Usisaidie masikini, acha wafe

Usisaidie masikini, acha wafe

3. USIMPE MASIKINI UONGOZI
Kumpa masikiniuongozi ni kumpa shetani usukani wa kuwaongoza. Masikini ni mtu wa visasi kama alivyo shetani. Masikini anataka kusikilizwa yeye tuu kama Mungu, huyo Mungu mwenyewe ameacha uhuru. Masikini kuua ni kitu cha kawaida. Ukimpa masikini uongozi ni lazima vifo viwepo.
Ni kweli kabisa, hapa Watanzania tumeshuhudia kwa macho yetu.
 
Matajiri wengi ni
Wachawi
Wanafiki
Walozi
Wachoyo
Wadhulumu
Hujihesabia haki kuliko wengine
Waabudu shetani
Hawatoi sadaka kamili kwenye ibada, kumbuka yule mjane masikini ambaye YESU mwenyewe alisema ametoa sadaka kubwa kuliko wote waliotoa
Wana dhambi nyingi ndiyo maana hata YESU alihubiri kwamba ni rahisi ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuuona ufalme wa MUNGU nk nk
 
Mkuu, mimi mpaka leo siamini katika mtu aliyekulia kijijini au katika familia maskini. Yaliyonikuta najua mimi kupitia aina hizo za binadamu.
 
Mabeberu wanawapa madawa chanjo na bado mnawatukana lkn hawaachi, unatakiwa uangalie great cause sio emotional satsfication,km unamsaidia mtu ili akunyenyekee umfanye chawa bora uache tu,wanaotoa msaada wengi wanaangalia impact to humanity sio individual personality ya unayemsaidia,
Wanatoa misaada Ili wafanikiwe
 
Matajiri wengi ni
Wachawi
Wanafiki
Walozi
Wachoyo
Wadhulumu
Hujihesabia haki kuliko wengine
Waabudu shetani
Hawatoi sadaka kamili kwenye ibada, kumbuka yule mjane masikini ambaye YESU mwenyewe alisema ametoa sadaka kubwa kuliko wote waliotoa
Wana dhambi nyingi ndiyo maana hata YESU alihubiri kwamba ni rahisi ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuuona ufalme wa MUNGU nk nk

Hii ni nadharia tu, uchawi ni imani na sio KILA mtu uiamini,hizo element zingine ni tabia personal
 
USISAIDIE MASIKINI; ACHA WAFE

Na, Robert Heriel

Umasikini ni laana. Huwezi kuwa masikini kama hujalaaniwa. Ukiona wewe ni masikini jua tayari unalaana, ukiona ukoo wenu ni masikini jua koo yenu mnalaana. Ukiona kabila, taifa au bara lenu ni masikini basi fahamu kuwa hiyo ni laana. Huu ni ukweli mchungu.

Mimi ni masikini nafahamu kuwa nimelaaniwa. Siwezi kujidanganya kuwa ati umasikini wangu ni mipango ya Mungu, huko ni kujifariji. Umasikini ni laana, nimelaaniwa jamani, jamani masikini wenzangu tumelaaniwa, tuache kujifariji.

Ukitaka kujua umasikini ni laana angalia jinsi masikini wengi 90% tulivyo na roho mbaya, wengi tuna roho ya husda, wengi hatupendi maendeleo ya wengine, wengi tuwashirikina na wachawi, wengi tukisaidiwa hatuna shukrani, yaani masikini ni mashetani wenye vibali vya kufanya uovu duniani.

Kama kuna mistake utakayoifanya kwenye maisha, ni kusaidia masikini. Ndugu yangu, hata umuone masikini anakufa njaa hapo usimsaidie, muache afe, jitie kihere here kumsaidia yatakayokupata mimi simo.

Ni bora umpe hicho chakula mbwa wako usiku atakulinda. Bora uwape kuku hicho chakula utakula mayai yake. Lakini sio masikini, masikini kumsaidia ni kumsaidia shetani. Huwezi msaidia mtu aliyepewa laana na Mungu hata siku moja. 90% ya masikini wanalaana ya asili, iwe ni mimi au wewe, au yule ilimradi ni masikini basi usitusaidie.

