ya chini kuliko wewe.

Mpaka uje ugundue tayari mwenzako kashapga faida na kashakulostisha sana miezi yote uliyokua hufanyi biashara vizuri,wateja ni watu wa ajabu sana yani bei pungufu ya sh.100 tu inamkimbiza dukani kwako anaenda kwa jirani,Hivi mnakumbuka BONITE na PEPSI bei za soda zao zilikuaga vpi? najua wote mnakumbuka bei ya soda za coca/fanta vs bei ya soda za pepsi Kila mtu ni shahidi pepsi walikua wanauza soda zao 600 bonite soda zao walikua wanauza 700,hiyo bei ilikaa hivyo kwa muda mrefu na watu wakazoea.

Pepsi akaaamua kubadili game akanyofoa sh 100 kwenye ile 600 bei ya soda ikawa 500 bwana bwana bwana nani hanywi pepsi,kila mtu kahamia pepsi BONITE walijitutumua sana lakini wapi mwisho wa siku leo hii wamekubali wenyewe wameleta bei imekua 500 soda zote ni jero saivi lakini nani chanzo cha kuuzwa soda 500 najua wote mtakubali PEPSI ndio chanzo,bonite sio kwamba walipenda kuuza fanta zao na sprite jero ila iliwabidi kwasababu wasipofanya hivyo kampuni itafungwa kwakukosa faida.

Nikirudi huku kwetu pia usikubali mtu baki akufanye ubadilishe bei ya vitu vyako weka siri kwenye bei ya vitu vyako,nimesema hapo juu ni lazima ujue tofautisha mteja na window shopper, mtu uliza uliza ukimtajia bei za dukani kwako hakikisha unataja bei kubwa kubwa yawezekana kweli una perfume OG na COPY original unaiuza 50,000 copy yake unaiuza 25,000 sasa mtu akija dukani akikuuliza bei ya perfume mwambie bei yako ni sh.50,000 usimtajie ile ya 25,000. (narudia tena usimtajie)

Kama ni mteja utamsikia akianza kulalamika "jamani mimi nimezoea kununua ile ya 25,000 kwani hiyo hauna" ukishamsikia analalamika hivi ujue aliepo mbele yako ni mteja sasa mfungukie sasa mpooze kwanza mpeti peti mwambie asijali maana ya 25k ipo na ile ya 10k ipo lakini hata ile ya 5k ipo mtoleeee zote jinafasi na mteja wako,lazima atanunua.

Kama sio mteja utamsikia akiitikia tu na kukwambia sawa ntakuja kesho au badae maana sasa hivi hajabeba hela,hatokuuliza next step wala mbadala kulingana na hela yake aliyonayo kwasababu mfukoni hana hata piiii ni muulizaji tu. (usiuuze mechi kwa sampuli hii ya raia)

Kwa hiyo ndugu zangu mjifunze kuwa wasiri wa bei ya vitu vyenu mnavyouza,acha kuropoka ropoka bei kwa watu wasio sahihi,kila siku mnasikiliza radio mnaangalia ma tv nk hivi nani amewahi kusikia tangazo la radio au tv linataja bei ya bidhaa wanayouza? NANI KASIKIA ETI??? watabwabwaja weeeee utasikia karibu OFA ya siku kuuu bei zetu ni cheeee lakini kamwe hutosikia wakiropoka bei ya vitu vyao hata siku 1.

Unajua kwanini hawataji bei? sio kwamba hawataki ujue bei zao ila hawataki kutajia watu wasio sahihi bei ya vitu vyao maana wanajua kabisa wakitaja bei yupo ngedere anaweza akafungua ofisi kama yao akauza vitu kwa bei ya chini kuliko wapo ndio maana wapo makini eneo hilo.

na wewe leo nakwambia kuwa msiri katika biashara yako acha kuropoka ropoka bei za vitu vyako,acha kutaja mahali unanunulia mizigo yako acha kuuza siri za biashara yako kaaa kimyaaa jifunze ukimya jifunze kufunga mdomo huo ukikaaa dukani tulia kimya sio kila anaeingia dukani kwako ni MTEJA wengine sio wateja ni wafanyabiashara wenye pesa mara kumi ya zako kuwa makini nao,be a man of few words like Kyle xy ukiwa kwenye biashara yako hakikisha upo makini kumjua unaeongea nae ni mteja au mkusanya data.

Kuwa makini na hao wakusanya data wanatufelisha sana,wanatufanya tuonekane hatujui biashara shenzi hao waepuke na ukiwagundua wafanyie masifa,yani mimi akiingia mtu ofisini nikakugundua ni mkusanya DATA nakwambia kitu cha laki na nusu ntakwambia nauza laki 6,bidhaaa ya elfu 10 ntakwambia nauza 50k yani kitu cha 5000 ntakwambia nakiuza 30k yani usiombe ukanikuta mimi ofisini,wewe si unataka kujua bei ya duka langu lote ntakutajia BEI hizooo hutorudia tena kuja niuliza,tena nakutajia kwa upoleee na utaratibu maana nishajua wewe ni mkusanya taarifa na siwapi nafasi watu aina hiyo kabisa.

