Usipike nyama kwenye pressure cooker inaweza kusababisha saratani

Usipike nyama kwenye pressure cooker inaweza kusababisha saratani

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Dr. Luka Mkeni anaeleza namna mapishi ya nyama yanavyoweza kuathiri afya yako.

Kupika nyama kwa joto kali sana, hasa inapofikia zaidi ya 220°C (428°F), kunaweza kuongeza uundwaji wa kemikali zinazoitwa Polycyclic Aromatic Hydrocarbons (PAHs). Baadhi ya PAHs zina uwezo wa kusababisha saratani, na kuathiriwa nazo mara kwa mara kumehusishwa na ongezeko la hatari ya baadhi ya saratani, ikiwemo saratani ya utumbo mpana.

Kwa upande mwingine, utafiti uliochapishwa kupitia PubMed Central (PMC) uliochunguza vyakula vilivyopikwa kwa pressure cooker ulionyesha kuwa upikaji wa kawaida wa nyumbani kwa pressure cooker haukuleta tatizo la uundwaji wa furan, kemikali ambayo imeainishwa kuwa inaweza kusababisha saratani.

Aidha, aina ya nyama yenyewe pia ni muhimu. Nyama nyekundu kama ng’ombe na nyama zilizosindikwa kama bacon na sausage zimehusishwa na ongezeko la hatari ya saratani ya utumbo mpana kwasababu ya kampaundi Kama heme iron au nitrates zilizoongezwa bila kujali tu namna zinavyopikwa. (Kwa mujibu wa Cancer Research-UK)

 
Aise sasa nimeamini sisi binadamu sehemu zakufia zipo nyingi.
 
Back
Top Bottom