Usisaidie masikini, acha wafe

Usisaidie masikini, acha wafe

Basi endelea kukaa hapo kwa shem wako Samia atakujaza mipesa tele
Na ndo inatakiwa hivyo hata kulingana na mujibu wa katiba ni haki yangu kukaa kwa dada yangu na ni haki yangu Samia kunijaza mipesa
 
Sawa.

Kila mtu atabeba mzigo wake, pengine hii bado hujaijua vyema.
Hiyo ndio Kanuni.

Kila mtu apambane na Hali yake.
Kama aliyemuumba au aliyetuumba ameshindwa kutusaidia unafikiri wewe binadamu utaweza.

Mungu anamaana zake kuiacha Dunia iwe hivi ilivyo.

Hata hivyo sitaki kubishana na mtu hapa.

Kama hujajionea basi omba uzima utanielewa siku moja
Mungu hupitisha msaada kupitia kwa watu.
Unapomhurumia masikini unamkopesha Mungu,yeye anawategemeza hao watu..
Iko hivyo mkuu.

Wala hatubishani bali tunatoa mawazo,au uzi wako hauruhusu kupokea mawazo tofauti na uliyoandika wewe?
 
Mungu hupitisha msaada kupitia kwa watu.
Unapomhurumia masikini unamkopesha Mungu,yeye anawategemeza hao watu..
Iko hivyo mkuu.

Wala hatubishani bali tunatoa mawazo,au uzi wako hauruhusu kupokea mawazo tofauti na uliyoandika wewe?


Nipo tayari Mkuu na ndio maana nimeuweka hapa.

Ila hiki nilichoandika ni kitu kikubwa ambacho kukitambua yakupasa utumie zaidi akili kuliko hisia.

Huwezi msaidia masikini ukabaki salama.
Labda umsaidie ili nawe ujipatie faida kutoka kwake
 
bila kukupesa watu masikini wakutupwa wakipewa nafasi huwa wanafanya maajabu makubwa sana katika taasisi na nyanja mbalimbali, hata mashuleni fuatilia vizuri utaona mayatima wanavyoperform vizuri sana na wana nidhamu ya juu sana....

Naona umefananisha umasikini na ushamba kwasababu ukimsomesha mtu mshamba na akajanjaruka, ataanza kweli kuwa na tabia za ajabu, lakini ukimsomesha masikini atakulipa fadhira na ataweka mazingira yawewe kuendelea kumuamini....

Nimejibu kwa kuzingatia muktadha wa mada, ila najua unaweza kuwa umemaanisha vitu vingine kabisa kama fasihi inavyokupa uwanda mpana......
Vp kuhusu uongozi wakipewa mamlaka??
 
Una maana kwa kuwa Mungu ndie kawaumba hao masikini basi ni yeye anajua watakula nini. Tazama ndege wa angani wanakula na kushiba na hawana shamba.
 
Maandiko ya vitabu yanatwambiaje? kumsaidia Maskini au tumuache afe kwa njaa na kiu?
 
Back
Top Bottom