Usipoweza kuutoa Uzungu kwenye Ukristo na Uarabu kwenye Uislam, huwezi kumjua Mungu

Usipoweza kuutoa Uzungu kwenye Ukristo na Uarabu kwenye Uislam, huwezi kumjua Mungu

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Kwa wakristo angalau watakuwa na kazi nyepesi kuliko waislam katika hili.

Mungu ni Mungu wa binadamu wote. Ili umuelewe vizuri na umfaidi inabidi utoe uarabu na uzungu kwenye Biblia na Quran ndio angalau utaanza kumfaidi.

Mungu sio wa wazungu, hata wao walikuwa wanaabudu mapangoni kama wasandawe. Mungu sio wa waarabu hata wao walikuwa wanaabudu majini, vimondo na mapangoni kabla hata ya vuguvugu la uislam.

Uhuru wa kiroho unaanza utakapotenganisha dini na kabila, au lugha.

Ni hayo tu.

Mtumishi Matunduizi.
 
Uko sahihi , ishu ni vile akifanya muarabu wanatukanwa waislamu wote ,waarabu wana mila zao za miaka kenda hata wazungu ...Kama unataka kujua dini usifuate watu soma maandiko .
 
Waislam hujiona waarabu na huwaona waarabu n watakatifu kumbe hakuna watu wabaguz roho mbaya kama waarabu. Ajabu waislam huwaona wakristo kama wazungu ktu ambacho si kweli ndo maana wazungu wao wako waz sn mambo yao na huyatetea mfano ushoga wao wamejiweka waz sasa humu waislam hutukana wakristo n mashoga ksa wazungu, twende kwa waarabu je mashoga wapo au hawapo jbu n wapo tena uwenda n wengi kuliko huko kwa wazungu bt sheria zao znawabana wanajficha huku kwetu ambako kuna waislam wengi bs na ushoga upo kwa wingi nenda zanzibar, tanga, dsm utagundua hlo.
 
Dini pendwa bongo zote zimeanzia mashariki ya kati. Kwa hiyo huwezi kuitenga influence ya Watu wake katika kuihifadhi na kuieneza duniani..
 
Kuna nabii yeyote wa dini hizo alikuwa muafrika,.....kama Kuna mtu anamjua anitajie?
Nb.achana na wakina mwamposa
 
Dini sio FACT

Kwa 80% Ili mtu kuamini imani ya dini fulani huwa ni matokeo ya vitu vitatu

Historia
Geografia na
Makuzi/malezi

Dini imekua ni mapokeo ya kitamaduni zaidi kuliko kuchagua na kuamua based na FACT

Ukizaliwa Iran na wazazi wa Iran kwa kiasi kikubwa utaishia kuwa Muislam tena wa madhehebu ya Shia
Ukizaliwa na wazazi Jew pale Tel Aviv utaishia kuwa Jew
Ukizaliwa China utaishia kuabudu dini za kichina kama vile Mtoto wa wazazi wahindu pale Tamil ataishia kuwa Muhindu

Nje ya hizo tamaduni za kimapokezi hakuna MUNGU mmoja........ Kuna “miungu” kulingana na mazingira ya sehemu husika
Na kwa bahati mbaya sana hizi dini zililetwa kibabe na zikaua “miungu” yetu kwa kuita ni imani potofu
Lakini ukweli ni kwamba hakuna MUNGU ila kuna tamaduni za imani ya Mungu
 
Back
Top Bottom