Hansss
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,370
- 2,723
Mkuu acha kuongopea eti domo kaanza mziki 2009' yaani kamwambie na mbagala ni za 2009? Au mwaka huo ndio ulianza kuzisikia nnLengo kuu la uzi huu ni kuweka historia sawa.Naomba sana mods msiunganishe na uzi mwingine.
Nadhani wote tunakubaliana kuwa EX hawaachani bali wanatengana tu kwa muda endapo mmoja akiamuwa kuliamsha dude basi kurudiana ni rahisi kama kumsukuma mlevi
Nimeamuwa kuweka sawa historia kwa sababu kumezuka katabia siku za karibuni naweza sema"kakijinga"Eti wanasema mashabiki/fans wa Alikiba ni wale ambao wanamchukia Diamond kwa sababu ya mafanikio yake na mashabiki wengine wanamchukia kutoka kwa waliokuwa ex wake.Hii ni kauli ya kujifariji na Coward. Kama umeanza kusikiliza mzika start 2010's sitashangaa uku support hiyo kauli....
Labda niwakumbushe.Alikiba alianza mziki rasmi mwaka 2005 kwa kupata collaboration kutoka kwa wasanii waliomtangulia kama Dully Syksi,EB by skills na wengine wengi.Mwaka 2006 aliaachia wimbo wake mwenyewe official song ulioitwa Cinderella,nyimbo was a mega hit kwani àliweza kuingia kwa miguu miwili katika tasnia ya bongo fleva. Baada ya hapo nyimbo zilizofuta zilikuwa ni hit songs kama vile Nichumu,Msela,Nakshi Nakshi,Njiwa,MacMuga,n.k.mwaka 2008 ilikuwa ni bahati kwake hakuna msanii ambaye hatamani kufanya kazi na legend kama R.Kelly hivyo kupitia project ya One 8 msanii alikiba alifanya kazi na Wasanii waliokuwa wanafanya vizuri kipindi hicho.Project hii iliweza kumtambulisha Alikiba kimataifa zaidi kuanzia Afrika and Europe,US. Nyota ya alikiba iling'aa sana miaka hiyo kabla ya kuachia ngoma ambazo zina hit hadi leo kama vile,Mapenzi yana run dunia,Single boy,My Every thing,na Dushelele.
Late 2009's aliacha mziki/kupumzika katika tasnia ya bongo flava.Kuanzia mwaka huu ndipo kizazi kipya cha bongo fleva kiliibuka wasanii kama vile Marlow,Barnaba,Amini na Diamond n.k waliibuka.
Kwa upande wa Diamond ni msanii anayejituma sana kwani tangu alipoanza rasmi mzika mwaka 2010 graph yake inapanda siku hadi siku.Ni msanii ambaye amepata mafanikio makubwa tofauti na alionza nao.
Kumbuka tangu Alikiba anaacha mziki kulikuwa na malalamiko ya chini kwa chini kwa blood fans wake.Kuna wakati alisikika akisema kati ya moja ya interview zake kuwa"kizuri kikikosekana kibaya kitakuwa kizuri"mwisho wa kunukuu.Hivyo tangu amerudi rasmi katika tasnia ya bongo fleva ameweza kurudisha heshima na uwezo wake wa awali.
NOTE;
Mashabiki wa Diamond walikuwa mashabiki wa Alikiba kabla ya kuacha kuimba so sishangai leo kurudi katika asili yao ya awali.Alikiba na Fans wake ni mtu na Ex wake.
Asante
great thinker
Sent using Jamii Forums mobile app