TAIFAKWANZA
Senior Member
- Apr 20, 2013
- 162
- 67
Salaam wana JF.Poleni kwa majukumu na mahangaiko ktk michakato ya maisha ya kila siku.Mwenzenu nimekuwa na wasiwasi juu ya usiri mkubwa unaofanywa na serikali juu maslahi halali ya watumishi wa umma hasa walimu ambao mpaka dakika hii hawajui viwango vyao vipya vya mishahara kwa mwaka mpya wa fedha 2013-2014.Hali hii imewafanya walimu kupoteza molari wa kazi licha ya shule nyingi kufunguliwa mwezi huu.Si hilo tu lipo swala la malimbikizo ya mishahara kutolipwa pamoja na upandishwaji vyeo kufanyika kwa upendeleo mkubwa.Ningeomba kama kuna mwenye taarifa sahihi za waraka mpya wa mishahara mipya basi atujuze ili walimu wetu wa tz wajiandae kufanya kama wa huko Kenya.
Nawasilisha.
Nawasilisha.