Mtumaini Mungu
JF-Expert Member
- Aug 3, 2021
- 879
- 1,084
Habari ewe mwanadamu.
Ninamshukuru Mungu kwaajili yako, pole pia kama upo katika magumu yoyote kwa fikra na macho ya kibinaadamu.
Moja kwa moja niende kwenye kusudi la kuanzisha nyuzi hii ambayo naamini endapo utaisoma vyema na kuitendea kazi kazi basi utayaona Mabadiliko kwenye maisha yako.
Hapa ulimwenguni kuna mambo mengi sana ambayo kwa ujumla wake yanaendeshwa na nguvu ya IMANI, nguvu hii kiimani imegawanyika katika sehemu kubwa mbili, Mosi nguvu ya nuru (Upande wa Mungu) na Pili nguvu ya giza (Upande wa shetani). Yeyote awaye mwanadamu ana Uhuru wa kuchagua upande atakao, lakini Mimi leo hi nitakuelekeza namna unavyoweza kufanya Mabadiliko ya kudumu kwenye maisha yako na ya wengine kwa kuifuata nguvu ya nuru.
Licha ya mwanadamu kuwa na Uhuru wa kuchagua upande wa kuutumikia, hakuna mwanadamu awezaye kuchagua kuzitumikia pande zote mbili, kimwili unaweza ukaamua kuchagua upande wa nuru lakini kiroho ukawa unatumia upande wa giza kufanikisha mambo yako (Hapa ni wazi wewe Huna nafasi kwa Mungu, ila kwa shetani umepewa cheo kikubwa). Ili uutumikie upande wa Nuru, yakupasa kufanya maamuzi lakini ili uutumikie upande wa giza bila hata maamuzi yako unaweza.
Mungu hupenda watu wote Wamjue na Kumtumikia yeye lakini Hawalazimishi, shetani hufanya kila awezalo (anakulazimisha) utumikie yeye. Hivyo Basi kwakua Mungu Hamlazimishi mtu inakupasa wewe mwanadamu kuwa tayari, kwa moyo wa dhati kuamua Kumtumikia yeye, na endapo utaamua toka ndani yako nikuhakikishie Mungu yupo naye Huonekana na Kuwajibu wote Wamtafutao.
Shetani kikawaida hunyemelea sana wale ambao hawajafanya maamuzi ya kwenda kwenye nuru, huwavuta kwake kwa vitu mbalimbali, anasa za maisha, itikadi na misimamo, uzinzi, bidhaa za matumizi n.k Lakini mtu anapofanya maamuzi ya Kumtumikia Mungu, Basi Mungu humlinda kusudi shetani asiweze kumshurutisha mtu na kumtumikisha huyo kupitia baadhi ya mambo tajwa hapo juu.
Je, Ninawezaje Kumtumikia Mungu?
Mungu yupo tayari kwaajili ya wote Wamtafutao, hivyo hatua ya Kwanza yakupasa kuazimia toka ndani ya nafsi yako kuwa "Nitamtafuta na Kumtumikia Mungu" baada ya hapo fanya toba, Muombe Mungu akusamehe makosa yako, haijalishi umekua mzinzi, mlevi, mwizi, muuaji, au hata mchawi kwa muda gani na umefanya mabaya mangapi punde tu utakapo amua kwa dhati kumrudia Mungu, basi atakusamehe na Kukukaribisha nyumbani mwake. (Toba sio kwaajili ya dini, Bali toba ni kumpa Mungu nafasi ya kuingilia kati matatizo yako na kujenga uhusiano binafsi na yeye).
Ukishafanya toba, unatakiwa kupiga hatua sasa kwa kutoyarudia yale ambayo yalikuzuia Kumtumikia Mungu, Kama ni ulevi jizuie usiguse wala kutumia vilevi, kama ni uzinzi jitahidi basi kujiweka mbali na vile vichagizo vilivyokuwa vinakuhamasisha kuzini, na kama ni uchawi choma moto kila zana (Kama unaogopa peleka sehemu unapoabudia kulingana na dini yako, na kama huna pa kuabudia lakini umeeazimia kuacha basi omba msaada kwa kiongozi yoyote wa dini yoyote aliye karibu nawe).
Baada ya kuweka jitihada za kutorudia tena, Sasa jikite kwenye kutenda mambo mema na ya Kumpendeza Mungu, Mtumaini na Kumtegemea yeye katika kila Jambo, saidia wasiojiweza kila unapoweza/wiwa kufanya hivyo, Ongea na Mungu wako kwa swala/sala kila saa kila wakati.
