Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwenye macho haambiwi tazama.......kufa hufi leo ila cha moto utakipata mkuu, utapo pata maradhi utazunguka kwa kila doctor, sikia kuumwa kwa jirani ila yakikukuta maradhi......
Huyu atakuwa Msabato ambao kwao karibu kila kinywaji kina kilevi. [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]Habari za kwenu wadau,
Sio mbaya leo nikiwashirikisha madhara yanayotokana na unywaji wa chai na kahawa,
Kuna nini kibaya kwenye CHAI na KAHAWA?:
Kwenye chai na kahawa kuna kitu kinaitwaCAFFEINA/KAFEINA.
Kafeina ni nini?:
1. Kafeina ni madawa ya kulevya kundi la ‘Stimulants drugs’.
Utashangaa. Habari ndiyo hiyo. Hii ndiyo sababu kwa mtu aliyezoea kunywa chai hii kila siku au kahawa, siku asipokunywa kichwa humuuma, ni kwa sababu amekuwa mtegemezi au teja wa kafeina.
Kafeina ni kiungo mhimu karibu katika soda zote zenye rangi nyeusi; Coca-cola, Pepsi, Sayona nyeusi, Azam cola na kadharika. Kafeina huongezwa pia katika Red bull, Malta na katika baadhi ya dawa za kupunguza maumivu mwilini.
Kwahiyo Kafeina ambayo hupatikana katika chai na kahawa ni aina mojawapo yamadawa ya kulevya.
2. Kafeina ni kikojoshi (diuretics).
Kafeina ni dawa ya kukufanya ukojowe. Ukinywa kikombe kimoja cha kinywaji chenye kafeina yaani chai au kahawa, basi muda si mrefu utaenda kukojoa vikombe viwili. Kwa sababu kafeina ni taka isiyotakiwa mwilini, mwili utafanya kila uwezalo ikibidi ujikamuwe wenyewe kupata maji ya ziada kuweza kuitoa kafeina hii uliyoinywa kwa kisingizio cha chai, kahawa au soda.
Madhara yake ni nini?, Moja; kama unakunywa kinywaji na muda si mrefu unalazimika kwenda kukitoa inamaanisha kinywaji hicho hakikutumika vema na mwili. Pili; kumbuka ulikunywa kikombe kimoja na umeenda kutoa viwili, hivyo umekopwa maji mwilini mwako na ukumbuke kuwa MAJI NI UHAI.
3. Kafeina husababisha KANSA.
Seli ndani ya mwili lazima zibaki katika kiasi kidogo cha alkalini kutoka 7.2 mpaka 7.4, wakati 7.0 ni ya kati au husemwa sifuri katika kipimo cha PH (potential hydrogen). Chini ya 7.0 ni asidi na juu ya 7.0 ni alkalini. Kafeina yenyewe ni asidi, hivyo ikiwa mtu anafanya chai au kahawa ndivyo vinywaji vyake vya kila siku basi mtu huyo lazima atakuja kupatwa na kansa katika siku za usoni kwakuwa seli za kansa huishi katika hali ya uasidi pekee na kafeina ndimo mazingira mazuri ya kuishi asidi.
Jarida moja la afya la Uingereza, ‘The British Medical Journal Lancet’, limeripoti uhusiano mkubwa uliopo baina ya utumiaji wa kahawa na kansa ya kibofu cha mkojo na kupungua kwa uzarishwaji wa mkojo.
4. Kaffeina huchangia upotevu wa madini na vitamin mhimu mwilini.
Kafeina ambayo ni kikojoshi, huyalazimisha maji kukimbia nje ya mwili kwa haraka na kuziacha seli bila muda wa kutosha kuyatumia maji hayo, maji yanapokimbia kwa haraka nje ya mwili huyakimbiza pia madini mhimu nje ya miili yetu.
5. Kaffeina husababisha kisukari.
Mwili una vyanzo 3 vya nguvu ambavyo ni Sukari, Mafuta, na Maji/Chumvi. Tumesema kaffeina ni kikojoshi, hivyo kaffeina hupelekea upotevu usio wa lazima wa maji mwilini, mwili unapokosa maji kama chanzo chake cha nguvu, moja kwa moja huhamia kuitegemea sukari kama chanzo chake cha nguvu na mwishowe kisukari lazima kitokee.
