chama mpangala
JF-Expert Member
- Sep 3, 2015
- 549
- 841
Tuwafundishe watoto wetu kazi kuanzia nyumbani mpaka shuleni. Tuwalee watoto wetu kama binadamu na siyo kama mifugo.
Zamani shamba la mwalimu lililimwa na wanafunzi, kuni za mwalimu zililetwa na wanafunzi na maji alichotewa na wanafunzi.
Mwanafunzi alijisikia fahari kutumwa na mwalimu wake, tuligombania kwenda kuchota maji ya mwalimu.
Mtoto akimaliza shule alijua kazi na alipenda kazi. Siku hizi mwalimu akimtuma kazi mtoto ni kesi kubwa. Anaweza kufukuzwa kazi. Akimchapa ndiyo hatari.
*Matokeo yake? Watoto wetu hawana kazi, wapowapo tu na wamekaa legelege, ni kula na kuangalia katuni. Hawana kazi za kuwatoa jasho. Hata maua nyumbani hawawezi kumwagilia. Nguo wanafuliwa. Wanaogeshwa na mafuta wanapakwa.
Anko Kennedy anasema *wazazi wengi tumepoteza sifa ya malezi kwa watoto wetu. Tumebaki na sifa ya ufugaji wa watoto. Wengi ni wafuga watoto na siyo walezi! Tunaandaa taifa la wagonjwa, wagombania Marathi na madalala wa mali tutakazoacha. Kazi ni tiba ya mwili kutokana na magonjwa ya kutokutokwa jasho.
Sasa hivi watoto wengi wanaumwa magonjwa ya wazee. Wanaumwa vifua, wanaumwa miguu, wanaumwa macho, wanatumia miwani, hawaoni vizuri, wengine mafua hayaponi, vikohozi haviponi, mtoto akinyeshewa na mvua analazwa. Akipigwa baridi hamlali. Akishinda njaa anakufa!
Unajua kwa nini? Hatuwashughulishi! Tunawalemaza sana.
Tuwapeni kazi ndogondogo watoto wetu. Zitawajenga kiafya na kiakili.
An idle mind is a devil’s workshop. Akili iliyolala ni karakana ya shetani. Usipompa kazi mwanao, atapewa kazi na shetani.
Leo watoto wetu wamepewa kazi za kutosha na shetani. Ushoga wao, bangi wao, uzinzi wao, ulevi wao, uchangudoa wao, wizi wao, utapeli wao. Ni watoto wadogo lakini wanauzoefu mkubwa katika mambo mabaya.
*Tuwanasue watoto wetu kwenye mikono ya shetani kwa kuwafundisha uwajibikaji. Tutengeneze mazingira rafiki ya watoto kushiriki hata kazi za nyumbani.
Mfundishe mwanao kutandika kitanda chake akiwa bado mtoto. Asipojifunza utotoni ukubwani hataweza kutandika kitanda. Ukiingia chumbani utadhani kuna upekuzi wa polisi ulipita, kumbe chumba cha msela😄😄. Ukimuuliza atakwambia ndiyo geto la kiume!😄😄
Narudia tena. Usipowapa watoto wako kazi za kufanya, shetani atawapa kazi. Kazi za shetani ni nyingi. Hata pale mgeni anapokuja nyumbani na watoto wako wanaanza kumparamia, mara kumpanda mgongoni, mara mtoto kachukua simu ya mgeni anataka aangalie katuni au acheze game na analia kabisa, mama yake unacheka tu😄😄. Haya ni madhara ya watoto kukosa kazi.
Au unakuta mama ana duka la reja reja, katoto kake kanashinda dukani kanarandaranda kama kumbikumbi. Mteja ukienda kununua katoto kanaanza kukuganda ukanunulie soda, mara bigboom, mara juisi, mara biskuti, mara nini! Na mama anaangalia tu hasemi. Kwa kuona aibu unakanunulia maana hakatoki. Utadhani kanakudai😄. Hii ndiyo kazi ya shetani.
Lakini pia wafundishe watoto wako namna ya kujikita katika kazi moja mpaka ikamilike ndipo wahamie kwenye kazi nyingine. Wawe na utamaduni wa kufocus.
Watu wengi wazima leo hii wakianza jambo hawalimalizi, wanahamia kwenye jingine mpaka wanakufa ni bure kabisa.
Mfundishe mwanao kuweka kando mambo yote yanayoweza kuingilia umakini wake. Asifanye assignment huku anaangalia TV.
Mjengee utamaduni huo anapoanza kufanya assignment anazima TV mwenyewe bila kushurutishwa.
Wafundishe watoto wako kuchapa kazi badala ya kulalamika. Mtoto akilalamika mpe mboko. Moja ya sababu kubwa inayofanya watu wanashindwa kufikia malengo yao na kukosa furaha ni kulalamika.
Unapolalamika unakwepa wajibu wako. Unazuia uwezo wako wa kutatua matatizo. Unataka watu watende kwa niaba yako. Unaziba nafasi ya kujifunza katika kipindi unachohitaji mno kujifunza.