Kwa kufanya hayo basi utakuwa umepiga hatua, umemkimbilia na Kumtumikia Mungu, kinyume na hapo shetani yupo karibu yako na niamini Mimi lazima atakutumikisha.
Je, shetani awezaje kumtumikisha mtu?
Shetani ndiye mfalme wa ulimwengu wa giza, yeye ana mawakala wengi sana (ambao tunaishi nao, tunafanya nao kazi, na hata kuwa nao katika mahusiano) lakini si rahisi kuwatambua, kwakua wale wanaojitambua kuwa ni mawakala wa shetani hujificha wasijulikane, na wale wasiojitambua wao hutumikishwa bila ya kujijua. Shetani huwatumikisha watu kwa kuwaweka kwenye vifungo vizito, vifungo hivi huwa ni tabia/mambo ambayo humfanya mtu akae mbali na Mungu.. mfano, shetani humtumikisha mtu kwa kumuweka kwenye kifungo cha ulevi, unakuta mtu ana kazi nzuri yenye kumpa kipato kizuri lakini Hana maendeleo, kwanini pesa yote anaimalizia kwenye vilevi, wengine huwafunga kwenye vifungo vya uzinzi, mda wa adhana ndio kwanza yupo gesti na mke/mume wa mtu, jumapili watu wanatoka kanisani misa ya kwanza yeye ndiyo anatoka gesti, hivyo ni baadhi ya vifungo ambavyo shetani huwafunga watu.
Soma kisa kifuatacho kiufupi, utaona namna shetani anakimbilia na kuwatumikisha watu ambao hawana msimamo thabiti wa kumkimbilia na Kumtumikia Mungu.
Kulikuwa na kijana mmoja, alikuwa ni kiongozi wa kwaya katika kanisa fulani, Mungu aliweka kipaji halisi cha uimbaji ndani ya huyu kijana, akampa na uwezo wa kutambua na kutumia kile kipawa chake.. Baada ya muda mfupi tu wa yule kijana kuiongoza ile kwaya basi kwaya ile ikapata umaarufu mkubwa sana ikaanza kurekodi nyimbo na video zao, ikaanza kupata mialiko ya kuuudumu katika majukwaa na mikesha mbalimbali ya kusifu na kuabudu.. sifa zikaanza kumwagika kichwani mwa yule kijana, shetani naye alivyo na hila akatumia mlango uleule wa sifa naye kuleta sifa zake ili kumuondoa yule kijana kwenye uwepo wa Mungu, basi kijana akaanza kujiona kuwa hayupo kama yeye, kiburi kikaanza kuinuka, majivuno yakaanza kumea na kustawi, tamaa nazo zikamuwaka.
Shetani hakuishia hapo, akatuma wakala wake kwenda kumpotosha yule kijana, shetani alimtuma mmoja ya wake za wazee wa kanisa kwenda kuangamiza huduma ya yule kijana, vishawishi vilianza taratibu, mwisho wa siku wakajikuta wakitenda dhambi ya uzinzi kwa Siri, ila Kwa kuwa Mungu ni mMwaminifu alituma ujumbe kwa yule kijana, kijana akapuuza akaendelea na tabia ya uzinzi, waswahili husema za mwizi arobaini, baada ya kuonywa na kufurahi sana katika zile 39 ilifika ya arobaini ambao juu ya kitanda walifumaniwa, kitendo cha kufumaniwa kilibadilisha kabisa upepo wa maisha wa yule kijana, licha ya kufumaniwa na kusamehewa lakini shetani akaweka moyo mgumu ndani yule kijana, akashindwa kujisamehe, mawazo yalipomjaa kichwani, shetani akapata nafasi nyingine tena akamvuta katika ulevi akimdanganya kuwa ataondoa mawazo lakini kumbe ni vifungo juu ya vifungo.. shetani hana huruma, yupo kazini jamani mpingeni kwa nguvu zenu zote na akili zenu zote na roho zenu.
Endapo shetani huwatumikisha walio upande wa Mungu wewe nani asiweze kukutumikisha? Jitafakari leo na umrudie Mungu wako yeye pekee ndiye awezaye kuyabadili maisha yako kikamilifu, kimwili, kiroho, kiakili.
Asante, niko hapa kusikiliza na kujibu maswali kutoka kwenu.

Upvote
7