6. Uchovu sugu.
Wapenzi wengi wa chai ya rangi na kahawa mara nyingi wanapojisikia uchovu hukimbilia kikombe cha kahawa au chai. Kaffeina iliyomo katika chai au kahawa huenda kuiamsha na kuitumia nguvu iliyokuwa imehifadhiwa na mwili kwa ajili ya matendo ya dharura na kukuacha wewe ukiwa huna nguvu ya ziada kwa ajili ya kazi za dharura, matokeo yake ni mwili unakuwa upo katika hali ya msukosuko muda wote.
Utolewaji wa sukari iliyokuwa imehifadhiwa, kunapelekea mfadhaiko mkubwa kwenye mfumo wa dharura wa mwili. Unaposhitushwa kidogo tu, unakuwa na nguvu za haraka (Unahamaki) kushughurika na tatizo. Hali hii hatimaye inaweza kupelekea kukauka kwa tezi ya adreno kutakakosababisha damu chache yenye sukari (hypoglycemia), udhaifu, na kuumwa sana iwapo sukari haitachukuliwa mapema kupandisha juu damu sukari.
Kwa sababu ya biashara kuunda vyakula vyetu vyote maalumu na vinywaji vyenye radha mpya, radha nzuri na nguvu ya kutosha kwa kutumia kafeina toka katika mimea na mitishamba kama vile ginseng kuisisimua tezi ya adreno, kunasababisha Ini kutoa sukari iliyokuwa imehifadhiwa mwilini kwa ajili ya matumizi yake ya dharura.
Hakuna nguvu iliyomo kwenye kafeina auginseng. Kuna majina mengine mengi ya visisimuwaji hivi kama vile, kokwa za guru,kokwa za cola na mfalme wa yote niguarana. Mbegu za guarana zina kiasi cha kafeina mara tatu zaidi ya zile za kahawa, na hawatakiwi kuliorodhesha neno kafeina kwenye vifungashio (packages) au kontena.
Ungaunga wa guarana hutumika kutengenezea vidonge vya kupunguza uzito kwa sababu kafeina itazisambaratisha hisia za njaa, lakini hakuna mahala neno kafeina linaonekana kwenye vifungashio vya dawa hizi.
Kuna mimea, kokwa na kemikali nyingi ambazo zitaisisimua tezi ya adreno na kusababisha ini kuitoa sukari iliyokuwa imehifadhiwa au hata kuitengeneza toka tishu za mwili wenyewe ‘(gluconeogenesis)’.
Imethibitika pia kuwa kafeina imekuwa ikiingilia na kuathiri unakilishaji wa kinasaba (DNA), namna ambavyo seli mpya hutengenezwa. Kafeina inaweza kusababisha upotevu toka mwilini wa vitamini nyingi za kundi B, kundi C, zinki, potasiamu na madini mengine. Kahawa huongeza hali ya uasidi kwenye utumbo mdogo.
Kafeina inaweza kusababisha msukosuko ndani ya mwili.
Kafeina siyo kwamba tu huimaliza nguvu iliyokuwa imehifadhiwa kwenye ubongo, bali pia huzuia mfumo vimeng’enya katika kutengeneza kumbukumbu kwenye ubongo.
Kituo cha Sayansi kwa maslahi ya umma (Center for Science in Public Interest) kimewashauri kinamama wajawazito kukaa mbali na kafeina kwa kuwa tafiti zimeonesha kwamba kiasi cha kafeina kilichomo kwenye vikombe 4 vya kahawa kwa siku kinaweza kusababisha matatizo wakati wa kujifungua kama yalivyoonwa katika majaribio kwa wanyama.
‘Madawa na wewe’, kwa mjibu wa Dr. Earl Mindell, mwandishi wa kitabu; ‘Earl Mindell’s New Vitamin Bible’ (zaidi ya nakala milioni 10 zimeuzwa), anasema katika ukurasa wa 414 wa kitabu hicho kuwa ‘kafeina ni dawa yenye nguvu kubwa, uwezekano ni kuwa, hauifurahii tu kahawa au cola yako ya kila siku, bali umekuwamtegemezi au teja (addicted) wa hiyo kafeina’.
Madhara ya chai ya rangi na kahawa mwilini ni mengi sana na tatizo moja litapelekea lingine na orodha inakuwa haiishi.
Namna ya kuepuka kaffeina kwenye kahawa na chai:
Badala ya kutumia majani hayo ya chai meusi, wewe chemsha maji yako ya chai kama kawaida na unaweza kutumia vifuatavyo kukamilisha chai yako; unaweza kutumia tangawizi na kumbuka pia tangawizi ni dawa ya zaidi ya magonjwa 72 mwilini.