Masikini wanaroho nzuri wakiwa wanashida ya kukuomba jambo fulani. Masikini ni wanafiki sana. Utakuta yanakuchekea na kukusifia lengo ni kukutapeli. Masikini wanajua kulia lia wakiomba mkopo, bahati nzuri kwa masikini wamepewa kauli thabiti ya kushawishi kama shetani ili uingie kingi. Ukijiloga kumkopesha utaipata fresh ya shamba. Utadai na kudai, limasikini litakuwa halipokei simu yako, halijibu sms zako, mwishowe litaku-block. Hahahahah! Sicheki kama mazuri lakini hayo ndiyo mambo yetu sisi masikini tuliojawa na laana.

Masikini usimsaidie.
Masikini usimsomeshe
Masikini usimpe kazi
Masikini usimuoe wala kuolewa naye. Kuoa masikini ni kuoa shetani na ukoo wake. Kisha utazaa matoto yenye roho za kishetani
Kumsomesha masikini ni kuyasomesha mashetani ili yazidi kutenda maovu.
Masikini usimkopeshe
Ukimpa kazi masikini ni kumpa shetani nguvu ya kupata kipato atazidisha maovu yake. Jamani jamani! Ngoja mtanielewa tuu! Bahati nzuri wengi wetu sisi ni masikini hivyo ni rahisi kuelewana, hata uwe kichwa ngumu.

Utakachoweza kumsaidia masikini ni kumzika siku akifa tena uchimbe shimo refu la futi ishirini, ulifukie na mchanga, huo ndio msaada pekee wa kumpa masikini ambao hautakuumiza lakini msaada mwingine wowote ule lazima ile kwako tuu.

Ninachowapendea matajiri hawawapendi masikini kabisa. Huwezikuta tajiri anamualika masikini nyumbani kwake. Matajiri wanajua kumuita masikini nyumbani ni kumkaribisha shetani ndani ya nyumba, mikosi na mabalaa yataandama nyumba hiyo mpaka wakome. Ndio maana majumba ya matajiri huwezikuta watu wanaingia ingia na kutoka.

Masikini hawapendi utulivu, utasikia makelele muda wote, huyu kawasha singeli, huyu taarabu, huyu ngoma ya Lugwadu yaani kelele tuu. Mara vigoma, sijui vigodoro, mtaa mzima matusi, yaani umasikini ni ushetani. Mitaa ya masikini ni kama kuzimu.

Uchafu kila pahala, nzi, mende, kunguni yaani vangala vangala. Masikini hawajipendi kwa nini wewe uwapendi.

Masikini unachoweza kumsaidia ni kumdhulumu, iwe pesa na vipesa vyake. Ukifika nyang'anya shamba lake, sijui kiwanja, akilia masikini kilio chake ndio baraka zako, niamini mimi.

Watu wote waliowadhulumu masikini walibarikiwa, kwa maana kumuangamiza mwenye laana ni kutafuta baraka kwa aliyempa huo umasikini. Lakini kumsaidia mwenye laana ya umasikini ni kupambana na aliyempa hiyo laana. Watu wote waliowasaidia masikini kwa nia njema walikufa vifo vibaya tena waliuawa na hao hao masikini.

Msaidie masikini kwa nia mbaya lakini mwonyeshee unania nzuri. Nafikiri mataifa makubwa yote hufanya hivyo. Wazungu wanajifanya wanania njema ya kuwasaidia masikini wa Afrika lakini ukweli ni kuwa wanawadhulumu kwa upande wa pili.

Msadie masikini shilingi 10 kisha jipatie shilingi elfu moja. Hapo masikini atakuheshimu, na utabarikiwa miaka nenda rudi wewe na ukoo wako. Matajiri wakubwa duniani, hata hapa nchini, matajiri wakubwa wote huwadhulumu masikini kwa kuwalipa mishahara ya misukule. Matajiri wanazidi kuneemeka wakati masikini wakizidi kuwa fukara na wanashangilia.

