Utangulizi
Ni kweli unasitahili kulaumu. Ni kweli wazazi hawakukuandalia mazingira rafiki ya kufikia mafanikio yako. Wewe siyo kama Mo Dewji aliyerejea nchini baada ya kuhitimu chuo Marekani 1998 na kuendeleza kampuni (MeTL) ya baba yake yenye mapato yanayofikia dola milioni 30 kwa wakati huo. Wewe umehitimu shule na hawana mtaji,biashara wala ajira kwa ajili yako.
Elimu uliyopewa tangu nyumbani hadi darasani ni tegemezi,haikufundishi kujitegemea. Umesoma naam wewe ni msomi ila elimu yako haina uhusiano na maisha halisi katika jamii,ulichosoma chenye uhitaji kwenye jamii hakuna ajira,unataka kujiajiri wakati kujiajiri kwenyewe hujafundishwa wala kuandaliwa tangu utoto,ikitokea umepata ajira kipato kidogo hakikidhi mahitaji yako,ukiwaza kuacha kazi mtaani kugumu,unaona bora uendelee kufanya kazi usiyoipenda. Kwa nini usilalamikie?
Serikali inasema vijana ni taifa la kesho lakini hailiandai. Inafanya mambo kurahisisha namna ya utawala wake,kurahisisha maisha yako ni jambo jingine! Inakutumia wewe ili kunufaisha watu wachache wenye mamlaka na siyo wewe usiyejulikana,utaacha kulaumu?
Ni rahisi kama nini kuhalalisha lawama kwani kila kitu ni kama umesababishiwa hivi! Lakini swali unalotakiwa kujiuliza,umezuiwa kufikiria tofauti na hali ilivyo? Watu wote waliofanikiwa hawana wazazi matajiri,siyo wote waliopewa mitaji au kurithi biashara walifanikiwa. Si wote waliopewa msaada na serikali walitoboa. Ila waliofanikiwa na wanaofanikiwa ni watu waliokubali kubadili mtazamo. Unalaumu sana kwa sababu ya mtazamo wako,ukibadili mtazamo tu kila kitu kitabadilika. Usipobadili mtazamo jiandae kulaumiwa wewe!
Kujitambua ni muhimu
Kujitambua ni kufungua kifuniko kilichoficha utu wako,hadhi yako,ubora wako na thamani halisi uliyo nayo. Ni kufufuka na kutoka ndani ya kaburi la kutojua wewe ni nani,umetoka wapi, unakwenda wapi, unatakiwa kufanya nini na kwa sababu gani. Ni kujikubali na kuamua kuishi maisha yanayoakisi thamani yako.
Moja ya changamoto kubwa zinazoikabili jamii ya kitanzania na vijana kwa ujumla ni kutojitambua. Kama tulivyoona hapo juu, mfumo wa elimu na jamii inayotuzunguka huzika thamani yako ndani ya kaburi la vyeti,ajira na utegemezi wa kifikra. Hivyo kujitambua siyo somo utakalofundishwa,bali ni somo utakaloamua kulijifunza peke yako.
Wewe ni kama nyumba kubwa,nzuri yenye mali za thamani nyingi ndani yake ikiwa na mlango uliofungwa kwa kufuri (akili) kubwa lisilofunguliwa kirahisi. Kuifungua nyumba hii si tu kuufungua mlango bali zaidi ni kulifungua kufuri (akili). Kulifungua kufuri (akili yako) ni kuufungua mlango,ni kuifungua nyumba,ni kupata kila kitu cha thamani kilicho ndani ya nyumba hii,ni Kufanikiwa.
(Picha toka mtandaoni)
Ushauri
•Gundua thamani halisi uliyo nayo. Usijione kama wakuonavyo au wakusemavyo wengine,usishangilie wala kujivunia kufanya mambo madogo usiyoridhika nayo,panga kufanya mambo makubwa hata kama akili yako haiyaamini kwa sasa! Sahau elimu yako,ufaulu wako,kushindwa kwako,vyeti vyako au kukataliwa kwako maana hivyo havihusiani na ubora au thamani ulio nao hata kidogo.
•Anza upya kutumia akili yako kufikiria. Rudia upya kuifikiria ile ndoto yako iliyokataliwa na wazazi wako,walimu,marafiki au washauri wako! Sababu ulizopewa zilikuwa sahihi? Je,bado ni sahihi? Kuna mahali pa kuboresha au unatakiwa kuiandika upya? Usitazame unakokwenda kwa macho bali kwa imani (akili). Ifikirie mara kwa mara,anza kuizungumza kwa watu unaowaamini ili iote mizizi akilini mwako na kuwa sehemu ya maisha yako. Ishikilie hadi itimie.
•Jifunze kuweka akiba. Ni wazi kuwa suala la kuweka akiba ni gumu sana kwa jamii ya kitanzania. Ukiachilia mbali matumizi yasiyo ya msingi kwa wengi,kuna suala la kuona unchopata hakitoshi kuweka akiba. Matokeo ya kutoweka akiba ni kufanya kazi miaka yote huku ukilalamika huna kitu. Kukosa akiba ni kukosa mtaji. Ni rahisi kuiona au kuiendea fursa ukiwa na mtaji kuliko ukiwa mikono mitupu. Ukiweka kidogo leo,kesho na kesho kutwa ikawa tabia yako,baada ya miaka mitano hutakuwa mlalamikaji tena. Ukianza kuweka akiba japo kidogo sana,utaanza kuwa mtu wa furaha,mwenye fikra pevu,unayetazamia mafanikio kuliko matatizo na kushindwa. Angalia kipato chako,jipangie uweke kiasi gani (angalau 10% kama huna majukumu makubwa weka hata 50%),usiiguse hiyo pesa baada ya miaka kadhaa (angalau mitano) hutajuta! Kama huna kazi ya uhakika kwa sasa,usikae kivivu! Tafuta kibarua fanya,weka akiba kwa kadri unavyolipwa, utafanikiwa hatimaye!
•Jifunze kuwa msimamizi mzuri wa mali. Linda na kuthamini kila kitu kilicho mkononi mwako. Kanuni ya umiliki inakutaka uweze kusimamia kwa ubora vitu vidogo kwanza ndipo utaweza kusimamia mambo makubwa! Kuwa mwaminifu:wahi kazini,fanya kazi bila kusimamiwa,heshimu muda wa kazi,heshimu mali isiyo yako hata kama imesahaulika; hii itakuandaa kuwa mmiliki na msimamizi bora wa kazi yako! Itakusaidia kulinda mafanikio yako.
Hitimisho
Wewe ni nyumba ya thamani. Wewe una kila kitu cha thamani unachotafuta. Wewe umejaa vitu vyenye thamani ndani yako asivyoweza kujua mtu mwingine. Ulichofanya hadi sasa ni sehemu ndogo sana katika vile ulivyo.! Ndani yako umejaa mafanikio uyatakayo ila yamefungiwa na wewe mwenyewe. Kufanikiwa kwako na kushindwa kwako ni wewe mwenyewe. Kama ilivyo mlango unategemea kufuri kufunguka ili ufunguke, mafanikio yako yamebebwa na kufungiwa na akili yako. Hutaweza katu kubadilisha chochote,kama hutafanikiwa kulifungua kufuri (akili yako). Kila kitu unachotaka kuwa,unachotamani kuwa,unachotamani kufanya au kufikia yote yamefungwa na kufuri. Lifungue kufuri uwe unachotaka.
Shukrani.

Upvote
8