Usipumbazwe na muonekano wa nje, mahusiano yanaendeshwa zaidi na mfanano wa ndani

Usipumbazwe na muonekano wa nje, mahusiano yanaendeshwa zaidi na mfanano wa ndani

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
TANBIHI: Andiko hili ni kwa ajili ya watu wanaotaka wenzi kwa ajili ya kuishi hivyo kama lengo lako ni kula na kuacha huna uhusika wako hapa.

Mvuto wa nje ni sehemu muhimu sana kwenye mahusiano kwa sababu itakufanya uwe na hisia dhidi ya umpendaye na pia utakuwa huru kutembea naye na kumtambulisha kwa rafiki zako mpaka kumchapisha( post) mitandaoni bila hofu yoyote 😊

Lakini ikiwa hicho tu pekee ndio kigezo namba moja basi mahusiano ya muda mrefu yatakushinda kwa sababu mkianza kuishi pamoja au kuwa karibu sana kitachoongoza mahusiano yenu kwa asilimia kubwa ni mfanano wenu wa ndani na sio wa nje tena.

Ni ngumu kukubali kuteswa na tabia yake nawe ukawa zuzu kwa sababu tu ana umbo zuri, Mwanya , nywele nzuri na mengine yanayopamba uzuri wa nje ila ni rahisi kuvumilia nywele zake za kipili pili lakini tabia yake ni njema na mnyenyekevu.

Mfanano wa ndani ni kuanzia tabia mpaka mitizamo na hapa ndipo upendo na uvumilivu upo kwa sababu mnakuwa wa moja kwenye malengo mpaka mafanikio ya nje.

Kuna muda huwezi kula uzuri wake ukashiba ila utahitaji ufahamu wake akushauri ili mpate pesa ya kulipa kodi na kuendesha maisha kisha ndio mje kuburudika na uzuri wa nje.

Mambo yakichanganya kuna muda hutoona thamani ya uzuri wa nje bali utahitaji uwezo wake tu kufikiria au tabia yake njema ili ushibe.

Kaulize waliovutiwa tu na muonekano wa nje bila kujali haiba ya ndani ni wachache walibahatika ila wengi wao hawafurahii tena mwanya wala macho ya kungu bali wanakiona cha moto kwa sababu kuna zaidi ya muonekano yanahitajika ili kuleta upendo wa kuvumiliana.

Uzuri wa nje sawa ila akili pia ziwepo na haiba nzuri ya ndani

#Mwanasayansi Saul kalivubha
#Fikia Ndoto zako.
 
Ukiendekeza sana zinaa Demu ukishampata ndo unaanza kuona kasoro zake unaanza kushangaa hivi huyu anatembeaje akitafuna moyoni unasema hee hivi huyu yukoje

Ndo maana sitaki mademu nataka kuja kuwa mtu mwema kwa mke wangu
 
TANBIHI: Andiko hili ni kwa ajili ya watu wanaotaka wenzi kwa ajili ya kuishi hivyo kama lengo lako ni kula na kuacha huna uhusika wako hapa...
Ulivhoongelea vyote vinaiuwa compiled na kuitwa chemistry, kuendana kimitazamo, kimawazo, hata baadhi ya tabia

Mkishindwana hapo, hata awe na pesa au muonekano mzuri kiasi gani hamto dumu
 
Hadi mbingu imeitikia
Hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah hallelujah
 
🔥🔥🔥🔥
 
Back
Top Bottom