Usipokuwepo, Hakuna Kilichopo!

Usipokuwepo, Hakuna Kilichopo!

Tuna uzoefu wa kutokuwa na uzoefu wowote wa kabla ya kuwepo. Hivyo,kabla ya kuwepo kwangu na kwako, hatuna namna tunaweza kutoa ushahidi wa kuwepo kwa dunia na vitu vingine. Hatukuwepo, kwa hiyo tunaweza kuelezea hali ya kutokuwepo lakini tukiwepo.

Hivi? Tupo kwa kuwa dunia ipo au dunia ipo kwa kuwa tupo?. Kabla ya kuwepo kwetu dunia ililikuwepo? Unaweza kuwa na ushahidi wowote wa kabla ya wewe kuwepo?
Kutokuwa na uzowefu ni uzowefu? na kutokuwa na uzowefu ndiyo uzowefu wa aina gani mkuu?
 
Ndiyo nimekuuliza ni kweli sie hatupo?

Kwa asiyekuwepo, sisi na kila kitu hakipo na hatutakaa tuwepo wala hakuna kitu kitakachokaa kuwepo. Unaweza kusema kuwa dunia inafikia mwisho wake siku ambayo mtu anapoteza uwepo. Labda lugha hii inaweza kueleweka.
 
"Usipokuwepo" hili ni neno linaloelezea nafsi ya pili umoja wakati "Kilichokuwepo" ni neno linaloelezea dhana ya mwili, yaani uhalisia wa kile kinachoonekana kama matokeo ya uwepo wa mwili na nafsi (mwanadamu).

Kwahiyo, tafakuri ya mtoa mada inajielekeza zaidi katika uzoefu wa mwili kama uhalisia wenyewe, yaani uwepo wake (yeye au wao) dunia juu ya hivyo vilivyopo pasipo kuhusisha ozoefu wa nafsi.

Katika maana nyingine mtoa mada unauona uwepo na vilivyopo baada tu yeye kuwepo kutokana na kwamba yeye anajenga mukutadha wa ozoefu wa mwili pekee na kutupilia mbali nafsi.

Hivyo basi, "Tusipokuwepo Hakuna Kilichopo" kama mtoa mada anavyodai; kitawezekana kusemwa hivyo ikiwa tu madai hayo yanahusisha tu mwili pasipo nafsi.
 
Acha ujinga ww
Hv unaanzaje kumtaja Almighty lord kimchezo mchezo kias hicho..?
Jiangalie ww..
 
Unaona sasa hapo? Tofauti ya mie na wewe ni kwamba mimi nazungumza vitu ambavyo naviexperience kutokana na uwepo wangu hapa duniani na kumbuka kuwa unaposema mtu kuwepo au kutowepo tunakusudia uwepo wa hapa duniani,sasa wewe unazungumzia vitu vya kufikirika tu.

Kwa kuwa tunazungumzia kuwepo hapa duniani na mie kuwepo kwangu duniani najua kabisa mtu ambaye bado hajazaliwa(hayupo) hana athari yeyote kwa huku duniani,na mtu akifa huiacha dunia uwepo wake unakuwa umeondoka hapa duniani.

Sasa ni ajabu kuacha mambo ambayo unayashuhudia na kutaka kutumia mambo ya kufikirika,halafu pia uthibitisho haufanyi jambo liwepo bali uthibitisho unatoa uhakika wa kuwepo hilo jambo ni suala la kujiridhisha.

Kwahiyo mie kabla ya kuja duniani dunia ilikuwepo(nimetumia uzowefu wangu wa uwepo wa hapa duniani) hata kama nilikuwa sijui na nasingeweza kuthibitisha hilo kuwa kuna dunia.
Kabla ya kuzaliwa ulijuwa kama kuna uwepo wa dunia?au baada ya kuzaliwa/kuwepo ndo ukajuwa kuna dunia tuanze hapo?
 
Ndio mkuu, uzoefu tulionao ni kuwa hatukuwepo na hatukuweza kutambua uwepo hadi tulipokuwepo. (Joke: Ikiwa umesahau ufunguo mahali, si yawezekana ulichokumbuka ni kusahau ufunguo mkuu? Kwa hiyo yawezekana pia kutokuwa na uzoefu nao ukawa ni uzoefu)
 
Hili ni moja ya maswali ambayo bila shaka nimekuwa nikikuuliza ama kulitolea ufafanuzi na hapa ndipo palipo na suala la uzoefu wa kutokuwepo na umuhimu wa kuwepo.