Ukitaka kushangiliwa na masikini basi mdhulumu kwa kumsadia ukiwa na lengo la kumnyonya kama agenda ya siri. Yaani humsaidii kutoka moyoni. Huoni huko kwenye makanisa ya siku hizi. Manabii na mitume wanavyopata utajiri. Wao wanajua siri hii; masikini hasaidiwi bali anapaswa kudhulumiwa ili azidi kuwa masikini asizidishe uovu wake.

MADHARA YA KUWASAIDIA MASIKINI

1. UKIMSOMESHA MASIKINI ATAFANYA HAYA;
Masikini nimeshakuambia hasomeshwi. Ukimsomesha cha moto utakipata. Akishamaliza shule atajiona yeye ndio yeye. Kazi kudharau wengine, kuwaona hawafai, Hatatumia elimu yake isaidie jamii yake. Badala yake elimu yake itaingamiza jamii. Kwanza atabadili mitindo ya maisha kuanzia mavazi, kuongea, atabagua kazi na kudharau baadhi ya kazi. Atataka mishahara mikubwa hata mara tatu ya watu wengine.

Masikini apike visheti, masikini auze mabumunda, auze kababu thubutuu! Masikini akipata matako hulia Mbwataa! Huoni masikini waliosomeshwa hapo mtaani?

Angalia matajiri waliosomeshwa, embu angalia watoto wa kihindi, kizungu, kiarabu, amemaliza shule utamkuta kwenye mgahawa anauza sambusa, nyama choma, piza, baga, dereva, fundi magari.

Usimsomeshe masikini, utaishia kudharauliwa.

2. USIMPE KAZI MASIKINI
Masikini ukimpa kazi utakuwa umeamua kumpa shetani nguvu ya kiuchumi kufanyia maovu. Atazilewea hizo hela bila akili, ataiba wake za watu kwa kuwahonga kimshahara chake, atatia watoto wa watu mimba na kuwatelekeza, kazini atakuwa na nyodo na dharau kwa wateja wake, atadharau wasio na kazi na kujiona Mungu mtu.

Masikini akipata kazi atasahau hata marafiki zake aliosota nao kipindi hana kazi. Masikini akipata kazi anaweza muacha hata mchumba wake au mke/mume wake kisa sasa anajiweza. Masikini ndiye shetani anayeombewa kanisani na misikitini kila siku.

Usiombe Limasikini ndio liwe polisi, hahahah! Mbona utakoma ukiingia kwenye anga zake. Litakupa kesi ya kubambikiza ili ulipe pesa, litakuomba rushwa, litakupiga bila sababu kama sio kukuua kabisa, yaani jitu ni masikini alafu ulipe kazi ya upolisi hahaha! Umechanganyikiwa wewe. Au ulipe kazi ya uhakimu, yaani hapo umekabidhi mahakama kwa shetani.

Umpe masikini kazi ya udaktari, litaiba madawa na kuuza, litauza viungo vya watu, litaua watu kwa makusudi tuu, yaani tafrani

Limasikini liwe Lichungaji, hahaha! Mara litajiita nabii, litajiita mtume, yaani majina yote yenye sifa, unajua masikini wanapenda sifa sana kama Shetani. Sasa angalia kwenye sadaka litakavyowapiga, na ninyi kwa vile limetumia mbinu ya kuwachota kisaikolojia na kupewa psychological effects ambazo wengi huziita imani, utajikuta unatoa pesa ukiamini kuwa siku moja nawe utakuwa tajiri wa majumba na magari ya kifahari. Hahahah! Hayo yanaitwa matatizo ya kisaikolojia. Kumbuka masikini humuwezi kwa mdomo, ni kama shetani, ni muongo balaa.

3. USIMPE MASIKINI UONGOZI
Kumpa masikiniuongozi ni kumpa shetani usukani wa kuwaongoza. Masikini ni mtu wa visasi kama alivyo shetani. Masikini anataka kusikilizwa yeye tuu kama Mungu, huyo Mungu mwenyewe ameacha uhuru. Masikini kuua ni kitu cha kawaida. Ukimpa masikini uongozi ni lazima vifo viwepo.

KAINI mtoto wa kwanza wa Adamu alikuwa ni Masikini lakini Mungu alimpa uongozi(uzaliwa wa kwanza). Umasikini wa KAINI ulitokana na kutokuwa mwaminifu katika kutoa dhabihu, alikuwa akimpunja Mungu, wakati mdogo wake alikuwa mwaminifu hali iliyofanya Mungu ambariki(akawa tajiri). Jambo hilo limfanya KAINI kuwa na wivu mbaya kwa mdogo wake.
Kumbuka uchoyo wa kutoa dhabihu kwa Mungu ndio chanzo cha umasikini wake. Masikini wote duniani ni wachoyo. Mbili, wanawivu mbaya, mwisho huwa wauaji.

Kaini akaamua kumua mdogo wake kisa utajiri(kubarikiwa) yeye ni masikini na ndiye kiongozi kwani ni mzaliwa wa kwanza.

Masikini akipewa uongozi uwe wa kifamilia, kijamii, kikampuni, au Kinchi hakika hakuna namba mtakazo acha kuzisoma.

4. USIOE/KUOLEWA NA MASIKINI
Kuoa/kuolewa na masikini ni kuoa/kuolewa na shetani. Hakuna rangi hutaacha kuziona. Umalaya yeye, ugomvi yeye, ubahaili yeye, wivu yeye, vizinga yeye, uchawi yeye, ulevi yeye, dharau yeye, matusi yeye, sasa hapo utasema unaishi na binadamu? huyo ni shetani, hakuna binadamu wa hivyo.

Masikini hupenda kupendelewa sana. Ukioa masikini unatafuta balaa. Ukisaidia kwenu kelele, ukisaidia kwao kimya, ndugu zako wakija kelele, ndugu zake wakija kimyaaa!

Wanaume masikini 90% wakianza kupata pesa huanza umalaya, na mara nyingi hufikiri walikosea kufanya uchaguzi kukuoa wewe. Ndio mashetani yalivyo.

Wanawake masikini 90% wakijiweza na kuwa na uchumi wa uhakika, huanza dharau, majibu ya shombo, vijembe hata wakati wa kiangazi utaviona, wengi hudai talaka kwa dizaini nyingi iwe kwa kusema au kwa matendo.

Usioe mwanamke/usiolewe na mwanaume masikini, hapo umechukua shetani ndani ya nyumba.

5. USIMKOPESHE MASIKINI
Masikini hakopeshwi. Kumkopesha masikini ni kumpa sadaka shetani. Kumsaidia masikini ni kutoa sadaka kwa Mungu. Yaani Ukiona umemkopa masikini ujue umezua balaa, kwanza unatafuta ugomvi, mbili unatafuta kufilisika kama umekopa kiasi kikubwa, tatu umedhamiria jamii ikuone wewe huna subira kwani muda wa kukurudishia hela yako utakapopita na hajalipa deni mtaanza kukimbizana. Masikini husikilizwa mbele ya baraza kwani uso wake ni wa huruma lakini moyo wa ibilisi.

Masikini anamaneno laini akikukopa, lakini utajuta ukienda kumdai, hutaamini maneno atakayokupa.

Masikini akikuomba umkopeshe 100,000 mpe elfu kumi mwambie huna pesa, na hiyo elfu kumi mwambie hutamdai. Hapo utapata baraka kwa Mungu kuliko umkope masikini laki moja ili akusajili kwenye timu zake za kishetani za kudaiana.

Hakuna tajiri anayeweza kumsadia masikini bila kujua atapata faida gani?
Hakuna Mungu atakayesaidia masikini bila kujua atapata faida gani?

Je wewe unamsaidia masikini bure ni nani kama sio mwendawazimu?
Tangu umeanz kusaidia masikini kuna lolote umelipata zaidi ya lawama, ugomvi, kukimbizana na hao hao masikini?

Masikini tulishapa laana kwa Mungu, kumsaidia masikini ni kupambana na Mungu. Kumuangamiza masikini ni kutafuta baraka kwa Mungu.

MUHIMU: Sisi masikini tubadilike, roho mbaya tuache. Tumuombe Mung atuondolee hii laana ya umasikini kwa maana sisi ni kama mashetani.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Zanzibar
Fikra mfu sana hizi.Anyway Kwangu Mimi kumsaidia Masikini ni ibada (For me, helping the poor is the kind of devotion).Kwa hiyo kila mtu na mtizamo wake.
 
Hakuna Tajiri wa kizungu anayekusaidia bila ya kupata faida.

Kanuni yasema; MPE kumi upate mara kumi(yaani Mia moja) Kama huelewi Basi.

Tangu lini Mzungu aliisadia Afrika, naomba unipe somo
Ahaa . Maendeleo ya Afrika ni products ya mkoloni,bila kutawaliwa tusingekuwa na maendeleo.Mfano Hapa Tza miji mikubwa imejengwa na wakoloni.
Wao ndio wameleta mifumo bora ya afya na elimu.
Mfano kama tukiutumia mfumo wa elimu wa mkoloni tutawaweza maliza tatizo la ajira.
 
Hizo ni hisia zako tuu ambazo wengi huziita Imani.

Imani ni uhakika wa mambo yatarajiwayo, hayana Kwa yasiyoonekana.

Ulimsaidia huyo Bibi Kwa kuwa na Imani utapata elfu 20? Jibu ni hapana.
Ulifanya Kwa hisia za huruma na wala sio Imani.

Wengi mnachanganya Imani na mihemko
Ila imework kwangu zaidi ya mara mia.
Hata leo nilimpa ombaomba 1200 nishapata simu ya dili najua hadi jioni nitakupa mrejesho ngapi nitapata.
Mwenyezi Mungu anasema "nijaribuni kama sitowabariki" Hata Luck Dube aliimba.God bless the hand that give."
Sasa tusipowasaidia masikini nani atawasaidia.
Maana Hakuna mwanadamu yeyeto ambae amewahi simama pekee yake bila kusaidiwa.
Saidia masikini upate heri na baraka tele.
 
Mungu anibaridi mwaka huu nimepanga kuagiza mashine china ya kutengeneza vigae na matofali fungani ya udongo kwa siku inatoa tofali laki moja na ishiriki. Kisha nitawagawia masikini wasio na makazi vijijini. Sababu najua wamekuwa ni masikini sababu hawana maarifa na pia roho za mababu ndizo zimewashikilia wengi wasiwe masikini.
 
Ila imework kwangu zaidi ya mara mia.
Hata leo nilimpa ombaomba 1200 nishapata simu ya dili najua hadi jioni nitakupa mrejesho ngapi nitapata.
Mwenyezi Mungu anasema "nijaribuni kama sitowabariki" Hata Luck Dube aliimba.God bless the hand that give."
Sasa tusipowasaidia masikini nani atawasaidia.
Maana Hakuna mwanadamu yeyeto ambae amewahi simama pekee yake bila kusaidiwa.
Saidia masikini upate heri na baraka tele.

Kama unasaidia ili upate baraka huo hauitwi msaada Bali biashara 😀😀😀

Bado hujaelewa pwenti yangu Mkuu.

Hakuna Binadamu atakayekusaidia pasipo ku-plan kupata malipo zaidi.

Ndio maana kwenye post nimesema Kama utasaidia basi Saidia 10 upate mara kumi.

Ahsante
 
Mungu anibaridi mwaka huu nimepanga kuagiza mashine china ya kutengeneza vigae na matofali fungani ya udongo kwa siku inatoa tofali laki moja na ishiriki. Kisha nitawagawia masikini wasio na makazi vijijini. Sababu najua wamekuwa ni masikini sababu hawana maarifa na pia roho za mababu ndizo zimewashikilia wengi wasiwe masikini.


Alafu Mungu ukimuomba hivyo hakupi🤣🤣. Kumbe hujui hata kanuni za kuomba.

Jenga Safina uingie wewe na Mkeo, na watoto wako, na wake au waume za watoto wako. Hiyo ndio kanuni😀😀

Ibrahim toka wewe na jamaa yako uende mpaka nchi nitakayokuagiza.

Lutu toka wewe na familia yako Kwa maana nchi hii nitaiangamiza Kwa Moto

🤣🤣
Bado pengine hujaelewa nature inahitaji nini.

Lakini utanielewa tuu
 
Kama unasaidia ili upate baraka huo hauitwi msaada Bali biashara 😀😀😀

Bado hujaelewa pwenti yangu Mkuu.

Hakuna Binadamu atakayekusaidia pasipo ku-plan kupata malipo zaidi.

Ndio maana kwenye post nimesema Kama utasaidia basi Saidia 10 upate mara kumi.

Ahsante
Achilia suala la biashara.Kusaidia ni uponyaji pia.
Healing the soul.Saidia mtu bila kutegemea kulipwa fadhila.
Kusaidia unafungua external world

Mzee wa fasihi burudika na hii kwanza.
 
Ahaa . Maendeleo ya Afrika ni products ya mkoloni,bila kutawaliwa tusingekuwa na maendeleo.Mfano Hapa Tza miji mikubwa imejengwa na wakoloni.
Wao ndio wameleta mifumo bora ya afya na elimu.
Mfano kama tukiutumia mfumo wa elimu wa mkoloni tutawaweza maliza tatizo la ajira.


😀😀😀

Nani kakudanganya Mkuu!

Umesoma History Kwa kiwango cha Ordinary ndio maana unahaki ya kusema hayo.
 
Achilia suala la biashara.Kusaidia ni uponyaji pia.
Healing the soul.Saidia mtu bila kutegemea kulipwa fadhila.
Kusaidia unafungua external world

Mzee wa fasihi burudika na hii kwanza.



KAZI yako sio kusaidia Mkuu.

Mungu ndiye kazi yake kufanya hivyo. Ndio majukumu yake hayo.

Huwezi msaidia mtu ambaye amekataa kusaidiwa na Mungu.

Masikini ni Yule asiye na miguu, mwenye kilema, kichaa na madhaifu mengine lakini kamwe usije ukajidanganya ukimsaidia mtu mzima mwenye akili timamu, viungo kamili ati Mungu atakubariki🤣🤣
 
😀😀😀

Nani kakudanganya Mkuu!

Umesoma History Kwa kiwango cha Ordinary ndio maana unahaki ya kusema hayo.
Ndio reality mzee ni bora wakoloni wangeendelea kuwepo tungekuwa mbali sana na kwa ustaarabu wa hali ya juu.
Mwafrika hana uwezo wa kuongoza Jamii na ikastawi.Hii ni nature ukishakuwa na chuki, ubinafsi,roho mbaya unajiconnect automatic na negative energy.Umasikini ni end product ya negative power. Ukimjua Mwenyezi Mungu na kuzijua kanuni zake huwezi kuwa masikini.
 
Ndio reality mzee ni bora wakoloni wangeendelea kuwepo tungekuwa mbali sana na kwa ustaarabu wa hali ya juu.
Mwafrika hana uwezo wa kuongoza Jamii na ikastawi.Hii ni nature ukishakuwa na chuki, ubinafsi,roho mbaya unajiconnect automatic na negative energy.Umasikini ni end product ya negative power. Ukimjua Mwenyezi Mungu na kuzijua kanuni zake huwezi kuwa masikini.
Samahani mkuu, wewe ni Young Lunya?
 
KAZI yako sio kusaidia Mkuu.

Mungu ndiye kazi yake kufanya hivyo. Ndio majukumu yake hayo.

Huwezi msaidia mtu ambaye amekataa kusaidiwa na Mungu.

Masikini ni Yule asiye na miguu, mwenye kilema, kichaa na madhaifu mengine lakini kamwe usije ukajidanganya ukimsaidia mtu mzima mwenye akili timamu, viungo kamili ati Mungu atakubariki🤣🤣
Neno masikini ni pana KILA mmoja ni masikini kwa tasfiri nyingine lakini kuu iliyozoeleka ni masikini wa kipato.
-masikini wa
.roho
. kipato
.viungo
.imani
.mawazo
Nk.
 
Back
Top Bottom