Jamani nimemaliza sina jipya narudia tena biashara inahitaji mambo mengi sana sana ukiona biashara inakua ngumu mara nyingi shida ni wewe mwenyewe kuna mambo ukibadilika kidogo vitu vinajipa,namalizia kwakusisitiza usiri ni siri ya mafanikio katika biashara yako.
 
Sometimes usipowajibu window shoppers wanakuona unaringa na kama unaipenda bize yako inabidi u-comply
 
sometimes usipowajibu window shoppers wanakuona unaringa na kama unaipenda bize yako inabidi u-comply
Wajibu ila usiwape majibu sahihi hawatakiwi kupewa ukweli wa unachokiuza, usiache kuwajibu.
 
Mbali na kumtajia bei tuliowengi ni wavivu wa kufanya ubunifu katika biashara.
 
...ni kweli Kwenye biashara kunahitaji usiri Ila sidhani kwa style hyo ya Bei elekezi...

Mana nimejaribu kuchukulia mfano makampuni makubwa apa nchini kama Azam na Metl...afu nikajaribu kulinganisha na ulichoandka naona bado haileti maana.

Haya makampuni makubwa Siri zao zinakuwa ktk uzalishaji na ktk vitabu vyao (mapato na matumizi) Ila sio Kwenye Bei.

Kuhusu coca na pepsi hzo ni substitute goods ni kawaida kwao mmoja Bei akipanda na mwengine demand huongezeka...

So,kwa kifupi ni kwamba mfanya biashara asiogope kutangaza Bei za bidhaa zake kwa wateja wake...kwasababu Bei hutokana na gharama za bidhaa na ubora wake,so mfanya biashara anaejiamini huwa huwa haogopi kupoteza wateja kwa kuwatajia Bei sahihi.

Pia kaa ukijua mfanyabiashara mwenzangu...kuna aina ya wateja tofautitofauti,hao aliowataja mleta mada ni mojawapo ya aina ya wateja...ukiwatreat vibaya ndo umewafukuza hvyo.
Kuna aina nyingi za wateja na sifa zao so ni vizuri mfanyabiashara ukawajua.

Baadhi ya vtu vinavyoweza kuvuta au kufukuza wateja ktk biashara yako ni:-
Ubora
Uaminifu
Usafi
Bei
n.k.....
 
Wale wanaweka maspika hasa kariakoo, buguruni na manzese ??

Wanataja na Bei za bidhaa zao kbs !!!
Mathalani wauzaji wa phone accessories
 
Umeongea utopolo tu,bei nayo ni siri kwa mteja?
super market kila bidhaa inajielez n bei imebandikwa.
Maduka mbali mbali nje y nchi wanafany hivyo.

Ile nyie waganga njaa wa manzese na kariakoo ndo zenu hamna ubunifu zaidi ya kushikana uchawi,maana mnaamini hadi macho eti yanaroga,sasa mmehamia kwa wateja na windowshoppers.
 
Kwa kufanya hivyo unapoteza mkuu. Mimi ni mmoja wa wateja wanaouliza bei ya vitu madukani si chini ya vitano, tar 30 naenda kununua.
 
Mimi kabla sijanunua chochote huwa napenda kufanya window shopping kwanza.naweza ingia duka labla la vifaa vya umeme nauliza Bei za vitu mbalimbali.

Anyway wewe muuzaji ndo unauzoefu na umeeleza kutokana na uzoefu wako siwezi kutokubaliana na wewe,nimejifunza kitu japo sijaanza kufanya biashara
 
Si lazima wote tumuelewe mtoa mada! Wafanya biashara waliokutana na changamoto kama zake na wanaofanya biashara ya dizaini hiyo naamini wamemuelewa kinaga ubaga.

Binafsi kuna kitu nimejifunza hapa!
 
Kweli bana siri ni uhai wa biashara yako!!

Mtoto wa Boss wangu tulilingana umri (26 yrs) so akawa rafiki!! one day alifanya kosa kubwa sana kunituma kwenda kununua bidhaa, za ofisini kwa Babae, siku hiyo rafiki angu James alikuwa na mchuchu alikuwa Nesi,! tena hela ndogo tu faida kubwa!! yaani alinipa nusu, na nusu nyingine akabaki nayo ili hata nikikimbia na ile hela haitamsumbua atajazilishia tu pale!!