Dunia nimeifahamu baada ya kuzaliwa(kuwepo). Nilitambua uwepo wa dunia baada ya kuwepo. Kabla ya kuwepo, hakukuwa na kitu dunia na kama si kuwepo,kusingalikaa kutokea kitu dunia. Nafikiri hadi hapa, utakuwa umenielewa. Kuwepo kumefanya kila kitu kikawepo, siyo dunia tu, hadi Mungu.
 
"Usipokuwepo" hili ni neno linaloelezea nafsi ya pili umoja wakati "Kilichokuwepo" ni neno linaloelezea dhana ya mwili, yaani uhalisia wa kile kinachoonekana kama matokeo ya uwepo wa mwili na nafsi (mwanadamu).

Kwahiyo, tafakuri ya mtoa mada inajielekeza zaidi katika uzoefu wa mwili kama uhalisia wenyewe, yaani uwepo wake (yeye au wao) dunia juu ya hivyo vilivyopo pasipo kuhusisha ozoefu wa nafsi.

Katika maana nyingine mtoa mada unauona uwepo na vilivyopo baada tu yeye kuwepo kutokana na kwamba yeye anajenga mukutadha wa ozoefu wa mwili pekee na kutupilia mbali nafsi.

Hivyo basi, "Tusipokuwepo Hakuna Kilichopo" kama mtoa mada anavyodai; kitawezekana kusemwa hivyo ikiwa tu madai hayo yanahusisha tu mwili pasipo nafsi.
Inawezekana mkuu. Ningependa kufahamu ikiwa nafsi ingehusishwa, pengine hoja hii ingeathirika kwa namna gani?
 
Kwa asiyekuwepo, sisi na kila kitu hakipo na hatutakaa tuwepo wala hakuna kitu kitakachokaa kuwepo. Unaweza kusema kuwa dunia inafikia mwisho wake siku ambayo mtu anapoteza uwepo. Labda lugha hii inaweza kueleweka.
Nimekwambia mtu anaweza kusema kuwa kwake yeye rais wa Tanzania ni Lowassa ila hiyo ni kwake yeye tu,kiuhalisia rais wa Tanzania ni Magufuli.

Kwahiyo kama kwa asiyekuwepo kwake yeye sie pia hatupo basi hiyo ni kwake yeye tu,ila sio kweli kuwa sie hatupo ni kama ambavyo mtu anayesema kwake yeye rais wa Tanzania ni lowassa.

Na ndiyo maana nikakuuliza je ni kweli sie hatupo?
 
Kabla ya kuzaliwa ulijuwa kama kuna uwepo wa dunia?au baada ya kuzaliwa/kuwepo ndo ukajuwa kuna dunia tuanze hapo?
Kwanza unapozungumzia kabla ya mimi kuzaliwa unakusudia wakati nikiwa tumboni kwa mama ama unakusudia vp?
 
Ndio mkuu, uzoefu tulionao ni kuwa hatukuwepo na hatukuweza kutambua uwepo hadi tulipokuwepo. (Joke: Ikiwa umesahau ufunguo mahali, si yawezekana ulichokumbuka ni kusahau ufunguo mkuu? Kwa hiyo yawezekana pia kutokuwa na uzoefu nao ukawa ni uzoefu)
Hivi mtu aliyepoteza fahamu anaweza kuielezea hali ya kupoteza fahamu ikoje? yani wakati amepoteza fahamu kuna ambacho anaweza kukieleza ambacho kilikuwa kikiendelea wakati hana fahamu?

Mtu aliyesahau funguo katika kipindi chote hicho anaweza akawa anafikiri kuwa funguo anayo kumbe hana hadi pale atakapokuja kugundua kuwa kumbe hana funguo,hicho kitendo ndiyo kinaitwa kusahau.
 
Hili ni moja ya maswali ambayo bila shaka nimekuwa nikikuuliza ama kulitolea ufafanuzi na hapa ndipo palipo na suala la uzoefu wa kutokuwepo na umuhimu wa kuwepo.

Dunia nimeifahamu baada ya kuzaliwa(kuwepo). Nilitambua uwepo wa dunia baada ya kuwepo. Kabla ya kuwepo, hakukuwa na kitu dunia na kama si kuwepo,kusingalikaa kutokea kitu dunia. Nafikiri hadi hapa, utakuwa umenielewa. Kuwepo kumefanya kila kitu kikawepo, siyo dunia tu, hadi Mungu.
Ni sawa na kuwepo bomba kubwa ambalo unaweza kupita kutokea upande wa pili,ila ndani ya hilo bomba kuna kiza kkikubwa kiasi cha kushindwa kuona chochote wakati ukiwa unapita kwenye bomba hilo. Lakini baada ya kufanikiwa kupita na kutokea upande wa pili kutokea kwenye bomba unaona vitu.

