Usipokuwepo, Hakuna Kilichopo!

Binafsi ninayo tafsiri ndiyo maana nathubutu kuelezea ninacho kielewa, pamoja na hayo ili kuthibitisha kile ninacho kielezea ni halisi nalazimika kuthibitisha kwa kupitia msingi na kiini cha maelezo yangu yaani Maandiko Matakatifu.

Wewe mwenzangu unathibitisha vipi kuwa hoja zako ni halisi? Ikiwa bado yale unayo yatolea hoja bado hatuwezi kuyagusa ama kuyaona dhahiri kwa macho ya kibinadamu?
 
Ndugu, ni rahisi sana kujadili tafsiri yako ya maandiko kuliko kuweka kifungu. Namna unavyotafsiri wewe yawezekana hata mchungaji wako akatafsiri tofauti kama inavyoweza kutokea kwangu. Kwa hiyo, ni muhimu kutafsiri ili nielewe kile unachokusudia.
 
Naona mnabishana kuwepo mara kutokuwepo,hebu mfafanue huko "kuwepo" ni kuwepo wapi maana mnasema tu usipokuwepo na uwepo haupo lakini haielezwi huko kuwepo ni kuwepo wapi?
 
Nisipokuwepo, au wewe usipokuwepo, hakuna jamii forums wala chochote, wala Mungu. Kabla ya kuwepo kwako, ulikuwa na kumbukumbu yoyote ya kuwepo kwa chochote? Hapana. Kwa hiyo hakuna kilichokuwepo hadi ulipokiwepo, siyo?
Usipokuwepo wapi mkuu hebu fafanua?
 
Mungu alikuwepo kabla na ataendelea kuwepo hata kama binadamu na vibe vote hawata kuwepo.
 
Tupo pamoja Mkuu ktk fikirishi hii KUBWA!

NB: Mungu alimuumba Binadamu ili amnyenyekee na kumtukuza. Je,asingekuwepo Binadamu ni nani angemnyenyekea na kumtukuza Mungu?
Jibu linakuja ili Mungu awepo ni lazima Binadamu awepo.
HITIMISHO: ili uwepo uwepo ni lazima wewe uwepo.

Nawasilisha,
Asanteni.
 
@Oltung'anyi

Unafanya makosa kubwa hapa, your premise is completely wrong! Kuna mwana falsafa mmoja aliwahi kujikwaa kwenye kisiki kwa sababu alikuwa hajakiona! Baada ya kujikwaa akagundua kuwa kumbe VITU HUWA VINAKUWEPO BILA KUJALI KAMA WEWE UNAJUA KUWA VIPO. Kwa mfano, babu wa babu yako anaweza kuwa alikuwa hajui kuwa Ulaya ipo, je ni kweli kwamba Ulaya haipo? Material things exist irrespective of the knowledge of the knower. Nikuulize swali jingine, kwa mfano wewe ulipokuwa bado haujazaliwa, maana yake ni kwamba hukuwepo. Je mama aliyekuzaa naye hakuwepo wakati huo ambao wewe ulikuwa haupo? Kama alikuwepo, je ulikuwa unajua kuwa alikuwepo?
 
Nimekuelewa
 
Asante ndugu kwa maoni yako. Kama Mwanafalsafa huyo asingekuwepo, ni dhahiri kuwa asingejikwaa na kwake kusingalikaa kutokea kwa kitu kinachoitwa kisiki. Hali kadhalika kwa Babu, kama sipo, hakuna kitu kinachoitwa babu. Hakuna babu wa mtu asiyekuwepo. Lazima uwepo ili babu awepo (hata kama hayupo tena, angalao utafahamu alikuwepo babu), lakini wewe usipokuwepo, babu hawezi kuwepo hata kama bado yupo.

Unazungumzia mama, unamwita mama kwa kuwa upo, siyo? Hakuna namna unaweza kumwita mama usipokuwepo. Kwa hiyo, ninajua kuwa yupo, na ninamwita mama kwa kuwa nipo, nisipokuwepo, naye hayupo na hatakaa kuwepo hadi siku nitakapokuwepo.
 
Mungu alikuwepo kabla na ataendelea kuwepo hata kama binadamu na vibe vote hawata kuwepo.
Hali hii ya kuona kuwa Mungu ataendelea kuwepo ipo kwa kuwa wewe upo. Usipokuwepo, hakika hakuna kitakachokuwepo. Unaweza kuwaza kuwa wapo watakaokuwakilisha kuona kuwa Mungu yupo, ila ili ujue kuwa wapo wanaokuwakilisha na Mungu anaendelea kuwepo, lazima uwepo.
 
kwahyo tukikunyonga leo ukifa na mungu anakua hayupo si ndio

Usininyonge bhana! Ndio maana yake mkuu, sijui kama ulitambua kuwa Mungu yupo kabla ya wewe kuwepo. Unaweza kutupa uzoefu mkuu.
 
Bado ubongo wako una njaa upe chakula ili ufikiri zaidi haiwezekan usipokuwepo na Mungu hayupo ninachojua Hata Kama haupo Mungu yupo
 
Bado ubongo wako una njaa upe chakula ili ufikiri zaidi haiwezekan usipokuwepo na Mungu hayupo ninachojua Hata Kama haupo Mungu yupo

Haya maoni yako yanawezekana kwa kuwa wewe upo. Kwa hiyo, usipokuwepo, siyo haya maoni wala Mungu unayemjengea uwepo ataendelea kuwepo.
 
mkuu naona jamaa kajtahidi kukusuport ila umemkataa
ye kaja kimungumungu mi huko sipo kbs endapo yote yanaweza kushabiina lkn ni vitu 2 tofauti,sipendi unafki bure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…