Usipoteze muda kubembeleza watu

Usipoteze muda kubembeleza watu

Joined
Nov 6, 2016
Posts
77
Reaction score
271
Na Comrade Ally Maftah
KING OF ALL SOCIAL MEDIA

Moja kati ya makosa nuliyowahi kuyafanya miaka kadhaa iliyopita ni kubembeleza watu wanielewe, kumshawishi mtu kwamba ninafanya kitu sahihi, nakumbuka siku naamua kwamba sitaki tena kuajiriwa na nimeamua kujisimamia mwenyewe na kuingia katika harakati za kijamii hakuna aliyenielewa, ilikuwa 2020, nilikuwa Teritory Sales Manager Airtel - Makambako Territory, hakuna aliyenielewa si marafiki, ndugu na wafanyakazi wenzangu, nakumbuka kauli ya bosi wangu mmoja alisema sintofika mbali nikamwambia kwa sababu wewe si MUNGU baki na akili zako za matope ukifikiri kila mtu anataka kuajiriwa.

Ilikuwa ni maamuzi mazito na matamu sana kwangu, nilishinda hofu, nikasonga mbele.

AKILI MBAYA NI KIMBEMBELEZANA KATIKA DUNIA HII INAYOKWENDA KASI YENYE WATU ZAIDI YA BILIONI NANE
Kuna watu wanafikiri wao wasipokubaliana na harakati zako pengine utaacha au hautofanikiwa, wanajikita kwenye kutoa maoni maoni na ukiwaambia ushauri wako siutaki wanaanza kulia lia.

Brother and Sisters mtu hakutaki achana nae asipoteze nguvu yako, asiyekutaka hakutaki hata umwelezee nini, deal na wanaokupenda hata kama ni wawili tu hao ni wengi wataita wenzao.

NDIMI
Comrade Ally Maftah
KING OF ALL SOCIAL MEDIA

20240524_105007.jpg
 
.
 

Attachments

  • Screenshot_20240524-145639_Instagram.jpg
    Screenshot_20240524-145639_Instagram.jpg
    540.6 KB · Views: 4
Back
Top Bottom