Kwahiyo unapoinywa chai ya tangawizi siyo tu unaepuka madhara ya kaffeina peke yake, bali pia unakuwa umekunywa dawa ya zaidi ya magonjwa 72 mwilini!. Unaweza pia kuweka mdalasini, mchaichai, kukamulia ndimu, pia unaweza kutumia mchanganyiko wa viungo vingi vya chai (spiced tea) ambavyo vinapatikana kwa wingi katika soko la Kariakoo Dar – Es – Salaam na Zanzibar
View attachment 351496
Nadhani amekurekebisha na wala siyo kukulekebishaNashukuru kwa kunilekebisha ila ...
Yapo kweli, cha msingi hata kama unapenda chai sana unaweza tumia mbadala ukaweka tangawizi, mchaichai tatizo watu wanafikiri ninawatisha lahasha ni kukumbushana tu kwamba kitu hichi madhara yake ni haya....Asante nimekalibia kijana ..ubish hauna maana .. nimeona kuna madhara kweli
Ni kweli kaka, base on how much you take tea or coffee will count on the impact....Toxic9, habari hii ina ukweli ndani yake isipokua imekua over exaggerated hadi kupoteza maana halisi ya Somo lenyewe.
Msimuliaji anaonyesha kujua Biochemistry lakini siyo kiviiile.
Everything to much is harmful, the same applies to Caffeine containing drinks. Katika dose ya kawaida caffeine ina manufaa mengi tu mazuri na ndiyo maana haijakatahaijakatazwa kama Madawa mengine ya kulevya. Ila kama ikitumika hadi kufika lethal dose (vikombe vya chai 50-100 kwa mara moja) madhara makubwa hutokea.
Kwahiyo katika unywaji wa kawaida wa chai na Kahawa hakuna madhara yoyote.
Otherwise ni vizuri watu kujua pande mbili za chai na kahawa.
Nakuuliza swali wewe pia mtu mwenye kisukari ushaona wapi anashauriwa anywe pombe..... Pombe upelekea ukaushaji wa maji mwilini(dehydration) the same to Tea, sasa maji mwilini yanapo pungua huongeza concentration ya glucose mwilini halafu insulini imesizi ku-operate what do you expect mkuuSamahani naomba kuuliza mleta mada kati ya chai, kahawa na pombe hasa bia kipi kinakojoza zaidi na kipi bora? Na ni kipo kinasababisha zaidi kisukari?
Not the case, halafu fahamu sipo hapo kumtisha mtu its not my concern, i did my part to share its not necessary to take my advice, binadamu tunatofautiana sana interms of biological factors from body immunity nk.... Penda kujifunza sana than to argue...... Nilitegemea baada ya kuona uzi huu ungeenda kufanya zaidi details research than kuniambia nawatisha..Acha vitisho miaka 80 kulikuwa na mtu mmoja yeye ugonjwa wake ilikuwa ni chai tukiwa wadogo tukambatiza jina mama chai alikuwa mpenzi sana wa chai yeye akikutembeleeni anataka chai ukienda kwake muda mwingi anakunywa chai, amefariki juzi akiwa na miaka 90+ na hajakuwa akiuguaugua
Karibu my dia, kweli tena ni swala lakuchukua tahadhari na kucheza kwa steps,Thank God vitu hvi vimenipitia mbali sana tena ghafla tu kumbe najiepushia baadhi ya maradhi!!!asante mtoa mada somo zuri!!!!
Yaani mkuu miaka ya nyuma niliathirika sana na chai na soda,we shangaa mpka ninapokula ugali na chai pmben kwa cku mara tatu namaanisha kila mlo lzma chai iwepo!!!Karibu my dia, kweli tena ni swala lakuchukua tahadhari na kucheza kwa steps,
Mimi najuwa namna soda ina madhara pia so much kemikali no fruits zinawekwa ila ni Flavour tu but tunakunywa kwa tahadhari not to apply too much soda as drink to cut off thrist
Ni kweli kabisa kila kitu atumiacho mwanadamu siku ikifika kitaml'etea madhara yote ndivyo mungu alivyopangaAhsante kwa kuueneza usabato vyema.
Ni vyema ukasoma na kuwa na uhakika na unachokizungumza hapo.
Umeongea uongo ambao hata sayansi na tafiti za sasa hazisemi hivyo.
Kingine, chai na kahawa sio sawa wala chemical compounds zake sio sawa.