Usipokuwepo, Hakuna Kilichopo!

Baada ya kifo changu, hakuna kitakachokuwepo, hata mawazo yangu.

Kuna siku ambayo sitakuwepo kama mabavyo sikuwepo, je unaweza kuelezea katika hali hii, ki kipi kitakuwepo kwa upande wangu?
Huo uelewa wa baada ya kifo chako wewe umeutoa wapi? unawezaje kujua mambo ya baada ya kifo hali ya kuwa upo hai na hujawahi kufa?

Na ndiyo maana nakwambia wewe unapingana na uhalisia kwa mambo ya kufikirika .
 
Jinga kabisa wew . Unafikiri hiyo suruali ulovaa iliumbwa kama wewe ulivoumbwa?
Hio suruali lilikuwa wazo LA mtu hapo kabla na huyo mtu hayupo tena lakini suruali zipo

Hahaha, hakika unanifurahisha ndugu. Unaweza kuamini ati pamoja na wazo lake hili zuri sana lakini kwake hakuna kitu kama suruali wala wazo la suruali kwa kuwa tu hayupo? Yaani kwake, hakuna kitu kilichopo kabisa. Wakati mwingine unaweza kuwaza ni kwa nini ulimwengu hauna huruma kwa kiasi hiki.
 
How can my imaginary house exist without my existence? Hoja ndio ipo hapa, kwamba vitu vipo kwa kuwa mimi nipo. Nisipokuwepo, hakuna kilichopo.
Uwepo wako haufanyi vitu viwepo ila uwepo wako ndiyo umekufanya uweze kushuhudia uwepo wa vitu,hivyo wote tunaishuhudia dunia hii kwa sababu tupo na asiyekuwepo ameshindwa kushudia ila kiuhalisia dunia ipo hata ameshindwa kuishuhudia.
 
Hapa tunaongea mimi na wewe ....je wewe hutambui kuwa suruali ulovaa ni wazo LA mtu ambaye sasa ni marehemu
 
Hapa tunaongea mimi na wewe ....je wewe hutambui kuwa suruali ulovaa ni wazo LA mtu ambaye sasa ni marehemu

Ninatambua kwa kuwa nipo. Hebu tumfikirie huyu aliyeleta wazo la suruali ikiwa anatambua kuwa wazo lake kuwa lipo.
 
Uwepo wako haufanyi vitu viwepo ila uwepo wako ndiyo umekufanya uweze kushuhudia uwepo wa vitu,hivyo wote tunaishuhudia dunia hii kwa sababu tupo na asiyekuwepo ameshindwa kushudia ila kiuhalisia dunia ipo hata ameshindwa kuishuhudia.
Mkuu, siyo kwamba uwepo wako ndio unaokuwezesha kushuhudia uwepo wa vitu na watu? Kwamba, kama haupo, huwezi kupata fursa ya kushuhudia chochote na kwa maana hiyo, kwako hakuna kilichopo kabisa?
 
Huo uelewa wa baada ya kifo chako wewe umeutoa wapi? unawezaje kujua mambo ya baada ya kifo hali ya kuwa upo hai na hujawahi kufa?

Na ndiyo maana nakwambia wewe unapingana na uhalisia kwa mambo ya kufikirika .

Kutokuwepo kwa kabla na baada ya kuwepo kunafanana mkuu, ni kutokuwepo tu.
 
Kwa namna ambayo wewe huwezi kuielewa. Kwasababu wewe unatambua kwa milango yako ya fahamu tu. Kitu imani hauna

Hata kama wewe una imani lakini ili imani yako iwe na maana na uweze kuitumia, lazima uwepo.
 
Oltunganyi wewe na wafu hamna tofauti

hahahaha, basi naona unatumia vyema maarifa uliyoyapata. Kwa wafu, kwao hakuna chochote, na wala hakuna kilichokaa kuwepo kwao, siyo mawazo yao mazuri, siyo ufahari wao, siyo kwenda kwao Ughaibuni, hakuna chochote. Kwa hiyo ndugu, vyovyote iwavyo, lazima uwepo ili hivyo unavyohesabu vipo, viendee kuwepo au ulimwengu na mambo yake uendelee kuwepo. Nafikiri ndio maana tunaweka juhudi kubwa sana ya kuwekeza kwenye kuhakikisha kila mmoja wetu anaendelea kuwepo. Kuwepo kuna thamani kubwa sana.
 
Death is inevitable brother. Separation of the soul and body must occur but the soul is deathless and will keep on living. Believe it or not you will keep on existing even after your death
 
Mkuu, siyo kwamba uwepo wako ndio unaokuwezesha kushuhudia uwepo wa vitu na watu? Kwamba, kama haupo, huwezi kupata fursa ya kushuhudia chochote na kwa maana hiyo, kwako hakuna kilichopo kabisa?
Hapana,kama kitu kipo kipo tu na kama hakuna ni hakuna tu haijalishi umepata fursa au umekosa.

Halafu hili si suala la mtu binafsi,tuchukulie mfano mtu kafa(hakuna uwepo wake duniani) ina maana ni kweli sie hatupo kwa sababu tu ya kukosekana uwepo wake?

Hapana,ukweli ni sie tupo ila yeye amekosa fursa ya kushuhudia hilo.
Mtu akisema kwake yeye rais wa Tz ni Lowassa basi hiyo ni kwake yeye ila ukweli rais wa Tz ni Magufuli huo ndiyo ukweli.
 
Kutokuwepo kwa kabla na baada ya kuwepo kunafanana mkuu, ni kutokuwepo tu.
Bado hujaeleza unajuaje?

Hakuna hata anayekumbuka au kuelewa maisha ya tumboni kwa mama yake yalikuwaje,ila wewe unataka kutueleza mambo ya kabla ya kuwa tumboni kabisa sijui umeyajuaje?

Tueleze umejuaje?
 
Tuna uzoefu wa kutokuwa na uzoefu wowote wa kabla ya kuwepo. Hivyo,kabla ya kuwepo kwangu na kwako, hatuna namna tunaweza kutoa ushahidi wa kuwepo kwa dunia na vitu vingine. Hatukuwepo, kwa hiyo tunaweza kuelezea hali ya kutokuwepo lakini tukiwepo.

Hivi? Tupo kwa kuwa dunia ipo au dunia ipo kwa kuwa tupo?. Kabla ya kuwepo kwetu dunia ililikuwepo? Unaweza kuwa na ushahidi wowote wa kabla ya wewe kuwepo?
 
Amekosa fursa kwa kuwa hayupo na hakuna namna anaweza kushuhudia uwepo au hali ya kutokuwepo kwako. Kwa hiyo, kwake yeye, hakuna chochote na hakuna kilichowahi kuwepo kwake labda hadi atakapokuwepo tena.
 
Ndiyo nimekuuliza ni kweli sie hatupo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…