Usiruhusu mwanaume kuhamia kwenye nyumba yako uliyojenga kwa jasho lako

Usiruhusu mwanaume kuhamia kwenye nyumba yako uliyojenga kwa jasho lako

Kasiano Muyenzi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2018
Posts
13,858
Reaction score
22,729
Mwanamke Usiruhusu Mwanaume Kuhamia Nyumbani Kwako...

Ukiamua kuolewa usimruhusu ahamie kwako, hata kama unamiliki jumba la kifahari katika soko la juu halafu huyo jamaa anaishi katika nyumba ndogo ya kupanga, ni heri ujishushe daraja na utoke kwa jumba lako la kifahari na uhamie katika kijumba chake hicho muishi hapo hadi mnunue au mjenge nyumba yenu pamoja.

Kuna sababu tatu za kutomruhusu ahamie kwako …

1. Mwanamume anayehamia kwenye nyumba ya mwanamke hukimbia wajibu.

Kwa kawaida mwanaume anayejua wajibu wake huchukua hatua kabla ya kuoa.

Hutayarisha makao ya bibi-arusi wake kabla ya kumpata huyo bibi-arusi.

2. Ikiwa unaweza kumudu kumiliki nyumba halafu mwanaume unayeishi naye hawezi kumudu kumiliki nyumba basi yeye sio saizi yako.

Akihamia kwenye nyumba yako ipo siku mtaingia katika ligi ya kupigana juu ya nani anayedhibiti nyumba.

Hivyo achana naye mwache aende akapate mwanamke wa saizi yake.

3. Ikiwa mwanamume atahamia nyumbani kwako, matarajio yake makuu ni kulelewa na wewe, atakufanya uwe mtoaji wake kwa kila kitu. Muda si muda, hutamheshimu tena, yeye pia hata kupenda tena.

Katika dunia ya sasa wanawake hawawezi kujisalimisha kwa wanaume ambao hawatoi.

NB: ujumbe huu ni kwa wanawake wote ambao hawajaingia ktk ndoa, ila kwa wale waliopo ktk ndoa na wanaishi na hao wanaume majumbani kwao huu ujumbe hauwahusu, wakomae tu na waume zao wazembe.
 
Ila wanaume wawaruhusu tu kuamia kwenye nyumba zao walizojenga kwa jasho lao... jenda binafs sana hiyo KE

Tutawanyanyasa na sisi na Mali zetu itakuwa mnawanyanyapaa sana wanaume wenzetu wasiokuwa na kitu kwa ubinafsi wenu
 
Uzi huu nia yake ni kuwaongezea wanawake confidence ya kuwa wachoyo na wabinafsi zaidi.

Katika umri wako hujui tofauti ya kuoa na kuolewa?

How old are you?
 
Uzi huu nia yake ni kuwaongezea wanawake confidence ya kuwa wachoyo na wabinafsi zaidi.

Sawasawa 👍
 
Katika umri wako hujui tofauti ya kuoa na kuolewa?

How old are you?

Mjinga et unajiita kambi ya Fisi alafu mimi najiita jina langu lenyewe kabsa alaf unaniuliza mimi umri wangu alaf unaniuliza nimewahi kuoa au?

Em badili huo utoto kwanza wa kujiita majina ya vikundi vya kina dada mashauzi alaf njoo tena na maswali yako nguruwe pori wewe Mbwa kambi ya fisi mbuzi kavimba.. tafuta shughuli ya kufanya
 
Uzi huu nia yake ni kuwaongezea wanawake confidence ya kuwa wachoyo na wabinafsi zaidi.

Siyo hivyo mkuu, nia ya uzi huu ni kuweka sawa uwajibikaji ktk ndoa, mwanamume akiwa kama kichwa lazima apambane kiume awe na nyumba au ashirikiane na mkewe wajinyime wapate hela ya Kujenga wakiwa ktk ndoa.

Kinachopingwa ktk huu uzi ni "mwanaume kuhamia kwenye nyumba ya mwanamke" hii haifai kabisa.
 
Mjinga et unajiita kambi ya Fisi alafu mimi najiita jina langu lenyewe kabsa alaf unaniuliza mimi umri wangu alaf unaniuliza nimewahi kuoa au?

Em badili huo utoto kwanza wa kujiita majina ya vikundi vya kina dada mashauzi alaf njoo tena na mashwali yako nguruwe pori wewe Mbwa kambi ya fisi mbuzi kavimba.. tafuta shughuli ya kufanya
Mjinga mwenyewe
 
Back
Top Bottom