Sasa huwezi kusema kuwa hakukuwa na chochote kabla ya wewe kutokea upande huo wa pili kisa tu wakati unapita kwenye hilo bomba hukuwa unaona chochote.
 
Baada ya kifo changu, hakuna kitakachokuwepo, hata mawazo yangu.

Kuna siku ambayo sitakuwepo kama mabavyo sikuwepo, je unaweza kuelezea katika hali hii, ki kipi kitakuwepo kwa upande wangu?
Sasa ni ujinga kuwa na mawazo kuwa wewe usikuwepo na vingne vinavyohusiana na wewe havitakuwepo! We should probably stop arguing aboout this, it appears there is that wide gap of knowledge between us!
 
Nimekwambia mtu anaweza kusema kuwa kwake yeye rais wa Tanzania ni Lowassa ila hiyo ni kwake yeye tu,kiuhalisia rais wa Tanzania ni Magufuli.

Kwahiyo kama kwa asiyekuwepo kwake yeye sie pia hatupo basi hiyo ni kwake yeye tu,ila sio kweli kuwa sie hatupo ni kama ambavyo mtu anayesema kwake yeye rais wa Tanzania ni lowassa.

Na ndiyo maana nikakuuliza je ni kweli sie hatupo?
Mimi na wewe tupo kwa kuwa tupo. Sasa hivi mimi nisipokuwepo, wewe haupo kabisa na wala hukuwahi kutokea, labda siku nikiwepo tena, jambo ambalo si rahisi. Kwa hiyo, mimi nisipokuwepo, wewe hukuwahi kuwepo na hutakaa kuwepo.
 
Nimekwambia mtu anaweza kusema kuwa kwake yeye rais wa Tanzania ni Lowassa ila hiyo ni kwake yeye tu,kiuhalisia rais wa Tanzania ni Magufuli.

Kwahiyo kama kwa asiyekuwepo kwake yeye sie pia hatupo basi hiyo ni kwake yeye tu,ila sio kweli kuwa sie hatupo ni kama ambavyo mtu anayesema kwake yeye rais wa Tanzania ni lowassa.

Na ndiyo maana nikakuuliza je ni kweli sie hatupo?
Kumbuka pia mada inasema, usipokuwepo,hakuna kilichopo.Kuhusu mfano wa Rais, mtu hawezi kujisemea kuwa Rais wake ni fulani halafu akawa Rais wa wote. Ninakubali.

Ila, mimi leo hii kama sipo, ninawezaje kujua kama wewe upo? Ama dunia ipo? Kumbuka kuna wakati sikuwepo na sina kumbukumbu yoyote ya kushuhudia uwepo wakati wa kutokuwepo kwangu. Kwa hiyo, kimsingi, kabla ya kuwepo, hakukuwa na chochote, hadi nilipokuwepo
 
Sasa ni ujinga kuwa na mawazo kuwa wewe usikuwepo na vingne vinavyohusiana na wewe havitakuwepo! We should probably stop arguing aboout this, it appears there is that wide gap of knowledge between us!

Ndugu, wewe leo usipokuwepo kuna namna unaweza kusema ama kuwa na ufahamu wa kuwa maisha yanaendelea au yalishakoma?
 
Ni sawa na kuwepo bomba kubwa ambalo unaweza kupita kutokea upande wa pili,ila ndani ya hilo bomba kuna kiza kkikubwa kiasi cha kushindwa kuona chochote wakati ukiwa unapita kwenye bomba hilo. Lakini baada ya kufanikiwa kupita na kutokea upande wa pili kutokea kwenye bomba unaona vitu.

Sasa huwezi kusema kuwa hakukuwa na chochote kabla ya wewe kutokea upande huo wa pili kisa tu wakati unapita kwenye hilo bomba hukuwa unaona chochote.

Sio kwamba ulikuwa huoni, ulikuwa unaona giza. Hebu fikiria pia kuwa mbali na kuona giza, lakini baada ya kutokea upande wa pili uone vitu fulani ambavyo vingekuwepo. Hebu fikiria kama kwa bahati mbaya ukapoteza maisha ndani ya lile bomba, unaweza kuniambia nje ya bomba kutakuwa na vitu gani ndugu?
 
Back
Top Bottom