So!! kwa manunuzi yale nilofanya nikagundua Super faida inayopatikana ofisini, kumbe mishahara ya wafanya kazi wote ilikuwa ni mapato ya Masaa sita tu, na faida juu, Roho ikafanya Paaaa!!!!! kirohoni sikuwapo, baada ya mida kwani aliniona tena?

Mwezi mmoja tu hakuamini nilicho kifanya, yaani nikafungua Biashara kubwa sana kupita yake Mara tatu, lkn mbali na hapo alipo . habari zikavuma. siku nikawafuma wafanya kazi wenzangu wananiteta

''eti huyu chizi kamshahra hako kiduchu vile! vipi anajipa misifa eti anafungua biashara ataweza? ''mtu mwenyewe hana hata kitanda? mbona walikuja omba hajira!!!!

Kosa moja kubwa alilifanya mtoto wa Boss!!
 
Umeongea utopolo tu,bei nayo ni siri kwa mteja?
super market kila bidhaa inajielez n bei imebandikwa.
Maduka mbali mbali nje y nchi wanafany hivyo.

Ile nyie waganga njaa wa manzese na kariakoo ndo zenu hamna ubunifu zaidi ya kushikana uchawi,maana mnaamini hadi macho eti yanaroga,sasa mmehamia kwa wateja na windowshoppers.
Bro kama hukubaliani na mtoa mada bora ukapinga kwa point kulko ivi ulivoandika
 
...ni kweli Kwenye biashara kunahitaji usiri Ila sidhani kwa style hyo ya Bei elekezi...

Mana nimejaribu kuchukulia mfano makampuni makubwa apa nchini kama Azam na Metl...afu nikajaribu kulinganisha na ulichoandka naona bado haileti maana.

Haya makampuni makubwa Siri zao zinakuwa ktk uzalishaji na ktk vitabu vyao (mapato na matumizi) Ila sio Kwenye Bei.

Kuhusu coca na pepsi hzo ni substitute goods ni kawaida kwao mmoja Bei akipanda na mwengine demand huongezeka...

So,kwa kifupi ni kwamba mfanya biashara asiogope kutangaza Bei za bidhaa zake kwa wateja wake...kwasababu Bei hutokana na gharama za bidhaa na ubora wake,so mfanya biashara anaejiamini huwa huwa haogopi kupoteza wateja kwa kuwatajia Bei sahihi.

Pia kaa ukijua mfanyabiashara mwenzangu...kuna aina ya wateja tofautitofauti,hao aliowataja mleta mada ni mojawapo ya aina ya wateja...ukiwatreat vibaya ndo umewafukuza hvyo.
Kuna aina nyingi za wateja na sifa zao so ni vizuri mfanyabiashara ukawajua.

Baadhi ya vtu vinavyoweza kuvuta au kufukuza wateja ktk biashara yako ni:-
Ubora
Uaminifu
Usafi
Bei
n.k.....
Umejibu vyema , totally napingana na mtoa mada , mi binafs huwa sinunui kitu moja Kwa moja Kwa muuzaji nitakayemfikia ni lazima nifatilie bei kuanzia mtandaoni , mpak kwenye Duka halisi na lazima niulizie bei maduka mawili au matatatu Yule nitakayeona ana unafuu namrudia , sasa ukisema uzingue kuwaelekeza wateja bei wanazokuilizia utachemsha mapema sana na utakimbilia Kwa sangoma ..wateja wengne huwa wanatumwa na taasisi kuulizia bei Kwanza mfano miez kama mitano imepita tulienda kununua vifaa vya mziki Kwa ajili ya kanisa , tulipitia maduka kama sita hv tofaut tofaut badae tukakaa chini kuchekecha akli , tukamrudia jamaa mmoja baada ya kuzichambua taarifa zake...so hz mambo za kuuliziwa bei na wateja ni kawaida kabisa l...
 
Umejibu vyema , totally napingana na mtoa mada , mi binafs huwa sinunui kitu moja Kwa moja Kwa muuzaji nitakayemfikia ni lazima nifatilie bei kuanzia mtandaoni , mpak kwenye Duka halisi na lazima niulizie bei maduka mawili au matatatu Yule nitakayeona ana unafuu namrudia , sasa ukisema uzingue kuwaelekeza wateja bei wanazokuilizia utachemsha mapema sana na utakimbilia Kwa sangoma ..wateja wengne huwa wanatumwa na taasisi kuulizia bei Kwanza mfano miez kama mitano imepita tulienda kununua vifaa vya mziki Kwa ajili ya kanisa , tulipitia maduka kama sita hv tofaut tofaut badae tukakaa chini kuchekecha akli , tukamrudia jamaa mmoja baada ya kuzichambua taarifa zake...so hz mambo za kuuliziwa bei na wateja ni kawaida kabisa l...
Mkuu nisaidie duka la huyo jamaa nahitaji kununua vifaa vya mziki vya kanisa pia.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom