Usisaidie masikini, acha wafe

Hongera mkuu, umeongea ukweli kwa asilimia kubwa sana. Umasikini ni laana, hasa umasikini wa roho, maana masikini wa roho hata akipata matako hulia mbwata.

Kuna mazingira mtu ukiishi unaweza kurudi kuwa masikini, tena kuzidi uliowakuta, msengenyaji, mnafiki, mwizi, dhulmati dah.

Ila nini, wengi sisi ni masikini tu, jamii ya kitanzania imejaa masikini wengi mno.
 
Mada yako haina uhalisia wowote ni utumbo kwa kiasi kikubwa .

Wapo matajiri wamepambana wenyewe kutoka kwenye umaskini wakatajirika
Je njia walizopambana unauhakika siyo za kishetani?
 
Wanaofanya vizur ni asilimia 10 ndivyo nilivyomuelewa mwandishi.
 
Mkuu me nadhani umemuongelea mtu mshamba na sio masikini
Tafsiri ya maskini hajaipambanua vizuri sababu tabia alizoainisha zina reflect limbukeni by 100% ila umaskini unaanzia katika nafsi!

Wapo watu ni millionaires ila ndugu zao wanateseka na maisha ambayo ni very basic!

Ukiniuliza tafsiri ya mtu maskini nitakwambia ni yule mwenye roho ya choyo na husda! Huyu hata akiwa billionaire huwezi ona impact yake kwenye jamii ila mwenye roho ya kitajiri ni kinyume impact huanzia tokea kwenye level ya familia,ukoo mpaka kitaifa.
 
Masikini hata akipata, umasikini wake hauondoki akilini, kuna watu hawana pesa lakini ni matajiri, as hawana attributes za kimasikini, lakini masikini hata akipewa bado umasikini wake hauondoki.
Wewe ndio umeongea kile ambacho kilikuwa kichwani mwangu kwa wepesi zaidi.

Mtu mwenye rich spirit hata kama hana anakuwa hana tatizo na mtu. Na akiwa nacho ndio kabisaa yani wote mtafurahi. Wako positive mda wote!

Ila wenye roho ya kimaskini ndio wanakuwaga na attitude ya kilimbukeni tu. Hawa ndio wale anawaza apate ili awakomeshe akina flani..Ata strive kupata recognition akipata nafasi na sio kwa nia ya kusaidia kuwainua walio karibu nae bali kuwa oppress ili awe ni mtu wa kutukuzwa, ili akusaidie ni lazma umsujudie na msaada unaambatana na matangazo.Husda na choyo ndio vimeijaza mioyo ya hawa watu.

So kwangu tafsiri ya umaskini ina stem kwenye roho ya mtu. Haijalishi una hela au hauna ila umaskini upo rohoni. Binafsi naweza kuwa sina kitu ila siji count kama maskini sababu najua i have a rich heart na nikiwa nacho im good at giving a hand to others sibaguagi watu.
 
Elimu ndio ufunguo wa maisha,elimu uliyoipata ni maisha bora tosha.
Kilichobaki in utashi na udhubutu.
Ajira haitolewi kwa MTU asiye na utashi.ndo maana kuna kitu inaitwa USAHILI.

Kifo ndo jaji mkuu wa maisha yako.
 
Konyoko puzi sana nenda tume kaombe kugombea urais tukujaribu kwa miaka 5 ili uthibitishe ulichomwaga hapa😩😩😩
 
Kama ndivyo vp yule mwanamke wa kwenye Bible aitwae Esther??
 
Ndio

husikii alivyowaambia kesho yake, aliwaambia mmekuja leo tena kwa sababu ya chakula na sio neno la Mungu, yaani jana kwa vile walipewa samaki na mkate ndio maana siku iliyofuata wakaongezeka maradufu.
Brother Umejipanga Kila Kona[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Umeandika kwa ujumla hii mada yako.
Umaskini upo wa aina nyingi, umaskini uliondika ni kuhusu mali.

Kuna umaskini wa akili...unaweza kuwa tajiri wa mali(pesa, viwanja n.k) ukakosa utajiri wa akili....kama wewe hapo.

Eti zakayo alikua anatafuta kiki kutoka kwa Yesu...huo ni ulimbukeni...Yesu kwa mujibu wa maandiko ni Mungu na ana uwezo wa kusoma nia ya moyo wako.

Yesu mwenyew kwenye stori zake alisema siku itafika utaulizwa, mbona nilikua nakufa na njaa na ukanilisha....mathayo 25:35-40.

Jamani tusaidie maskini kwa moyo mmoja tuache huu upotoshaji.

Sharing is caring.
 
Sema ukiangalia watu ambao hawajapiga hatua ni wafitinishaji, wanaroga, wivu, wagombanishi, wajuaji, wanadharau wanajiitaga wao masikini jeuri, wana viherehere, yani muda mwingi wana , ukiongea nae muda mwingi anakistukia kama una mdharau,kwa kuwa hawana shughuli wanayofanya ni wasengenyaji wanapenda kuwasema watu vibaya ni wambea nk

Ni tabia iliyomo ndani mwao lakini silinganishi hiyo ni laana, Mungu hutupenda sisi sote na ndiyo maana akatuumba hawezi kutubagua, asili ndiyo imetufanya kuwemo wenye nacho na wasionacho wenye akili na wasionazo hatuwezi fanana kila kitu kuna watafutaji na wavivu sasa wavivu ndiyo wanaangukia kwenye umasikini, hizo tabia za masikini walizonazo ni kutokana na tabia tu zao za makuzi waliyoyapitia katika jamii au familia wanazoishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…